2022: Naliona Jeshi la Polisi Tanzania likifanyiwa marekebisho makubwa

Mtemi mpambalioto

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
3,263
7,400
Jeshi hili lipo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani na Usalama wa Raia

neno usalama wa Raia ndipo chimbuko la mabadiliko ninayoyaona mbeleni mwakahuu. Jeshi hili halijawahi kuwa karibu na Raia hata kidogo!

jamii ambayo inaweza kukimbilia polisi ni wezi wanapokuwa wamebananishwa kipigo kikaanza wakatokea polisi inakuwa kwao ni salama!

Raia ambaye anakuwa kaonewa huwa anawaza mara mbili mbili kwenda Polisi kwa hofu ya kugeuziwa kibao:

1. RUSHWA: Polisi wanapenda rushwa, si ajabu mtuhumiwa akapewa haki kulliko mlalamikaji.

2. HAWANA HOFU: Polisi hawana hofu ya Mungu na watawala: wao wanaweza kukuua kwa kipigo au kwa kutaman mali uliyokamatwa nayo ili mradi wanafaidika:

3. WASIOJULIKANA: Matukio mabaya kabisa ambayo watawala hawaoni ni mabaya ni yale ya mtu kuchukuliwa kimya kimya au kupekuliwa kimya kimya! hivi ni mojawapo ya vitendo vya kinyama kabisa ambavyo polisi hufanya na hakuna wa kuwahoji.

4. KUTUMIKA: kutumika na watawala au wafanyabiashara wenye nguvu kumewasababisha wakawa wanaona wanaeza fanya lolote na wasiwajibishwe!

5. BIASHARA: Polisi kugeuza raia mtaji wa kibiashara! unakuta polisi wanalazimisha mfano makosa ta barabarani kuwa lazima wapate mapato na bila aibu huwa wanatangaza wamepata kiasi fulani kwa mbwembwe: maana yake wanafurahia makosa kuwa mengi ili wapate hela badala ya kupambana na kutoa elimu

6. WAKUU WA POLISI WASIO NA WELEDI: Viongozi wa Polisi wengi wao wana uwezo mdogi sana wa kuelewa majukumu yao! wengi wamepitia njia panya kupata vyeo hivyo wanafanya kazi kimazoea! wengi elimu zao za kuunga unga ambazo imekuwa shida

7. ELIMU YA SAIKOLOJIA: matukio mengi tunayobahatika kuyaona yakirekodiwa yanaonyesha polisi wanatumia nguvu kubwa kupambana na watu wasio na nguvu na wasio na elimu ya kipolisi. mwisho wa siku wakiharibu wanakuunganishia tukio lolote baya ili uonekane ulikosea wewe.

8. WIZI na UJAMBAZI: Baadhi ya polisi wanahusika na wizi na ujambazi mkubwa maana machaka haya ya ujambazi wanayafahamu kiundani ila kwa kuwa wanafaidika na migao inakuwa kwao ni faida. wakati wa mkono wa chuma mambo yalitulia kwa kuwa hata polisi waliguswa na kukomeshwa kisawasawa

NINI KIFANYIKE?
1. Mkuu wa nchi abadilishe kabisa viongozi wa ngazi za juu! abdilishe wahumi wote awaweke pembeni na wawe monitored atakayeleta mambo ya ajabu ni kupiga chini mazima

2. Mkuu wa nchi asiwaonee aibu polisi wanapofanya matukio ya ajabu kama lile la mtwara kuia raia kupora fedha zake

3. Kuwe na tovuti au mawasiliano maalum ya kuwaripoti polisi ambao wanafanya matukio mabaya kwa raia! hili litafanya wananchi wawe na imani na serikali yao!

4. Rais aboreshe jeshi la polisi, walipe vizuri, wape vitendea kazi na makazi bora ili atakayeharibu kazi akitolewa aone uchungu wa kukosa kazi.
 
Bila shaka utakuwa Mpiga Lamli mzuri sana hongera ,lakini kumbuka hili Jeshi ndio lile linalo tumika kipindi Cha Chaguzi hivyo lazima litengenezwe ki ukijani
 
Bila shaka utakuwa Mpiga Lamli mzuri sana hongera ,lakini kumbuka hili Jeshi ndio lile linalo tumika kipindi Cha Chaguzi hivyo lazima litengenezwe ki ukijani
wapinzani ni jicho la serikal na chama tawala katika kurekebisha makosa kiutendaji,! bahat mbaya hili ni tatizo kwa africa
 
Nimesoma uzi huu nikamkumbuka HAMZA na kumshukuru Mungu kwa ajili yake.
 
Natamani tuwe na jeshi la polisi kama la Uk, Marekani na kwingineko. Mbona wao wanaweza sisi tunashindwa njni??
 
Back
Top Bottom