2025 na mbeleni

2025 na mbeleni

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
97,930
Reaction score
141,891
Sijaelewa ni kwanini kuna watu wanauhusisha uteuzi wa Dkt. Bashiru kuwa katibu mkuu kiongozi na Rais Magufuli kuongeza muda kuiongoza Tanzania kwa zaidi ya mihula miwili.

Dkt. Bashiru amewahi kunukuliwa akisema kuwa anapendelea iwe hivyo? Yaani Rais Magufuli aongezewe muda wa kutawala?

Au ni kiwewe tu cha wasiompenda Magufuli? Maana kiwewe huwa kinavuruga akili ya mtu.

Kiwewe kinaweza kumfanya mtu aione 1 ni 3 na 3 ni 2!

Kiwewe kinaweza kumfanya mtu alione giza ni mwanga na mwanga ni giza, salamu ni tusi na tusi ni salamu.

Halafu ni kama vile kuna watu wanaombea Magufuli kweli aongezewe au aongeze muda ili wapate sababu za kumsema na kujipatia vijipointi vya kisiasa.

Na asipojiongezea, watu hao watakuwa disappointed sana maana atakuwa ‘kawaangusha’.

Mimi bado naamini endapo ataendelea kuwa mzima, basi ataongoza kwa idadi ya mihula inayoruhusiwa na katiba tuliyonayo sasa.

Otherwise, uhusiano wa Dkt. Bashiru kuwa katibu mkuu kiongozi na uongezwaji wa muda Rais Magufuli kuendelea kuwa Rais ni nini?
 
Je, kuna kiongozi yoyote au Mtanzania mwenzetu ambaye ameshawahi kutamka kwamba, kama inawezekana Magufuli aongozewe muda?
 
Kauli ya Bashiru Ali kuwa watashinda uchaguzi kwa kutumia Dola na hata wengine(wapinzani ) wakishika dola wataitumia kubaki madarakani kwa nguvu

Ni aibu na ajabu kauli hii kutolewa na kiongozi mkuu wa chama akidhihirisha kuinajisi demokrasia hadharani na matokeo yake tulipata uchafuzi wa mitaa na uchafuzi mkuu (sio uchaguzi).

Bashiru wa katiba mpya si huyu wa sasa ni walakini kuwaamini watu wa jinsi hii kamwe! Maslahi mbele !

Alisema hawatotumia wasanii wa bongofleva kwenye kampeni badala yake watatumia waimbaji wa nyimbo za asili matokeo yake ilikua kinyume.

Mwisho ni kusema hatohitaji teuzi zaidi nyingine ukatibu mkuu kwake ndio cheo kikubwa ila kashindwa kuyaishi maneno yake

Je, utamuaminije mtu wa hivi?
 
Sasa kwa nini watu wauhusishe uteuzi wa Bashiru na uongezwaji wa mihula?
Mzee waacheni tu mtateseka bure kujibizana nao. Rejea mwaka 2015.....ilifikia hatua akisa Sugu walimuita Kikwete kuwa ni Nkurunzinza wa Tanzania...kila siku walikuwa na press za kuitaka tume ya Taifa ya Uchaguzi itangaze tarehe ya uchaguzi.

Rejea baadhi ya Wabunge wa upinzani kudai Kikwete amesema hakuna uchaguzi....yaani hawa ni wale ambao wao wapo kufuatana na upepo au uelekeo wa jua.
 
Wasi wasi unakuja kwa vile tayari kuna watu walishaanza kutest mitambo, kuanzia bungeni mpaka kwa wasataafu wenye kuheshimika katika hii Nchi, mashaka zaidi yanakuja kwamba hakuna kiongozi yoyote wa CCM ambaye ameshawahi kukemea hili kwa KUMAANISHA, narudia kwa KUMAANISHA ukiacha Mzee Mkapa ambaye hatunaye kwa sasa.

