1960: Vita za kutafuta nguvu, umafia na mikono itendayo miujiza

1970:VITA ZA KUTAFUTA NGUVU, UMAFIA NA MIKONO ITENDAYO MIUJIZA.

Sehemu .03

NIMERUDI!!

Nilipoishia.

Rashid Marangwe bosi wa UTOPIAN GENERAL ENTERPRISES & CO.LLC, Don Rui Acosta mafia kutoka Bolivia na vipenyo wa idara ya ujasusi ya kijeshi na kiraia ya Black African iitwayo "Millitary Intelligence and secret service" almaarufu kama"MISS" Hawa wote wakageuka maadui wa Bw.Robert Kimani kisa maokoto.

Uadui huu nilieleza ulitokana na mambo matatu, Vipenyo wa "MISS" walipewa kazi na Boss wakanuse sakata la maswahiba Bw.Kimani na Bw.Marangwe kutaka kutupana nyuma ya nondo, na wakagundua kesi ilikufa baada ya BSHS.858M kutoka.Waliposhikwa na tamaa wakaanza kumuaandama "mkikuyu" na kuna siku wakampora U$D.5700 walipoenda kulala hawakuamka yaani walilala mazima.

Uadui kati Don Rui Acosta na mkikuyu nao ulihusu maokoto baada ya Mkikuyu kugoma kumpa kiramba mchuzi mafia huyu ilihali hakujua kuna kijana wa huyu mafia amepewa hifadhi ya kudumu kutokana na makala zake gazetini.Halafu nikaeleza suala la "Mtu wa dili" bw.Rashid Marangwe kukosa Ile tenda ya ujenzi wa apartment kwa BSHS.130Bilion.

Nimelazimika kuwakumbusha maana yamepita masiku lukuki bila kuweka muendelezo, baadhi makumbukumbu yatakua yametambaruka kutokana na shughuli za kusaka ugali.

Tuendeleee........

Wakili Adv.Kevin Odhiambo alijichotea zile Bshs.330M akakwea pipa kurejea kwenye ardhi iliyoumeza mwili wa Dedan Kimathi na Mzee Jomo Kenyatta, na ni hapa hapa Kenya ndipo Mafia Don Rui Acosta aliweka maskani yake kule Mombasa baada ya DEA na wahuni waliopewa vibali vya kulima coca huko Cochabamba,chapare-Bolivia kumnyima uhuru wa biashara zake.

Jamaa alishajua wakili msomi ana pesa hivyo akamchorea ramani ya vita asepe na pesa!Lakini hakujua pesa itafutwayo kwa jasho huwa haiibiwi wala kupotezwa kizembe.Hata wakili nae alikua anaelewa Nini maana ya msoto wa kukosa pesa Sasa amepewa mpunga wake ambao kwa wakati ule Bshs.1 kwa pesa ya Kenya ilikua kama Kshs.38 hivi yaani ile Bshs.330Milion ukiipeleka kwa pesa za Hustler Ruto unapata kama KSHS.8.6Milion yaani milioni nane na laki sita na chenji zake sasa pesa hii unawezaje kubali ipotee kirahisi?Tena umeipandia na ndege kabisa halafu anakuja mtu aje aibebe kizembe!?

Naam ilibidi lifanyike tukio ambalo liliibua kizaa zaa na kuharibu maficho ya Mafia huyu!Bw.Robert Kimani alishamtonya wakili awe makini kuna ametibuama nae kisa maokoto ambayo yeye kachukua hivyo aishi kikachero mambo ya kuagiza bia misitu na kuzungukwa na wana wa Eva akiwa viwanja virefu aache watampukutisha pesa yote maana wakora sio watu.Wakili akaelewa somo maana alikua ni mtu wa kula bata sana kama "MacMuga" kila akidaka okoto.

Lakini wakili hakuacha asili kwa kua jasiri haachi asili na akiiacha asili hana akili.Kwanza akavuta "TOYOTA LAND CRUISER 200 SERIES V8" ukitaka kujua utamu wa V8 waulize Tamisemi kwa nini wanataka kuyanunua kila mwaka?Achana na wasionazo wanaokwambia eti gari za serikali wakati hata bagadu hajawahi miliki.Akanunua mjengo mitaa ya pembezoni mwa Jiji la Nairobi maisha yanataka nini tena?Wakili aliamua kusema na maisha na maisha yakamtii lakini aliishi kimkakati kila aendako "Beretta-92" iko kwa kiuno ikimngoja mnoko ashikwe umbea na aneng'eneke na pesa zisizomhusu ashindiliwe vyuma.

