2021 - Oktoba 2025: Muda mwafaka wa wapinzani nchini Tanzania kujijenga ili kufanya mageuzi ya kisiasa

MR BINGO

JF-Expert Member
Feb 12, 2016
1,092
2,270
Salaam wana jamvi,

Twende kwenye mada tajwa moja kwa moja.

Tukianza na utawala wa awamu ya tano wa John pombe magufuli ambako tulishuhudia mtikisiko mkubwa wa upinzani nchini Tanzania ambao uliosukumwa na matumizi mabaya ya demokrasia hayo yalithibitishwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Pamoja na kwamba Magufuli alifanya baadhi ya mambo mazuri ambayo hatuwezi kujifanya vipofu na hatuyaoni lakini moja ya makosa makubwa aliyoyafanya ni udidimizaji wa demokrasia uliofanyika mwaka 2020 ambao tunaweza kuuita "ubakaji wa demokrasia". Pengine unaweza kumwelewa Magufuli kwa kusema kuwa alikuwa akikitetea chama chake lakini ukiangalia kwa jicho la tatu utaona ya kuwa alikuwa anakwenda kukibomoa chama chake katika uchaguzi unaofuata ambao ni wa 2025.

Uchaguzi wa mwaka 2025 unaweza kuwa uchaguzi mbaya zaidi kwa chama cha CCM kutokana na sababu ya kwanza niliyooitoa hapo juu na sababu ya pili ni kuwa Magufuli mwenyewe hayupo na hakutengeneza mfumo bora wa uongozi bali alitengeneza serikali inayomtegemea yeye kwa hiyo tunaweza kusema baada ya Magufuli kuondoka kila alichokitengeneza kimevurugika/kitavurugika (kwa hili nadhani tunashuhudia wenyewe).

Tuangalie basi sababu zipi zinawapa upinzani nchini Tanzania fursa ya kujirudi na kujijenga tena kwa wananchi katika mwaka 2025.
  1. kukosa uzoefu wa kisiasa kwa wabunge wengi wa bunge la 21 (bunge la Ndugai): wabunge wengi waliopo katika bunge hili la 21 hawana uzoefu wowote wa kisiasa maana wengi walipitia mgongo wa Magufuli ili kupata madaraka hayo ya ubunge swala ambalo litawafanya kupata wakati mgumu sana kwenye uchaguzi wa mwaka 2025 kwani watakutana na upinzani mkubwa kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wa zamani wa upinzani ambapo hoja kubwa itakayowatoa ni kuhoji mambo yaliyotekelezwa na wabunge hawa waliopo bungeni kwa kipindi hiki cha miaka mitano. hivyo tunaona kabisa kushinda chaguzi hizi za ubunge kwa wapinzani itakuwa kama kumsukuma mlevikwa maeneo mengi ya nchi.
  2. Mpasuko ulioko ndani ya CCM : sababu nyingine itakayowaumiza CCM katika uchaguzi wa 2025 ni mpasuko uliojitokeza ndani ya chama ambapo tunashuhudia kuwa kuna makundi kama matatu yenye interest tofauti yaliyojitokeza baada ya kifo cha Magufuli. makundi haya yaliyopo ndani ya chama tawala kila kundi linapinga juhudi za kundi jingine hivyo kuna upinzani ndani ya CCM wenyewe. jambo hili linachagizwa pia na mrithi wa Magufuli ambaye haonekani akitumia nguvu kubwa kukiunganisha chama na kukifanya kuwa kitu kimoja hivyo hili tunaweza kulitafsiri kama udhaifu kwani na yeye naye amejiweka kwenye mojawapo ya makundi hayo yaliyopo CCM. Hii inatoa fursa kwa wapinzani kuwa na nafasi kubwa ya kushinda endapo watajijenga vizuri kwani wanaenda kushindana na chama ambacho kina mgawanyiko.
  3. Mrithi wa J.P.M : Mama Samia Suluhu ambaye ni mrithi wa J.P.M naye atakuwa chagizo kubwa kwa wapinzani kufanya vyema katika uchaguzi ujao kwani amejipambanua kuwa tofauti na mtangulizi wake katika nyanja mbalimbali jambo ambalo linatupa picha kuwa uchaguzi wa mwaka 2025 hautakuwa na mgandamizo wa kidemokrasia kama uliojitokeza mwaka 2020. Japo hatuwezi kujihakikishia kuwa uchaguzi utakuwa wa huru na haki kwa asilimia 100 lakini pia hatutarajii ukandamizaji uliojitokeza kwenye uchaguzi uliopita kujitokeza tena na hivyo upinzani wanapata nafasi ya kushindana katika "fair environmet" na hivyo kuongeza nafasi yao ya kufanya vizuri.
  4. serikali iliyoundwa na CCM watupu: serikali iliyopo madarakani katika kipindi hiki cha mwaka 2020 mpaka 2025 kwa asilimia zaidi ya 90 imeundwa na CCM jambo hili litawawia vigumu kuwashawishi wananchi mwaka 2025 endapo ahadi walizoahidi mwaka 2020 hazitatekelezeka kwani kisingizio cha "wapinzani walituchelewesha" hakitakuwepo tena, hapo wapinzani watapata nafasi kubwa ya kushinda mioyo ya wananchi.
Baada ya kuona sababu hizo nadhani upinzani wanatakiwa kufanya yafuatayo ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kushinda
  • wahakikishe wanajiimarisha katika mikoa na wilaya ili kuwa na wagombea wenye ushawishi huo mwaka 2025
  • waepuke malumbano yasiyo na faida ambayo yatapelekea migawanyiko katika vyama vyao
  • kutengeneza sera nzuri ambazo zitatumika katika uchaguzi huo wa mwaka 2025 kwani wakati ndo huu wasisubirie mpaka mwaka 2025 ufike
  • wautumie mpasuko ulioko CCM vizuri kujipatia watu watakaowasaidia katika uchaguzi huo wa 2025 lakini pia wawe makini kupokea mamluki
  • wawainue vijana wapya wenye ari ya kuipigania nchi kutoka vyuo na sekta mbalimbali
Pamoja na hayo yote bado itakuwa ngumu kwa upinzani kuchukua uraisi ila kwa nafasi za ubunge kushuka chini kuna nafasi kubwa ya upinzani kufanya vizuri katika uchaguzi unaokuja wa 2025 endapo wataitumia fursa hii vizuri

