GE2025 Bashiru: Samia alikutana na majaribu mengi alisimama kidete

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,039
Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ali amemtaja Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kama kiongozi mwenye ubunifu, uchapakazi na umahiri katika mipango ya kuwatumikia Watanzania.

Dkt. Bashiru amebainisha hayo leo Jumanne Oktoba 28, 2025 kwenye Viwanja vya CCM Kirumba Jijini Mwanza wakati wa ufungaji wa kampeni za Dkt. Samia katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, akitolea mfano namna ambavyo aliagiza fedha za mapambano ya Ugonjwa wa Uviko-19 zielekezwe kwenye kuboresha huduma za afya, maji, elimu na miundombinu mbalimbali kote nchini.

Soma pia: Dkt: Bashiru: CCM ndio chama pekee chenye nguvu ya kupambana na Rushwa

"Huyu ndiye kiongozi ambaye tulipokuwa bungeni alileta mpango wa serikali wa namna ya kutumia pesa za mkopo kwaajili ya kukabiliana na madhara ya kiuchumi na kijamii yaliyotokana na ugonjwa wa Corona. Ule mpango ulivyokuja bungeni si tu kuwa ulikuwa wa maana lakini hakuna Mbunge ambaye hawezi kuthibitisha kuwa mpango ule wa matumizi ya fedha ulitokana na ubunifu wake wa Kiuongozi." Amekaririwa akisema Dkt. Bashiru.

Bashiru amesema kutokana na maamuzi yake, Tanzania imejijengea heshima ya kuweza kujitawala kwa kuweka vipaumbele vya nchi licha ya kukopa ama kusaidiwa, akimtaja kama Kiongozi anayeweka vipaumbele vyake katika mahitaji halisi ya Watanzania na Tanzania kwa ujumla.

"Sifa nyingine Dkt. Samia ni mstahilimivu na mtulivu sana. Uchaguzi wa mwaka huu na kampeni zake ulikuwa ni uchaguzi kwenye kampeni kujadili masuala na sio watu, hivi ni viwango vya aina yake katika historia ya uchaguzi wa nchi yetu na hata pale ambapo alitukanwa yeye binafsi na familia yake na Chama chake na serikali anayoiongoza alisimama na kuwasihi na kuwaasa Watanzania akasema msichokozeke." Amekaririwa akisema Dkt. Bashiru Ali.
 
Hivi former mwenyekiti kawatapeli mboga mboga mbona hadi dk za jioni kauchuna gu
 
Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ali amemtaja Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kama kiongozi mwenye ubunifu, uchapakazi na umahiri katika mipango ya kuwatumikia Watanzania.

Dkt. Bashiru amebainisha hayo leo Jumanne Oktoba 28, 2025 kwenye Viwanja vya CCM Kirumba Jijini Mwanza wakati wa ufungaji wa kampeni za Dkt. Samia katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, akitolea mfano namna ambavyo aliagiza fedha za mapambano ya Ugonjwa wa Uviko-19 zielekezwe kwenye kuboresha huduma za afya, maji, elimu na miundombinu mbalimbali kote nchini.

Soma pia: Dkt: Bashiru: CCM ndio chama pekee chenye nguvu ya kupambana na Rushwa

View attachment 3495218

"Huyu ndiye kiongozi ambaye tulipokuwa bungeni alileta mpango wa serikali wa namna ya kutumia pesa za mkopo kwaajili ya kukabiliana na madhara ya kiuchumi na kijamii yaliyotokana na ugonjwa wa Corona. Ule mpango ulivyokuja bungeni si tu kuwa ulikuwa wa maana lakini hakuna Mbunge ambaye hawezi kuthibitisha kuwa mpango ule wa matumizi ya fedha ulitokana na ubunifu wake wa Kiuongozi." Amekaririwa akisema Dkt. Bashiru.

Bashiru amesema kutokana na maamuzi yake, Tanzania imejijengea heshima ya kuweza kujitawala kwa kuweka vipaumbele vya nchi licha ya kukopa ama kusaidiwa, akimtaja kama Kiongozi anayeweka vipaumbele vyake katika mahitaji halisi ya Watanzania na Tanzania kwa ujumla.

"Sifa nyingine Dkt. Samia ni mstahilimivu na mtulivu sana. Uchaguzi wa mwaka huu na kampeni zake ulikuwa ni uchaguzi kwenye kampeni kujadili masuala na sio watu, hivi ni viwango vya aina yake katika historia ya uchaguzi wa nchi yetu na hata pale ambapo alitukanwa yeye binafsi na familia yake na Chama chake na serikali anayoiongoza alisimama na kuwasihi na kuwaasa Watanzania akasema msichokozeke." Amekaririwa akisema Dkt. Bashiru Ali.

Naona Bashiru kakataa kabisa kurudi kule JALALANI..............!!
 
Back
Top Bottom