Wakili akawa kwenye daftari la doria la maudhurio ya Don Rui Acosta kokote atakapopeleka nyayo zake wanae, ikafika siku ya siku.Naam ni tarehe 23 January 2017 wakili alitoka viwanja akiwa anaingia ndani kwake akakutana na wanoko!Waliokua wakimtamani sana maana ni siku kama sita hivi alitoka kuwagaragaza wahindi f'lani kortini akavuta Kshs.4Milioni hivi, sema wakili nae alikua mtu wa dili za gizani hivyo pesa hazikuvunja mahusiano yake mazuri na mifuko yake.

Wakati akiingia mara Toyota Corolla ikamuovateki na kwenda kuziba njia ya kuchepuka kutoka barabarani kuingia kwake, wakili japo alikua yuko tungi I'll la "Jack Daniel" kama "K-Vant" au "Snake Venom" zikakata maana harufu ya damu yake kumwagwa ilinukia puani akavuta bastola na kuteremka hakuuliza so unamjua mlevi likija suala la kujihami eeh!!? Shimo dogo ataruka kutoka chanika hadi mbagala.Alipoteremka jamaa wa kwanza alikua anashuka akala ya kichwa mwenzake akataka kujibu nae ya kichwa weeee!!! Dereva alitia gia akala kona akasindikizwa na mvua ya risasi pesa za bure zikaondoka na pumzi ya watu watatu maana zile alizowasindikizia risasi moja wapo ilimpata jamaa aliyekua siti ya nyuma wakazika.

Likafata balaa bastola haikua inamilikiwa kihalali halafu polisi wakaja kudai waliouawa sio majambazi bali ni polisi daaah!!Wakili yakamkuta, msomi ni msomi tu wakili akacheza kama pele ni baada ya kuona polisi wanataka kumfukarisha weee!!Pesa ni tamu bwana ni kweli mmoja ya wale majambazi alikua ni kachero Naam kachero mkuda na wakili alitonywa na kwa vile alijua aliewatuma akauza ramani ya vita.

DON RUI ACOSTA alikuja kudakwa na FBI akiwa kwenye maficho yake Mombasa pesa zisizomhusu zikamgharimu na kumnunulia hifadhi ya kudumu jela alitoka mwaka jana hana hamu na Africa!Nilisikia wababe wa SINALOA CARTEL walimpokonya uhai japo sijajua ilikuwaje.

Bw.Robert Kimani nae alikua mtu wa ndumba bhana!!Kusikia wakili alivamiwa na wakora akajua zamu yake haiko mbali akaenda kwa sangoma wake.Sangoma hakuwa tapeli akamuuzia kinga

Kuna siku vipenyo wakamdaka akiwa klabu anakata K-Vant zake wakambena hadi nyumba salama akala kibano shida yao ilikua pesa akawaambia waende ghetto akawape likawa kosa tamaa wakakubali.Siku ya pili yake ilikujaga kubainika wale jamaa walionekana klabu Moja ya usiku wakinywa maji, simaanishi maji kama ya kandoro?Namaanisha maji taka yenye kemikali na kutunzwa kwenye chupa safi halafu maiti zao zikakutwa ufukweni wa bahati ya Atlantiki na ndinga lao NISSAN PATROL NISMO limepaki ilikuja kubainika walikufa kwa kukata maji kupita kiasi japo kuna watu walihusisha sakata hilo na dini za kiafrika.

Vipenyo wakajua kuna watu wa kuwagusa ila sio Bw.Robert Kimani lakini unadhani ndio walimuacha? Boss alitoa maagizo awindwe na arudishwe mavumbini sababu alikua adui yake kisa sanduku la kura 2005.

Unajua unaweza jiuliza nini kilitokea 2005?

Bwana pale Black African kuna chama tawala kinaitwa "Constitution Movement Unity" Boss aliyeingia 2006 alikuwa na uadui na Boss wa sasa kisa maokoto!Wakati wa harakati za kumtafuta atakaepeperusha bendera huyu boss wa sasa alionekana ana mtaji wa watu na anaweza kushinda ndio hapa mwandishi Bw.Robert Kimani akaitwa na kupewa tenda ya kuharibu jina la mtu.

Siasa hizi bhana!

