2025 na mbeleni

2025 na mbeleni

Sasa kwa nini watu wauhusishe uteuzi wa Bashiru na uongezwaji wa mihula?
Uteuzi wa Dr Bashiru unafuatia kifo cha Balozi Kijazi. Binafsi sioni maandalizi ya kubadili katiba. Laiti Balozi Kijazi (RIP) angefutwa kazi kisha nafasi ikajazwa na Dr Bashiru kidogo ningeungana na kwaya inayoimba mapambio ya maandalizi ya kufuta ukomo wa miaka 10.
 
Naona njaa imekupanda kichwani hasa mara baada ya biashara ya kubeba mabox kuota mbawa.

Hata kama wewe ni ngosha hupati uteuzi ng'ooo
 
Naona njaa imekupanda kichwani hasa mara baada ya biashara ya kubeba mabox kuota mbawa.

Hata kama wewe ni ngosha hupati uteuzi ng'ooo
We jamaa dizaini una njaa sana hadi unaishia kui project kwa wengine.

Nani kakuambia mimi nataka uteuzi?

Na sijui uteuzi wa nini/ wapi?

Nyumbu bana...
 
Ccm haitambi, bali madaraka ya urais yanayotumika vibaya kuteka watu, kuua wapinzani, kunajisi uchaguzi na uhayawani mwingine kama huo ndio yamayotamba. Kinachofanyika katika kuibeba ccm na kuifanya ionekane imara ni kiburi cha madaraka ya urais ya mwenyekiti wake. Kuna wakati Iddi Amin, Moi, Mugabe nk waliamini vyama vyao ni imara, sio kwakuwa kweli vilikuwa imara, bali yalikuwa ni madaraka ya viongozi hao kutumia vyombo vya dola kutoa upendeleo kwa vyama vyao, ndio waliitafsiri wao na wapambe wao kuwa vyama vyao ni imara.

Kama kweli kuongea kwa kujinyeyekeza kwa ccm kunavipa nafasi vyama vya siasa, basi vyama vinavyojipendekeza kwa ccm kama TLP, UDP, NCCR, CUF nk vingekuwa na nafasi huko kwa wananchi. Mtu mjinga ya kama ww ndio anaweza kuamini ccm hii ni imara. Chama imara hakishindi uchaguzi kwa kutumia udhaifu wa katiba na shuruti, nakushauri urudi shule ukajifunze uimara wa chama ni nini.
Reaction ya Watanzania baada ya uchaguzi ilitosha tu kukujuza kuwa CCM ni chama cha namna gani. Watanzania hawakuwa na si wajinga kama unavyoamini wewe.

Ndo maana haya maneno ya kuibiwa kura, sijui katiba mbovu, mara sijui tuma.....yatabaki kuwa yenu hapa jf. Mwananchi wa pale Mziha anaihitaji umeme, akiupata kupitia CCM si mpaka nirudi shule kujifunza uimara wa CCM.
Mkulima wa pale NgareNairobi Sanya Juu akiiona ile lami inayokwenda kuiunganisha Siha na Longido.....Siha na Hai.....anaiona CCM,so hapo hata kama nchi ingekuwa haina katiba kwake sawa tu.

Mtu wa pale Moshi mjini akiiangalia hospitali ya Mawenzi pale mambo yanavyopamba moto hatajuwa kuwa upinzani uliibiwa kura.....anajuwa CCM ipo kazini. So siku mkiitambua CCM kama chama kikubwa,na wananchi watawaheshimu kama wapinzani wa CCM.
 
Wasi wasi unakuja kwa vile tayari kuna watu walishaanza kutest mitambo, kuanzia bungeni mpaka kwa wasataafu wenye kuheshimika katika hii Nchi, mashaka zaidi yanakuja kwamba hakuna kiongozi yoyote wa CCM ambaye ameshawahi kukemea hili kwa KUMAANISHA, narudia kwa KUMAANISHA ukiacha Mzee Mkapa ambaye hatunaye kwa sasa.

Hilo ni moja, lingine linalonitia shaka ni nani atajaribu kuinua mdomo kusema, kuandika au hata kuonyesha dalili ya kupingana na hilo suala siku litakapoamuliwa, angali vyombo vya habari vilivyojikunyata, hakuna atakayepinga ikitokea siku imeamuliwa hivyo.

Dr. Bashiru amekuwa sehemu kubwa ya ushindi haramu na wa kishindo kwa CCM 2020, pengine akawa tena sehemu ya mageuzi ya Katiba yetu kufanikisha kile wengi wanachokihofia.
Niseme tu kwamba Mh. Rais amekuwa msema kweli na mpenzi wa Mungu wakati wote, hope hili linalosemwa hatalikubali hata alazimishwe vipi.
Ni hayo tu.
Maneno ya paragraph ya mwisho kabla ya ni hayo tu, ni rushwa - unajaribu kumpa rushwa Mh. Rais!
Pia unashangaa nani ataweza kuinua mdomo kusema! Je! Si mnaye mtetezi wenu Amsterdam?
 
Kuna clip ipo humu mitandaoni ikimuonyesha Bashiru akiapa kuwa hatukubali akipewa nafasi nyingine zaidi ya huo ukatibu mkuu. Kama Magufuli hana nia kujiongezea muda, ni kwanini amchague mtu aliyekiri mbele yake, na hadharani kuwa hayuko tayari kupatiwa nafasi nyingine tena?
Hukuelewa kauli hiyo! Alimaanisha, baada ya kuwa katibu mkuu, hata taka uteuzi mwingine wa kuongezewa hapo (kwa kingereza - concurrently). Ukikumbuka, baada ya hapo watu wengi walinyang'anywa vyeo vingine wakabaki na kimoja!
 
Sasa kwa nini watu wauhusishe uteuzi wa Bashiru na uongezwaji wa mihula?
Ni wapuuzi tu ndiyo wanaozusha. Mwenyewe ukimuona JPM amechoka na angependa 2025 ifike kesho akabidhi kijiti ila michadema, mungu anaiona
 
Kuna clip ipo humu mitandaoni ikimuonyesha Bashiru akiapa kuwa hatukubali akipewa nafasi nyingine zaidi ya huo ukatibu mkuu. Kama Magufuli hana nia kujiongezea muda, ni kwanini amchague mtu aliyekiri mbele yake, na hadharani kuwa hayuko tayari kupatiwa nafasi nyingine tena?
Kapewa nafasi ile ile ya ukatibu...
 
Term limits zimeanza wakati wa Alhaji Ali Hassan Mwinyi.

Kwa kumbukumbu zangu hata Mzee Mwinyi alikuwa anabembelezwa aendelee kukaa madarakani.

Wakati wa Mkapa sikusikia sana hii habari ya kumbembeleza aongeze muda.

Labda ni kwasababu Salmin Amour alijaribu kule Znz lakini akakataliwa na chama chake.

Awamu ya JK nayo kulikuwa na wana-CCM waliomtaka aongeze kukaa madarakani lakini hakufanya hivyo.

Kishawishi cha kuongeza muda ni suala ambalo watangulizi wa Magufuli walikipitia lakini walikishinda.

Katika awamu hii mahali pa kuwa makini napo ni BUNGENI. Je, bunge hili la CCM watupu halitabadili katiba?

Baada ya hapo itabidi tumuangalie Magufuli, lakini hatuwezi kujua nini atafanya kwasababu uchaguzi mwingine ni 2025.

Mwisho, miaka yote kumekuwa na kambi mbili; inayotaka Rais aongeze muda, na inayopinga muda wa Urais usiongezwe.
 
Back
Top Bottom