2 Explosions rock Boston Marathon finish line...2 dead, scores injured!

2 Explosions rock Boston Marathon finish line...2 dead, scores injured!

Ni kweli yegomasika kuna watu wana kazi ya kutengeneza uongo uonekane kweli huu ni upuuzi kwasababu watu hapa jf wanasoma na kufuatilia habari, eneo la Watertown Lina wakazi karibu elfu 33, na nyumba za makazi elfu 15, mtu anasema FBI wamepeleka Askari wengi kumkamata mtu 1!
 
Hii saga serious..dunno but nahis kuna more behind the suspects... Vs...fbi..may be kuna more than that..
Maana hii government bana..hmm letw watch
 
He's Muslim terrorist period that doesn't mean all Muslims are terrorist, they're practice what Muhammad taught them kill non believer, slain them and you will be awarded heaven,if you hate American why the hell u going there anyway? Go to Sudan,Pakistan, Somalia, Saudi Arabia, Syria e.t.c. Bunch of losers, suck it up.
Aliyeuwa dazeni za watoto ambao hawana hatia na kujeruhi kule newton siyo gaidi sababu si muislam Lakini waliofanya tendo kama hilo boston ni gaidi sababu ni waislamu kwangu mimi hawa wote ni wauaji bila ya kujali dini hakuna uislamu unaosema ua au lazimisha mtu kuwa muislamu huu upotoshwaji wa kipropaganda ndiyo unaowafanya watu kutoshirikisha ubongo ktk kuelewa kuna baadhi ya binaadamu ni wauaji period!
 
HATIMAYE MTUHUMIWA WA PILI
WA MIRIPUKO YA BOSTON
ATIWA MBARONI


MABOMU1.jpg


Mshukiwa wa mwisho katika utegaji wa mabomu yaliyowauwa watu 3 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 180 katika mbio za Marathon za Boston amekamatwa akiwa ndani ya boti. Polisi imesema kuwa amepelekwa hospitali akiwa mahututi.

Kukamatwa kwa mtu huyo Dzhokhar Tsarnaev, mwenye umri wa miaka 19 kumehitimisha operesheni kubwa ya siku nne, na kumekuja siku moja baada ya shirika la upelelezi la Marekani FBI kuchapisha picha za washukiwa hao.

Mshukiwa mwingine, Tamerlan Tsarnaev mwenye umri wa miaka 26 na ambaye ni kaka wa Dzhokhar, aliuawa jana Ijumaa katika majibizano ya risasi na polisi.

0,,16758762_403,00.jpg


Umati wa watu katika mji wa Boston ulishangilia kwa shangwe baada ya kuibuka kwa ripoti ya kukamatwa kwa mshukiwa huyo. Shughuli zote katika mji huo zilikuwa zimesimamishwa wakati operesheni ya kuwasaka vijana hao ilipokuwa ikiendelea.

Bado yapo maswali yasio na majibu Akizungumza muda mfupi baada ya kukamatwa kwa Dzhokhar Tsarnaev, rais wa Marekani Barack Obama alisema kukamatwa kwa mshukiwa huyo ilikuwa hatua muhimu katika mkasa unaohusu miripuko ya Boston.

Hata hivyo, Obama alisema kuwa bado yanabakia maswali yasio na majibu, ambayo ni pamoja na sababu iliyowafanya vijana hao kufanya mashambulizi, na ikiwa walikuwa na msaada katika uhalifu wao.

''Tutatathmini kilichotokea, na tutachunguza kama magaidi hawa walikuwa na washirika, na tutafanya chochote kinachohitajika kuhakikisha usalama wa watu'', alisema rais Obama.