Huyu boss wa sasa alikua na machafu yake!Hayo machafu Boss wa zamani aliyajua maana alikua na "good spy network" wakampa tenda mwandishi akayabwaga hadharani kwamba Boss wa sasa alikua anamla mke wa mfanyabiashara mmoja ambae alikua n it swahiba wake, chama kikapata kashfa akakatwa na Boss wa zamani akapewa nafasi na kwa vile chama kilikua na mpini uchaguzi ukafanyika akaingia kwenye enzi.

Hii ishu Boss aliishi nayo tu mm oyoni Alijiapiza lazima alipe na alikua mtu wa visasi balaa lakini unadhani ndiyo ilimfanya mwandishi asomewe huku bila kushtakiwa?

Noooooo!

Kuna maokoto Bshs.3Trilioni za mwaka 1998 mwandishi alikua anataka kuleta nongwa zake!

Narudi
_____________________________________
Mussa Mayagila Daniel
(iamindustrious)
There is story in everything

Sent from my CPH2385 using JamiiForums mobile app
Safi
 
1960:VITA ZA KUTAFUTA NGUVU, UMAFIA NA MIKONO ITENDAYO MIUJIZA.

Sehemu 04.

Nimerudi.....

Bado tupo wiki moja kabla ya siku yenye utata sana, najaribu kueleza baadhi ya visa muhimu sana ili kuelewa kichwa cha makala hii.Naam najaribu kutafuta namna ya kufanya ujue namna ambavyo watu wachache kwa tamaa zao wanaweza kuweka rehani pumzi ya mtu na mali za umma ilikutafuta nguvu.

Naomba turudi tena mpaka 1998, hapa tunakutana na Bw.Robert Kimani akiwa katoka kumaliza elimu ya uandishi ngazi ya cheti jijini Nairobi.Kiasili ni mkenya lakini kuzaliwa ni raia wa Black African(code).Ajira yake ya kwanza alikua ni kama ripota wa kujitolea anaenda eneo kusaka habari na kuja kuziuza kwenye media kubwa kupata tongue la ugali na kazi hii ilimpa koneksheni matata!Koneksheni hii ya kukutana na Bw.Rashid Marangwe bosi wa UTOPIAN GENERAL ENTERPRISES &CO LLC, kulikua na tangazo la kampuni hii ambayo ilijihusisha na udalali kwa serikali ambapo kama serikali ilihitaji watu wa kutekeleza mradi f'lani basi kampuni ilipewa tenda then anapewa chake.

Sasa ikatokea tenda!Naam tenda adhimu, tenda ya kutakata mtakato wa kutakasika.

Benki kuu ya Black African ilikua inashikikilia akaunti moja ya kampuni ya kifaransa ambayo ilikua na kesi na wananchi wa kijiji kaskazini mwa nchi, akaunti hii inasadikika kulikua na USD.400M ambazo Ilikua zinangoja kesi kati ya kampuni hiyo na wananchi iamuliwe ili pesa hiyo ama apewe mmliki au sehemu yake wapewe wananchi kama fidia ya kumkodishia mmiliki(kampuni ya kifaransa) maeneo kadhaa kwa shughuli za nishati ya mafuta, gesi na madini.

Sasa muelekeo wa kesi ulikua unaenda kutoa rushwa wananchi wabwagwe!Naam mahakama za kiafrika zinajulikana? Sasa Kuna watu waliona sio sawa ukizingatia huyu muwekezaji alikua anadaiwa fidia ya kuwahamisha Wananchi Ili afanye shughuli zake, alikua na makubaliano ya kuwapa asilimia 10% kila mwaka kwa kipindi chote cha miaka 10 ya uwekezaji wake, lakini pia shuguli za madini mnazijua mali ikitoka ardhini yanabaki mashimo, ardhi kuharibiwa na mengine.

Sasa hii kesi ilikuja sababu mkataba ulisainiwa mwaka 1990 na huo ulikua mwaka wa 8 na ilibaki miwili uishe na huyu bwana muwekezaji ambae ni kampuni ya kifaransa hajalipa deni la 10% wala fidia na a mazingira yalionyesha alitaka kuingia mitini mahakama ikatoa amri mali zake zishikiliwe.Ndio hapa USD.400M zikaingia mikononi mwa benki kuu sababu katika mkataba pesa zote za mauzo ya madini zilkua lazima ziingie benki kuu halafu ziende kunakohusika.Huu mkataba ulikua una visa vyake bhana!Tofauti na makampuni mengi ya kimaghatibi ambayo watachimba na kuuza msione hata shilingi na kodi wanaweza wasilipe pia sababu ya koneksheni na wakubwa.

