Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,003
Wakati taifa bado linafuatilia habari za mgodi wa Barrick huko Tarime, habari nyingine ambazo zimepatikana zinadai kuwa viongozi 2 (mwenyekiti na Katibu) wa wafanyakazi kwenye mgodi wa Geita Gold huko Mkoani Geita wamefukuzwa kazi hapo jana huku wakipewa siku tatu kukata rufaa baadaya kuongoza maandamano ya kudai chama chao cha Wafanyakazi Migoni kisajiliwe kitu ambacho kinadaiwa kupingwa na menejjimenti kwa madai kuwa "idadi" ya wanachama haijatimia licha ya wafanyakazi hao kudai kuwa idadi imeshatimia ya kuweza kuundwa kwa chama cha kudai haki na maslahi ya wafanyakazi.
Upande wa menejimenti unadai kuwa wafanyakazi hao wamefukuzwa baadaya "kuwatukana" uongozi kwenye mabango yao ambayo yalitumika kudai chama chao cha wafanyakazi. Hadi hivi sasa imekuwa ngumu kwenye baadhi ya migodi kuunda vyama vya wafanyakazi wakati kwenye baadhi yao vyama hivyo vipo. Mgodi wa Kahama Mining unao chama cha wafanyakazi migodini (TAMICO).
Kuna mambo mengine ambayo yamo mikononi mwa vi-nzi na yataweletwa ili kuonesha harakati ambazo zinafanya kuzuia wafanyakazi kujiunga pamoja kupigania na kudai haki zao hasa huko migodini.
Fikra Pevu

Mh. Regia Mtema- Waziri kivuli wa Ajira na kazi.... hii yako komaa nayo mpaka kieleweke.
Ninaamini kama watanzania hawawezi kukemea tabia hizi basi CHADEMA as chama cha wakombozi kichukuwe jukumu la kuweka wakili wa kujitolea ili watu hawa wapate haki zao. Nchi haiwezi kuendeshwa kiholela halafu wananchi tunyamaze kimya. Wakati wa kunyamaza kimya umeshapita. Tundu Lissu, wewe ni mbunge ambaye unafahamu zaidi matatizo yanayowakabili watanzania wenzetu huko migodini. Huu ni wakati muafaka kulishughulikia tatizo hilo. Kumbuka: Wabunge wa CHADEMA ni wabunge wa Taifa zima (hiyo ni kwa mujibu wa CHADEMA yenyewe).
Twende kazini huko migodini na sehemu zingine.