Mripuko kwenye mbio za Marathon za Boston iliuwa watu 3 na kujeruhi zaidi ya 180

article-2311443-1965519A000005DC-483_964x542.jpg


Polisi wamesema walikuwa wakianza kukata tamaa katika operesheni yao, hadi pale walipopigiwa simu na raia ambaye ameiona damu kwenye boti yake, na kumkuta mshukiwa ndani ya boti hiyo akiwa ametokwa na damu nyingi.

article-2311443-19650BCC000005DC-84_470x423.jpg

Ufanisi na ushiriki wa jamii ni muhimu kukamata wahalifu sayansi na technologia ni jambo la msingi kwani wenzetu wana CCTV CAMERA almost alover hizi zinawasaidia sana kupata picha na real situation inavotokea kwa matukio muhimu kama muhimu
 
Kwan walifahamu adui yao amejipanga vpi?kwa osama waliingia wangapi?
Mkuu.@RGforever FBI wabovu kumkamata mtu wamekwenda kwake huyo kijana mwenye umri wa miaka 19 na wanajeshi Elfu 9 kumkamata mtoto wa miaka 19 huo ndio uozo mkubwa na udhaibu wa ulinzi wa Marekani nchini mwao hawafanyi kazi vizuri kabisa. Walivyokwenda kumkamata huyo kijan utafikiri wanakwenda kupigana vita ahhh? huo ndio udhaifu mkubwa wa ulinzi wa amerika haswa nchini mwao pumbavu kabisa.
 
Mimi ni mkristo ila Kitendo cha kuita Muslim terrorist sio kizuri.Mimi hayo nimeyasikia USA na kila dini Ina Extremist .We need to respect people's faith

...hiyo O ya mwisho ya MAZOO iweke katikati,,,ndio utajua sababu ya kuyaandika hayo
 
Fundisho muhimu sana kwa jeshi letu la polisi. Usalama wa raia na mali zao hauji hivi hivi bila ushirikiano wa jamii husika.
Sio hawa polisi wetu wanaua hawawajibiki wanapenda rushwa nk raia mwema anaweza kutoa taarifa muhimu ya mhalifu anayetishia amani ya mtaa wanamkamata baada ya masaa 2 wanamuchia baada ya kupewa kitu kidogo. polisi inabidi wabadili image yao kwa jamii yetu. Wapi watuhumiwa wa padri? Waliomjeruhi ulimboka? Waliomuua mwangozi?? Seriously police needs 2 change

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
FBI wamefanya kazi gani ya kijasusi saaaana hapa?

Baada ya kulipua marathon vijunki vimeenda ku stick up duka la Seven-Eleven na kuiba magari na kurushiana vibomu na polisi tena winji winji bila kujibadilisha toka siku ya marathon, sasa hapo polisi gani angeshindwa kuwadaka hawa? Walichofanya cha ajabu sana hapa FBI sikioni.
 
Mkuu.@RGforever FBI wabovu kumkamata mtu wamekwenda kwake huyo kijana mwenye umri wa miaka 19 na wanajeshi Elfu 9 kumkamata mtoto wa miaka 19 huo ndio uozo mkubwa na udhaibu wa ulinzi wa Marekani nchini mwao hawafanyi kazi vizuri kabisa. Walivyokwenda kumkamata huyo kijan utafikiri wanakwenda kupigana vita ahhh? huo ndio udhaifu mkubwa wa ulinzi wa amerika haswa nchini mwao pumbavu kabisa.
We unaona uzembe lakini wenzetu hawa-underestimate kitu. Tukio alilofanya ni la kigaidi hivyo hata kama angekuwa ni mtoto wa miaka 10 bado hatakiwi kuwa-underestimated. Kitu kingine hawa watu wanafuatilia any Lead wanayopata sio hapa kwetu mpaka polisi wamekua wanasiasa. Pamoja na madhaifu yote tuliyonayo kwa vifaa na mbinu lakini tumeamua kuweka siasa kila mahali na ndio inatutafuna.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
si waliomba wenyewe kazi, watimize wajibu wao,

Haianzii na kazi ya polisi tu. Ni mchanganyiko wa mambo mengi kuanzia mitaa kupangwa vizuri, watu kutambuliwa, uwepo wa surveillance cameras mitaani, wananchi kuwa na elimu, vitendea kazi, mafunzo ya polisi. Nadhani mmeona kuwa walitumika SWAT ambao ni polisi wenye mafunzo na vifaa maalum kwa kazi maalum.

Tusiwavunje moyo polisi wetu kwa kuwatolea kauli ya kejeli. Wanafanya kazi kwenye mazingira magumu sana.