Lakini huyu muwekezaji aligombana na wakubwa, wakubwa wakamuwekea ngumu bado akakaza kamba na katikati ya kukaza kamba wakaja watasha.Naam waliona tobo la kujichotea mipesa isiyowahusu.Hapa akaja Boss wa sasa na Boss wa zamani, walikua maswahiba!Uswahiba ulikuja sababu ya dili.Mr.Rashid Marangwe ndie kiunganishi wao.

Kesi wakati iko mahakamani na muwekezaji alianza kuona hatoboi na akaunti yake benki kuu ina pesa nono ambayo alijua akicheza haipati na mazingira ya kesi na walionyuma ya kesi yakamshawishi kucheza rafu.Katika kucheza rafu huku akamtafuta kibaka bila kujua lol!Naam alitaka kutumia koneksheni zake na watu fulani ile pesa waitoe benki kihuni ili kesi ikiisha na akashindwa asiwe na cha kupoteza.Hapa akamfata Bw.Rashid Marangwe.

Rashid akamvuta waziri wa fedha ambae ndie boss wa zamani halafu boss wa sasa alikua ni mtu nyeti ikulu tena ofisi ya bosi na alikua anashitikiana na bosi wa nchi kuiba na kuficha nje.Boss wa wakati huo alikua hausiki na hili sakata la mwekezaji na wananchi ila kuna watu nyeti kwenye wizara za sheria, madini na biashara ndio walikua wana pasenti zao na hawa ndio waliochochea kesi.

Ramani ya vita ikachorwa London, halafu ikahamia hapa bongo na mwisho ikaenda kutekelezwa Black African.Ilipangwa hivi.

Kwa kua katika mchoro yupo mtu anashea siri za wizi na Boss?Wazitoe pesa kwa amri ya Boss ambae walipanga kumkatia kiasi fulani Ili awalinde watu wa benki na muwekezaji.Hili Dili Boss akalipenda maana aliahidiwa okoto tamu kwelikweli na ili mambo yasiwe mengi ikaamuliwa pesa itolewe "cash" yaani taslimu bila kupita kokote yaani mzigo unatoka benki kuu likiwa packed kwenye begi.Then watu maalumu wa muwekezaji wataufata hapo na kuupeleka mafichoni halafu ndipo watagawiwa walioshiriki.

Nilisema wamemshirikisha kibaka!?Naam Rashid alikua chid kweli kweli, sasa ramani ya vita ilichotwa ukabaki utekelezaji.Wakati wanangoja siku ifike yakatokea ya kutokea kati ya Rashid na Boss wa sasa.Hawa walizinguana kitambo ila walikua wakikutana kwenye Dili mambo fresh ila hili dili lao lilikua nono halafu tamu!Naam tamu zaidi ya kula tunda kimasihara, lilikua tamu zaidi ya goli la kumtia mimba bae wako.

Ugomvi ulikuja katika magawiano ambapo ilikubaliwa Boss wa sasa alidai mkuu wa nchi wakati huo alitaka USD.100M muwekezaji alijitahidi kumshusha hadi kukubaliana lishuke hadi U$D.50M, halafu yeye alitaka U$D.20M wakati Bw.Rashid Marangwe aliahidiwa U$D.15 na Boss wa zamani hiyohiyo U$D15M halafu muwekezaji atatoka na U$D.300M safi bila shida walikubaliana hivyo.

Lakini mtu wa dili ni mtu wa dili siku zote ukikaanae kikabaila utamjua tu.Bw.Rashid Marangwe alikua anajiuliza yaani mimi niwafate wao(Boss wa zamani na Boss wa sasa) halafu mmoja nilipwe nae dau sawa na mwingine tena adui-rafiki anizidi?Aliikataa moyoni hiyo mambo na akaanza nusanusa zake kujua huendankina kitu na uzuri alikua na watu fulani idara ya kaunda suti akaanza kunusa.

Naam yakajulikana!Naam Bw.Rashid Marangwe akagundua katika ile U$D.50M ya mkuu wa nchi kuna U$D.30M ya Boss wa sasa weeel?Yaani Boss wa sasa aliwapiga kudai mkuu wa nchi sijui anataka 100M kumbe fiksi tu Mzee alikua anataka only U$D.20M tu!Kwa hiyo Boss wa sasa katika Dili la kushirikishwa alikua anaenda kuvuna U$D50M yaani ile 20 ya kwake na 30 ya cha juu kupitia mgongo wa mkuu wa nchi.Bw.Rashid Marangwe akatuliza fuvu na kuchora ramani mpya ya ku-hack mchongo kimya kimya na akamshitikisha boss wa zamani ila hakumwambia ile fiksi.

