moudgulf
JF-Expert Member
- Jan 23, 2017
- 158,365
- 775,921
Jina ni Brazili 🇧🇷🇧🇷Hebu tuambie jina limembeba vipi brazil
1. Brazil 🇧🇷ndiyo nchi pekee waliotwaa taji 👑 mara nyingi, mara 5.
1. Brazil 🇧🇷 ni nchi ya kwanza kuchukua Ubingwa nje ya bara lake 1958- Sweden. Bara Ulaya.
2. Brazil 🇧🇷 Ni nchi pekee iliyoshiriki fainali zote tokea zilipoanzishwa mwaka 1930- 2026 (96yrs).
3. Brazil 🇧🇷 ndiyo nchi yenye wachezaji wengi wenye majina makubwa kwenye mchezo wa soka Duniani.
4. Brazil 🇧🇷 ni nchi pekee miongoni mwa nchi zilizotwaa kombe la Dunia ambayo hajachukua Ubingwa kwenye ardhi ya nyumbani.
5. Brazil🇧🇷 Ndiyo nchi inayopiga mpira mkubwa.
6. Brazil 🇧🇷 ni nyumbani kwa wachezaji wenye vipaji vikubwa walioacha majina yao kwenye WC pamoja nao ni Edson Arrantes do Nascimento 'PELE'
7. Brazil 🇧🇷Ndiyo nchi iliyoandaa fainali za mfano za mwaka 1950 baada kusimama kwa miaka 12 kwa sababu ya vita kuu ya pili.
Mechi ya Fainali ilyochezwa july 16 1950 kwenye uwanja wa Maracana lilishuhudiwa na mashabiki 173,850, ambao asilimia 95 walikuwa wenyeji (Wabrazil).
Idadi hiyo ya watazamaji haijawahi kutokea popote kwenye kumbukumbu za mchezo wa soka ngazi ya timu za Taifa au hata virabu, na hilo halitarajiwi kutokea miaka ya hivi karibuni.
Rekodi hiyo imeishi kwa miaka 76 sasa.
Kwa sababu hiyo, zipo nchi zikisikia rekodi hizi, zinapoteza mchezo kabla mechi haijaanza.