2026 FIFA World Cup - Special Thread

2026 FIFA World Cup - Special Thread

1000832068.jpg
 
Mkuu hata Mimi kiukweli naona France wako vizuri na wanaweza kuchukua World Cup hii, ila ukweli ni kwamba hawajapata changamoto kucheza na timu ngumu... Sasa hawa Sweden hata ukiwakabidhi Colombia si wanakula nyingi.. Hata wakikutana na Morocco wanapasuka vizuri tu...

France sana sana wako vizuri pale Mbele yaani Mbappe, Dembele, Olise na hao Madogo akina Doue na Barcola... Ila beki yao akija kukutana na moto wa wanaume tutakuja kuongea lugha moja, Siku wamekutana na Messi ameamka na mashetani yake hao akina Kounde, Upamecano eti Digne watabondeka vibaya.

Kuhusu Portugal wanaangushwa na Ronaldo anazurura tu uwanjani na pia hamna kocha pale..
Timu ngumu za kuipa changamoto France ni zipi?..
 
France wako vizuri hapo mbele, wakikutana na Argentina kwa hiyo back itakua piga nikupige kama ile ya fainali ya 2022.. France akijutana Argentina au Colombia ndo itakua kipimo sahihi maana tunamwona mkali anavyowafunga hao wachovu
Colombia sio haba....labda tuone na hao Argentina kama watafurukuta..
 
Sure kabisa nahisi ana deserve kuchukua kombe... Lakini pia hajakutana na Kipimo sahihi design ya timu kama Argentina hapo ndo tutajua panapovuja.. Maana wote aliowagonga ni tia maji sana.
Ila nahisia safari hii wananyanyua kwapa, pale mbele wako clinical sana, mbappe, Dembele, Barcola wakisaidiwa na Olisse ni habari nyingine, hata Argentina kwa staili hii wanaweza pasuka tu
 
Ila nahisia safari hii wananyanyua kwapa, pale mbele wako clinical sana, mbappe, Dembele, Barcola wakisaidiwa na Olisse ni habari nyingine, hata Argentina kwa staili hii wanaweza pasuka tu
Ni kweli mkuu, hata nao Ufaransa hizo Beki za Upamekano, sijui Kounde siku hiyo Messi amemka na Mashetani yake huoni km mtu atakua anapasuliwa kwake... Gonga nikugonge km ile ya 2022
 
Ni kweli mkuu, hata nao Ufaransa hizo Beki za Upamekano, sijui Kounde siku hiyo Messi amemka na Mashetani yake huoni km mtu atakua anapasuliwa kwake... Gonga nikugonge km ile ya 2022
Ila gonga ni kugonge ya safari hii, sioni kama Argentina atabahatika safari hii ni kweli eneo la ulinzi kuna tatizo lakini naamini pale mbele patasahihisha makosa ya ulinzi, they are deadly Infront of the goal, watu weusi wa maana kabisa
 
Back
Top Bottom