Mchongo ulikua vizuri Boss wa zamani akakubali kumsaliti swahiba wake Boss wa sasa.Tarehe ikawa kama iko mbali hivi?Rashid akaona ngoja afanye jambo kushinikiza mzigo utoke mapema, hapa ndipo akatafutwa mkikuyu Robert Kimani akafanye jambo lake kwenye media.

Naam Robert yeye hakukjuzwa kiundani yeye aliambiwa tu aandike muwekezaji anataka kukimbia na pesa zinazoshikiliwa ili kukwepa kuwalipa wananchi hivyo mahakama iharakishe hukumu kabla hawajaachwa manyoya.Na kweli habari ikaandikwa weee! watu wakafura! Wakaomba rais aingilie kati na Rais kuona hivi akawaambia kamati ya ulaji,mnangoja nini?Ramani ya ulaji si iko tayari?

Wakajibu "ndiyo!"

"Basi toeni chakula tule tuoshe vyombo kabla msosi haujachacha!"

Naam hiki ndio alikua anakitaka Bw.Rashid Marangwe so taratibu zikafanyika lakini kihuni.Naam mtu wa dili alicheza na Gavana mzigo ukatolewa na kuwekwa katika masanduku 10 yenye ujazo ikawekwa ndani ya gari moja halafu likaandaliwa gari la pili likiwa na mzigo mtupu yaani masanduku matupu.Then team ya muwekezaji ikaja ikapewa gari lenye masanduku matupu na escort team ya kutosha wakaondoka zao halafu huku nyuma mali wakapewa team ya Rashid Marangwe na mzigo ukanyanyuliwa moja kwa zote mpaka airport ukapakiwa kwa ndege huo cayman islands kufichwa.

Usiku ule ulikua wa moto pale Black African bhana weee!!

kwanza zile escort ziliishia sehemu Fulani zikala stop ikapokea team maalumu ya muwekezaji hadi mafichoni yaani escort haikufika mwisho wakageuza kurudi benki kuu.Hili likawa kosa baya sanaaaaaaaaaaaaaa!!!!

Naam ubaya ulikuja nusu saa baada ya kufika huko mafichoni watu wakafungua masanduku wakakuta matupu!Weeeeh!!Nusura watu wapate uchizi kama sio utaahira.simu zilianza kutembea kwa kasi juu ya dili hili na habari zikafika kwa bosi wa sasa akadata inawezekanaje?

How!!?
Why!!?
Since when!!?

Usiku ulikua zaidi ya kiza U$D.400M zimetoweka hawakuvamiwa na mbaya zaidi waliipiga stop escort team isifike mwisho wa safari hii ilitosha kuwaangushia jumba bovu muwekezaji na Boss wa sasa,

Mkuu wa nchi akafura!!
Boss wa zamani akafura!!
Mr.Rashid Marangwe n'tu ya dili nae kinafki akafurah!!

Boss wa sasa na muwekezaji roho juu ni kweli walipewa mzigo japo hawakuhakiki kama ulikuwemo, Hilo likawa kosa lao pili kitendo cha kupiga stop escort team kikatosha kuthibitisha nia ovu wamecheza dili kuficha mzigo kama sivyo Kwa nini walizuia escorts team?

Narudi...

______________________________________
Mussa Mayagila Daniel
(iamindustrious )
There is a story in everything
iamindustrious shukurani sana
 
1960:VITA ZA KUTAFUTA NGUVU, UMAFIA NA MIKONO ITENDAYO MIUJIZA.

Episode ya 05

Nimerudi.

Kumbukizi-Tupo wiki moja kabla ya usiku wa dhahma kubwa!Kwa Mr.Robert Kimani.

Sometimes 1998

Usiku huu Boss wa nchi(wa 1998), Boss wa zamani(Alikuwa waziri wa fedha 1998) na Boss wa sasa(Mtumishi adhimu ofisi ya rais 1998) pamoja na mtu wa dili Mt.Rashid Marangwe walikua wapo ikulu, ni usiku huu pia ndipo zile U$D.400M zilipaswa zitolewe ili kila mtu akafe na fungu lake anapopajua.

