Elungata
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 40,424
- 33,597
juzikati hapa US drone imerusha makombora ya hellfire kwenye mkusanyiko wa harusi huko A.stan na kuua watu karibu 30.Tukio la Marekani linapaswa kulaaniwa na kila mpenda haki na amani. Vinginevyo tukidhani halituhusu eti ni la huko huko Marekani tunajidanganya. Vijana wetu wanajifunza nini hapo? Kwamba unaweza kuvamia mikusanyiko kama viwanja vya michezo, maeneo ya ibada, n.k. na ukauwa watu unavyotaka?
Ni tukio la kulaani kwa nguvu zote hata kama halijatokea kwenye ardhi yetu. Ni wapuuzi wachache watashabikia unyama huu kama wanavyoshabikia mengine kama yale ya kuvamia nyumba za ibada, kushambulia viongozi wa dini, n.k.
Wapi post yako ya kulaani?.
Au unalaani wakiuawa wazungu pekee.