Hilo ni moja, lingine linalonitia shaka ni nani atajaribu kuinua mdomo kusema, kuandika au hata kuonyesha dalili ya kupingana na hilo suala siku litakapoamuliwa, angali vyombo vya habari vilivyojikunyata, hakuna atakayepinga ikitokea siku imeamuliwa hivyo.

Dr. Bashiru amekuwa sehemu kubwa ya ushindi haramu na wa kishindo kwa CCM 2020, pengine akawa tena sehemu ya mageuzi ya Katiba yetu kufanikisha kile wengi wanachokihofia.

Niseme tu kwamba Mh. Rais amekuwa msema kweli na mpenzi wa Mungu wakati wote, hope hili linalosemwa hatalikubali hata alazimishwe vipi.

Ni hayo tu.
 
Mkuu usiwe mchoyo wa ukweli kufanya siasa za upinzani nchini ni vigumu mno na ilikuwa rahisi kwa ANC kufanya siasa ndani ya SA kipindi cha utawala wa kibaguzi wa makaburu kuliko kwa CUF kufanya siasa ndani ya Tanzania ya President Magufuri.
Na siyo CUF tu....hata CHADEMA.

Miaka ya 2010 mwishoni hadi na 14....hakuna mwana CCM alikuwa anathubutu kuvaa sare ya chama mtaani.....yaani tulikuwa tunazomewa kila kona.

Mambo yamebadilika CCM sasa tunatamba. Na itaendelea kuwa ngumu kufanya siasa mpaka pale wapinzani watakapotambua kuwa CCM ndicho chama tawala Tanzani....ili wakati watakapokuwa wanakosoa wakosoe wakijuwa wanaongea na chama kikubwa na wawe na adabu.
 
Sasa kwa nini watu wauhusishe uteuzi wa Bashiru na uongezwaji wa mihula?

Kuna clip ipo humu mitandaoni ikimuonyesha Bashiru akiapa kuwa hatukubali akipewa nafasi nyingine zaidi ya huo ukatibu mkuu. Kama Magufuli hana nia kujiongezea muda, ni kwanini amchague mtu aliyekiri mbele yake, na hadharani kuwa hayuko tayari kupatiwa nafasi nyingine tena?
 
Wasi wasi unakuja kwa vile tayari kuna watu walishaanza kutest mitambo, kuanzia bungeni mpaka kwa wasataafu wenye kuheshimika katika hii Nchi, mashaka zaidi yanakuja kwamba hakuna kiongozi yoyote wa CCM ambaye ameshawahi kukemea hili kwa KUMAANISHA, narudia kwa KUMAANISHA ukiacha Mzee Mkapa ambaye hatunaye kwa sasa.

Hilo ni moja, lingine linalonitia shaka ni nani atajaribu kuinua mdomo kusema, kuandika au hata kuonyesha dalili ya kupingana na hilo suala siku litakapoamuliwa, angali vyombo vya habari vilivyojikunyata, hakuna atakayepinga ikitokea siku imeamuliwa hivyo.

Dr. Bashiru amekuwa sehemu kubwa ya ushindi haramu na wa kishindo kwa CCM 2020, pengine akawa tena sehemu ya mageuzi ya Katiba yetu kufanikisha kile wengi wanachokihofia.
Niseme tu kwamba Mh. Rais amekuwa msema kweli na mpenzi wa Mungu wakati wote, hope hili linalosemwa hatalikubali hata alazimishwe vipi.
Ni hayo tu.
Usiwe na hofu....CCM inawatu wazuri sana wakukemea jambo kama hilo. Na tunavija ambao wanauwezo mkubwa sana wa kukemea hata wazee pale watakapopotoka.

Ni suala la muda.....na nakuhakikishia,Magufuli ataondoka kama wastaafu wengine walivyoondoka.
 
Kuna clip ipo humu mitandaoni ikimuonyesha Bashiru akiapa kuwa hatukubali akipewa nafasi nyingine zaidi ya huo ukatibu mkuu. Kama Magufuli hana nia kujiongezea muda, ni kwanini amchague mtu aliyekiri mbele yake, na hadharani kuwa hayuko tayari kupatiwa nafasi nyingine tena?
Kwani mtu hawezi kubadili mawazo?
 