Kumbuka Boss wa nchi alitaka U$D.20M lakini katibu wake mkuu wa ofisi yaani(Boss wa sasa) kwa sababu ya tamaa akawaeleza wenzie kuwa bosi anataka U$D.100M lakini yule muwekezaji wa kifaransa akamshusha hadi U$D.50M, hivyo huyu bwana katika hili dili alikuwa ana uhakika wa kuondoka na U$D.50M.Boss wa zamani ambae wakati huu 2016 ni marehemu aliahidiwa U$D.15M sambamba na Mr Rashid Marangwe ambae nae alikuwa anaenda kupewa U$D.15M, Hivyo usiku huu wakiwa wanasubiri "Alert" kutoka kwa muwekezaji pesa zako Wanazipataje stori zilikuwa zikiendelea taratibu kama hakuna ramani ya vita ya kikabaila iliyochorwa na manyamela wawili Bw.Rashid. Marangwe na Boss wa zamani.

Nilieleza kuwa ile "Escort Team" ya benki kuu Kuna .aeneo walifika wakapigwa stop na kutakiwa kurudi kwani kutoka hapo ilikuja Team ya ulinzi mpya kupeleka mzigo?Bila shaka mnakumbuka!Baada ya ile "Team" kurudi benki kuu gavana akanyakua simu na kumpa taarifa waziri wa fedha (Boss wa zamani) kuwa alitekeleza maagizo kama alivyoelekezwa ila anashangaa "Team" ya ulinzi imerudishwa kabla ya mzigo kufikishwa eneo husika.Hapa kwanza Waziri wa fedha(Boss wa zamani) akajifanya hajui lolote akawapasha habari wenzake na habari hii ikamshangaza Boss wa nchi na kama alikuwa na machale akatoa angalizo!

Naam alimpa angalizo Katibu wake mkuu(Boss wa sasa) kuwa isije ikatokea wakavamiwa njiani pesa ikapotea? Akasisitiza ikitokea mambo hajaenda ndivyo sivyo hatawaelewa kabisa!Boss wa sasa akamhakikishia kuwa mzigo utafika salama na asiwe na wenge akae kwa kutulia pesa ipo.Naam hakujua kua mjini siku hizi sio tu shule, bali ujanja wa kusaka fursa na kutumia nafasi hata iwe ndogo vipi, lazima uitumie kutengeneza pesa!Namaanisha mjini shule ikizidi unaweza kutumia akili nyingi kuliko maarifa ukaharibu.

Ndicho alichokifanya Boss wa sasa asijue kuna wenzie ujanja unawafanya mkono uende kinywani na baadae waende chooni, alisahau kuna wengine hawana elimu kubwa za vyeti ila wana elimu kubwa kuhusu mapambano ya kuhakikisha mifuko inajenga mahusiano mazuri na pesa!Wako tayari hata kuuza nafsi ya mtu kisa pesa na usiku huu ilikuwa zamu yake kumkuta ya kumkuta.

Stori ziliendelea Bw.Rashid Marangwe na Boss wa zamani walikua wanajua kitakachojiri dakika chache zijazo wao, walikuwa hawana presha!Kwanza itoke wapi wakati pesa washabeba!?Pili, adui yao anaende kuanguka kisiasa ili kurahisisha harakati zao za kuukwaa U-Boss wa nchi katika uchaguzi wa 2000.

Naam robo saa baadae simu ya Boss wa sasa(Katibu wa rais 1998) ikaita ile kupokea akakutana na taarifa ya maboksi waliyoyabeba kuwa matupu!

Sio tu alichanganyikiwa, ni kama vile alirukwa na akili na kupata vigezo vyote vya kupelekwa Milembe.Kikao kikabadilika na maswali yakaanza.

Imewezekanaje pesa ikatoweka!?
Kwa nini mlizuia Escort Team?
Ni vipi hizi pesa zikapotea ili hali hawajavamiwa?

Maswali haya yakakosa majibu na katikati ya sintofahanu hii, Siri iliyokwisha julikana na manyamela wawili juu ya upigaji wa Boss wa sasa ikawekwa hadharani na kumkaanga bila mafuta Boss wa sasa.Ni baada ya Boss wa nchi kunyakua simu na kumtaka mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo achague moja kati ya matatu.

1.Kutoliona jua la kesho asubuhi?
2.Kuleta gawio lake U$D.20M?
3.Kesho yake kuamkia korokoroni kwa tuhuma za kutorosha pesa zilizozuiliwa na mahakama benki kuu?