Wakati Marekani kila polisi ana gari lake la kufanyia kazi, sisi polisi wetu wanapanda dalala kwa kubishana na konda awasamehe nauli kwa sababu ya uniform.

Wakati Marekani kila polisi anapewa radio communication equipment, sisi polisi wetu wanatumia simu zao kwa credit zao kuwasiliana.

Kitu pekee ambacho polisi wetu wanapata kwa kiwango kinachotosheleza ni uniform na viatu tu.

Kwahiyo tusitegemee muujiza kwenye ufanisi kama hatuinvest kwenye usalama kwa kuwawezesha polisi wetu kupata mafunzo na vifaa vya kisasa.
 
Terrorist wa Kiislamu tayari yuko ndani.

Na huyu terrorist wa Kikristo je? GAIDI mkuu kabisa Africa ambaye hatasahaulika milele kwa kuua Waafrica kwa mamilioni na ambao bado Waafrica wanaendelea kuuawa chini ya mipango yake aliyoiacha ni NYERERE. Aliua Wazanzibar wasiopungua 20,000 kwa kumtumia Okello, mauaji ambayo yalikuwa ya kikatili haijapata kutokea kwenye historia ya Africa yaliyofanywa na Muafrica mwenzao aliyekuwa anatumiwa na Kanisa Katoliki pamoja na mabwana zake Wazungu na Wamarekani. Wazanzibari zaidi ya 200 walichomwa moto kwenye tanuri wakiwa hai kwenye mauaji hayo. Akaua Watanzania na Waganda wasiopungua 100,000 kwenye vita ya Kagera ili kumuondoa Idd Amin kwa maelekezo hayo hayo ya mabwana zake. Mauaji za DRC ya mamilioni ya watu yana mkono wake kupitia kwa Kabila. Mauaji ya kimbari ya Rwanda yana mkono wake kupitia kwa Kagame. Vita aliyopigana Museveni na kuua Waganda kwa maelfu ili aingie Ikulu ina mikono ileile iliyojaa damu ya Nyerere. Vita ya Biafra kule Nigeria ambapo Wakatoliki walitaka kujitenga na Serikali halali ya Nigeria ili wasiwe chini ya uongozi usiokuwa wa Kikatoliki ulifadhiliwa na Nyerere kwa kutumia rasilimali za Tanzania na kuua mamilioni ya Wanigeria.

Huyu Nyerere ndio GAIDI wa kujadiliwa ili tulinusuru bara letu kutoka kwenye makucha ya ugaidi yanayoendelea kuwatesa na kuua Waafrica chini ya mfumo wa ukoloni mambo leo badala ya kupoteza muda wetu kujadili vigaidi uchwara tena nje ya bara letu.
 
Mapolicccm matumbo makubwaaaaa, kazi kulinda usalama wa ccm tu.
 
Wanasema walikwisha anza kukata tamaa mpaka walipopigiwa simu na mama mmoja, nasi tujifunze kuvipa ushirikiano vyombo vyetu badala ya kuwa ndo walalmikaji daily!
Utawasaidia vp wakati ukiitwa kuisaidia polisi maana yake ni kwenda ku donate kucha na meno yako? chezeya shushushu wa bongo!
 
Wanasema walikwisha anza kukata tamaa mpaka walipopigiwa simu na mama mmoja, nasi tujifunze kuvipa ushirikiano vyombo vyetu badala ya kuwa ndo walalmikaji daily!
tatizo ni kwamba polisi wetu hawaaminiki, ukiwapa ushirikiano wako kwa kuwapa taarifa za muhalifu ni sawa na kuyaweka maisha yako rehani.!
 
polisi yetu ni chovu mno.!
watu mle ndani ya jeshi sio patriots yani kazi yao ni kupanga madili tu kama wako vijiweni..
tafadhani sana chdm kama mkishika dola naomba msiendeleze hizi itikadi za hawa wenzenu kutumia vyombo vya sheria kisiasa sababu kama tukitaka jeshi la polisi na usalama wa taifa wafanye kazi ni lazima wasiingiliwwe na wanasiasa kwa maslahi ya kisiassa..
jeshi letu liko katika hali mbaya sana..
 
Back
Top Bottom