ADIOS AMIGOS
 
WAPINZANI HAWANA SERA KAMA NI HIZI SERA ZA MBOWE HAKUNA KITU
Endapo watakuwa serious na kutengeneza sera na kuacha utani wanaofanya wa kukaa Twitter na kugombania BET nahic watafanya vizuri tu mkuu

Na muda ndo huu
 
Chama gani cha kuiondoa CCM!?.. Wapinzani gani wa kumuondoa mama Samia 2025!?.. Hawahawa waliogeuka na kumshangilia na kumsifu mama Samia kwenye kila kitu kisa chuki na hayati JPM!?....
Labda unachhongea ni kweli ila kushindwa kwa upinzani mwaka 2025 kwenye ngazi za ubunge kushuka chini kuko mikononi mwao wenyewe
 
Labda unachhongea ni kweli ila kushindwa kwa upinzani mwaka 2025 kwenye ngazi za ubunge kushuka chini kuko mikononi mwao wenyewe
Mkuu watu ambao mpaka dakika hii wameshupalia ishu Kama Diamond na BET wanasahau hata kukomalia tume huru ya uchaguzi ndo waje kushinda uchaguzi!?..

hata kwenye ngazi za ubunge wanahitaji sera za pamoja Kama chama. Hii kutojua wanachopigania ili kuwaaminisha/kuwaelewesha wananchi udhaifu wa CCM kutawafelisha vibaya sana hata 2025.
 
Hakuna kitu hapo! Mshindi wa uchaguzi huwa anatangazwa na Tume ya Uchaguzi na Returning Officers ambao ni Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na za Miji.
 
Hakuna kitu hapo! Mshindi wa uchaguzi huwa anatangazwa na Tume ya Uchaguzi na Returning Officers ambao ni Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na za Miji.
2020 na 2015 washindi wa uchaguzi walitangazwa na tume ya uchaguzi ya CCM lakini kuna utofauti mkubwa kati ya matokeo ya 2020 na 2015

Tume huru ya uchaguzi haiwez kuwa huru kwa 100% lakini hatutarajii ubakaji wa demikrasia uliofanyika 2020 kutokea 2025 Kwa kiwango kilekile
 
2020 na 2015 washindi wa uchaguzi walitangazwa na tume ya uchaguzi ya CCM lakini kuna utofauti mkubwa kati ya matokeo ya 2020 na 2015

Tume huru ya uchaguzi haiwez kuwa huru kwa 100% lakini hatutarajii ubakaji wa demikrasia uliofanyika 2020 kutokea 2025 Kwa kiwango kilekile
Kama hiki ndicho wanachodanganyana huko kwenye upinzani basi wana safari mrefu sana ya kuwa washindani wa kweli kwenye siasa zetu za Tanzania.
 
Hawa hawa waliogeuka na kuanza kupambana na Mondi huku wakiimba mi 10 tena kwa mama ili kumkomoa marehemu?
 
Back
Top Bottom