Ni hapa ndipo Bw.Rashid Marangwe akajifanya hakua anajua kama gawio la Boss ni U$D.20M na sio U$D.50M kama katibu wake (Boss wa sasa) alivyowaeleza, kikao kikazidi kuwa cha moto! maana muwekezaji aliomba hili jambo liishe kimya kimya na kama hiyo U$D.50M atampa usiku huohuo lakini Boss wa nchi akakaza kamba bila kulegeza

"Sitaki U$D.50M nataka gawio langu halisi U$D.20M tofauti na hapo chagua moja kati ya matatu niliyokupa!"

Hapa kwanza hata muwekezaji nae alishangaa!Inakuwaje mkuu wa nchi atake pesa pungufu ya gawio halisi walilokubaliana tena kalishusha kutoka U$D.50M hadi U$D.20M kivipi!?Wakati awali alitaka U$D.100M?" Msgabgao huu sio kwamba alimwambia Boss wa nchi simuni la hasha najaribu tu kudhani ama kuhisi huenda alijiukuza hivyo sababu baada ya kupewa machaguo matatu alimpigia simu Boss wa sasa(katibu mkuu wa rais), alimpigia ili ajue imekuaje Boss kabadilika na kutaka pesa pungufu zaidi?

Kama ni togwa lilishapata nzi, ugali moto mboga moto na njaa na tumbo linakulaumu, Boss wa sasa alikuwa kajipeleka machinjioni mwenyewe kwa kutoa mhakikisho asio na uhakika nao, kuleta tamaa kwa wakora na wahuni waliopewa teuzi na mtu wa dili ambae alijua kuitafuta pesa kuliko pesa ilivyojua kumtafuta yeye.

Simu ile akataka kupokelea pembeni maana alishajua kinachoe dabkumtokea lakini Boss wa nchi akataka simu ipokeleww hapo hapo kama ni kusikia wote wasikie hakuna kwenda chemba!Muwekezaji swali la kwanza halikutabirika na naweza kusema ama lilikua swali, sikitiko, tishio au mshangao.

"Kwa hiyo siku hizi umekua kama ulivyoamua kua!"

"Kivipi?"

"Mzee kasema anataka U$D.20M na sio U$D50M kama ulivyonieleza, fafanua imekuaje?"

Swali hili akakosa majibu, muwekezaji akaendelea kutapika nyongo

"Nilikueleza mapema uwe makini kuhakikisha mzigo unakaguliwa kabla hujaletwa na nilikuambia tutumie vijana wangu wako smart sana ukanihakikishia haina haja utatumia watu wako wa mfumo, haya watu wako wameniletea masanduku matupu!Pesa ziko wapi!?"

Hili swali nalo akabaki akibabaika sababu kila kitu lilikua kinaenda kumuangukia yeye na muwekezaji akajitapa.

"Unafukiri unanikomoa!?Umetumwa na wenzako wa sheria, madini na biashara eeh!?Sasa subirini nyani nyie.........mimi nitawalipa wote niliosaidiana nao kuitoa hiyo pesa ambayo wewe umeibeba halafu nitashugulika na nyingi katika namna inayotakiwa nyani wewe!"

Mazungumzo yote haya Boss wa nchi aliyasikia vizuri na yeye ndio akasanuka kumbe kuna watu ndani ya serikali yake wanajua hili dili?Akahisi huenda nao wana gawio lao katika huu uwekezaji wa mfaransa?Akajua pia kumbe huyu katibu wake aliwaokota wenzake ili ajipatie fedha za bure?

Mkuu wa nchi alifura kwelikweli na katikati ya hasira hizi muwekezaji akapiga tena simu akaipokea 'Nina pesa ipo Bahamas nieleze nikuwekee wapi pesa yako!?"

Boss akampa namba ya akaunti na nusu saa tu akapokea taarifa kutoka kwa mtu wake kuwa kuna U$D.50M imetumwa kutoka America, hapa bosi ikabidi amhoji katibu wake vizuri imekuaje yeye alipwe "U$D.50M" wakati aliomba apewe U$D.20M?Kwa kifupi usiku huu jumba bovu lilimuangukia (Boss wa sasa) na katika maelezo haya ikajidhihirisha huenda huo mzigo wa hela anao yeye.