Ile ilikuwa na kauli ya ndani ya chama......ameteuliwa kuingia serikalini.
Na pia hata kwa ustaarabu tu wa kawaida.....asingeweza kumkatalia Rais wa nchi na kwa nafasi nyeti kama ile.

Kingine,mwanasiasa akisema kitu,angalia nyakati na mazingira.
Mwaka 2010 Kiwete alibana na Slaa akajikuta anaahidi kila kitu. Yaani hata angekuta dimbwi mahali angeweza kuahidi meli. Zilikuwa nyakati ngumu na mazingira magumu ya siasa za wakati huo.

Kwa wakati Bashiru anatoa kauli ile....tulikuwa tunaelekea uchaguzi mkuu.....analikuwa anasisitiza jambo.
 
Na siyo CUF tu....hata CHADEMA.....
Miaka ya 2010 mwishoni hadi na 14....hakuna mwana CCM alikuwa anathubutu kuvaa sare ya chama mtaani.....yaani tulikuwa tunazomewa kila kona.

Mambo yamebadilika.......CCM sasa tunatamba. Na itaendelea kuwa ngumu kufanya siasa mpaka pale wapinzani watakapotambua kuwa CCM ndicho chama tawala Tanzani....ili wakati watakapokuwa wanakosoa wakosoe wakijuwa wanaongea na chama kikubwa na wawe na adabu.

CCM haitambi, bali madaraka ya Urais yanayotumika vibaya kuteka watu, kuua wapinzani, kunajisi uchaguzi na uhayawani mwingine kama huo ndio yanayotamba. Kinachofanyika katika kuibeba CCM na kuifanya ionekane imara ni kiburi cha madaraka ya Urais ya mwenyekiti wake.

Kuna wakati Iddi Amin, Moi, Mugabe nk waliamini vyama vyao ni imara, sio kwakuwa kweli vilikuwa imara, bali yalikuwa ni madaraka ya viongozi hao kutumia vyombo vya dola kutoa upendeleo kwa vyama vyao, ndio waliitafsiri wao na wapambe wao kuwa vyama vyao ni imara.

Kama kweli kuongea kwa kujinyeyekeza kwa CCM kunavipa nafasi vyama vya siasa, basi vyama vinavyojipendekeza kwa CCM kama TLP, UDP, NCCR, CUF nk vingekuwa na nafasi huko kwa wananchi. Mtu kama wewe ndio anaweza kuamini CCM hii ni imara. Chama imara hakishindi uchaguzi kwa kutumia udhaifu wa katiba na shuruti, nakushauri urudi shule ukajifunze uimara wa chama ni nini.
 
Kwani mtu hawezi kubadili mawazo?

Sasa unakataa nini, kwani huyo Magufuli hawezi kusema amebadili mawazo? Mtu mwenye nia ovu huwa anaacha viashiria, na watu kusema kuwa Magufuli atajiongezea muda wa kukaa madarakani, ni kwakuwa kuna viashiria vya zaidi ya 80%.
 
Ile ilikuwa na kauli ya ndani ya chama......ameteuliwa kuingia serikalini.
Na pia hata kwa ustaarabu tu wa kawaida.....asingeweza kumkatalia Rais wa nchi na kwa nafasi nyeti kama ile.

Kingine,mwanasiasa akisema kitu,angalia nyakati na mazingira.
Mwaka 2010 Kiwete alibana na Slaa akajikuta anaahidi kila kitu. Yaani hata angekuta dimbwi mahali angeweza kuahidi meli. Zilikuwa nyakati ngumu na mazingira magumu ya siasa za wakati huo.

Kwa wakati Bashiru anatoa kauli ile....tulikuwa tunaelekea uchaguzi mkuu.....analikuwa anasisitiza jambo.

Nilitegemea utoe utetezi huu dhaifu. Mambo mengine ni aibu, ni bora ukae tu kimya.
 
Back
Top Bottom