2 Wafukuzwa kazi kwa Kudai Kuundwa chama cha Wafanyakazi Geita Gold | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

2 Wafukuzwa kazi kwa Kudai Kuundwa chama cha Wafanyakazi Geita Gold

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 19, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wakati taifa bado linafuatilia habari za mgodi wa Barrick huko Tarime, habari nyingine ambazo zimepatikana zinadai kuwa viongozi 2 (mwenyekiti na Katibu) wa wafanyakazi kwenye mgodi wa Geita Gold huko Mkoani Geita wamefukuzwa kazi hapo jana huku wakipewa siku tatu kukata rufaa baadaya kuongoza maandamano ya kudai chama chao cha Wafanyakazi Migoni kisajiliwe kitu ambacho kinadaiwa kupingwa na menejjimenti kwa madai kuwa "idadi" ya wanachama haijatimia licha ya wafanyakazi hao kudai kuwa idadi imeshatimia ya kuweza kuundwa kwa chama cha kudai haki na maslahi ya wafanyakazi.  Upande wa menejimenti unadai kuwa wafanyakazi hao wamefukuzwa baadaya "kuwatukana" uongozi kwenye mabango yao ambayo yalitumika kudai chama chao cha wafanyakazi. Hadi hivi sasa imekuwa ngumu kwenye baadhi ya migodi kuunda vyama vya wafanyakazi wakati kwenye baadhi yao vyama hivyo vipo. Mgodi wa Kahama Mining unao chama cha wafanyakazi migodini (TAMICO).


  Kuna mambo mengine ambayo yamo mikononi mwa vi-nzi na yataweletwa ili kuonesha harakati ambazo zinafanya kuzuia wafanyakazi kujiunga pamoja kupigania na kudai haki zao hasa huko migodini.
  Fikra Pevu
   
 2. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Pole sana Shigela..Kaza Buti
   
 3. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Asante sana mkuu kwa taarifa.
  Leo asubuhi nimemsikia Mwenyekiti wa TAMICO taifa akilalamikia suala hilo.

  Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini inaeleza wazi kuwa mfanyakazi hatakiwi kunyanyaswa wal kubaguliwa kwa sababu ya kujiunga na chama cha wafanyakazi kinachotambulika kitaifa.

  Tatizo ninaloliona hapa ni kuwa waajiri wengi, hasa hawa wanaoitwa "wawekezaji" wanafanya hila za makusudi tena wakati mwingine kwa kushirikiana na "wazalendo".
  Serikali iko wapi? kwani hii si case ya kwanza ya wafanyakazi kunyanyaswa.
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  bi Regia mtema upo?
   
 5. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mkkwere na liserikali lake la kishikaji watatumaliza walahi
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mh. Regia Mtema- Waziri kivuli wa Ajira na kazi.... hii yako komaa nayo mpaka kieleweke.
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Ukoloni unarudi taratibu!
  Kama hao jamaa wanajiamini, basi waweke hadharani mambo yote ya kishenzi ya hao waajiri, maana naamini mabango hayakuweza kueleza kila kitu!
  Lakini utakuta baadhi ya oppressermen wa mgodi huo ni weusi wenzetu.
   
 8. c

  chimala Senior Member

  #8
  May 19, 2011
  Joined: Jul 2, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  pole sana Alloyce
   
 9. papason

  papason JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Wana TAMICO wa apo mgodini mpo kweli?
   
 10. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  kazi ipo!!!

  Wawekezaji hao!!!
   
 11. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  UMOJA NI NGUVU..UTENGANO NI UDHAIFU……Wathungu wanawachekechea hapa tuu…….Shigela maskini aliwatafutia mwanga wa dhahabu..utakuta weusi wenzake wamemgeuka na kusema yeye ndo kawashawishi lakini hawakushiriki kwa hiari yao…!! UMASKINI MTUPU TU UNATUDUNDA KA VITENESI…!!
   
 12. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ninaamini kama watanzania hawawezi kukemea tabia hizi basi CHADEMA as chama cha wakombozi kichukuwe jukumu la kuweka wakili wa kujitolea ili watu hawa wapate haki zao. Nchi haiwezi kuendeshwa kiholela halafu wananchi tunyamaze kimya. Wakati wa kunyamaza kimya umeshapita. Tundu Lissu, wewe ni mbunge ambaye unafahamu zaidi matatizo yanayowakabili watanzania wenzetu huko migodini. Huu ni wakati muafaka kulishughulikia tatizo hilo. Kumbuka: Wabunge wa CHADEMA ni wabunge wa Taifa zima (hiyo ni kwa mujibu wa CHADEMA yenyewe).
  Twende kazini huko migodini na sehemu zingine.
   
 13. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #13
  May 19, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  tatizo haya madubwana BARRICK na GEITA yako very musculine in financial terms ndo maana serikali inalegea kama mbuzi vile anamfuata chatu...
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kalumbu twa mashiku ulipo gwa myitu...
   
Loading...