1.Vijana waliofata pesa benki ni WA kwake.
2.Ni yeye ndie alitoka amri Escort Team igeuze mzigo utapelekwa na watu wake.
3.Kitendo cha kutaka kuwapiga wenzie cha juu.
4.Ukaribu wake na muwekezaji pamoja na kitendo cha muwekezaji huyo kukubaki kirahisi kuwalipa pesa yao bila shida olihali pesa imepotea katika mazingira tata.

Mambo haya yakaleta hitimisho kuwa ama Boss wa sasa kawasaliti wenzake na kutokomea na pesa au Boss wa sasa na Muwekezaji wanawaletea maigizo tu wakati pesa wameficha!Naam usiku huu ilikuwa mchungu kwa Boss wa sasa sababu aliyakoroga kotekote.

Bw Rashid Marangwe na Boss wa zamani(waziri wa fedha 1998) nao wakapewa magawio yao usiku huohuo ili kutuliza hali kesho yasije yakaamkia kwenye magazeti na runinga hali ikazidi kuwa tete.

Lakini malipo haya yalikuwa ni kama rambirambi kwa ajili ya waziri wa madini!

Lakini malipo haya yalikuwa ni kama rambirambi kwa ajili ya waziri wa sheria!

Halafu malipo haya yalikuwa ni ujumbe tosha wa onyo kwenda kwa

-Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo
-Waziri wa biashara na uwekezaji
-Vigogo wote waliopokea rushwa kukamilisha uwekezaji huo akiwemo Boss wa sasa kuwa pesa alizowahonga watazitapika maana hawa wote walikua wako nyuma ya hii kesi na ukichanganya pesa yake imepotea aliamini kabisa Boss wa sasa aliuza ramani ya vita kwa wenzake wakaondoka na pesa.

Asubuhi iliyofuata nchi ikaamka na bendera nusu mlingoti, waziri wa madini na waziri wa sheria walipokonywa uhai kikabaila!Naam mmoja alikufa kwa Stroke na mwingine ajali wakati anatoka kwenye harakati za kukata upwiru sirini licha ya kuwa na mke tena pisikali matata.

Ndege wawili wajanja wakaondoka kwa jiwe moja! Muwekezaji akatangaza vita, lakini asijue anazidi kujikaanga tu bila kujua!

Naam Bw.Rashid Marangwe n'tu ya dili yeye kila tatizo huona fursa ya kujichotea mipesa isiyomhusu, kila aliona tatizo anawaza kuligeuza fursa wakala mipesa.

Natamani niwaeleze kisanga kipya baada ya tukio hili lakini nitawachaganya!Nitawaeleza kwa kifupi tu.

Ile simu ya muwekezaji kwa Boss wa sasa Rais, Boss wa zamani na Bw.Rashid Marangwe si waliisikia?Naam kesho yake wakaamka na bendera nusu mlingoti?Bw Rashid Marangwe mtu wa dili akamtonya Boss wapige mihela kwa muwekezaji sababu walijua licha ya Vigo hivi kuonekana vya kawaida lakini kiuhalisia vilisababishwa na " skilled and most talented Assassin's" waliotinwa na muwekezaji.Wakati Wananchi wanahaha kujadili vifo wakati magazeti yakiripoti waziri wa madini amefia ajali akitoka kuvunja amri ya saba kwenye torati wenzako huku walikuwa wanajichotea mapesa tu!

Mchana kweuoe muwekezaji akapokea simu kutoka kwa mtu asiejulikana na kumtaka afike mahali fulani au akaidi azikwe!Muwekezaji akaenda mpaka kule alipofika akala pingu mfuko mweusi akatupwa kwenye buti la Mercedez Benz safari mpaka ofisi za kaunda suti.Huko akakutana na Boss wa nchi!Naam faili lake likafunguliwa na akasomewa tuhuma zake ambazo alishindwa kuzikana sababu hiko chumba alichokuwepo alihisi yupo buchani na kilichomshtua ni kitendo cha mkuu wa nchi kutojali mazingira yenyewe.

Elewa hizi zilikuwa ofisi za siri za kaunda suti maalumu kwa mateso kwa wale watuhumiwa walio tayati kuvuka magari wa kifo bila kutoa siri za uhalifu wao na nani anawatuma na kwa sababu gani?

Chumba kulikua kimejaa damu na maiti za watu waliokatwa vichwa au kupasuliwa matumbo viungo vyote wazi, muwekezaji akaamini kakutana na jehanamu ya duniani.

Akapewa masharti kwanza zile pasenteji za uchimbaji madini am azo Vigogo walikuwa Nazi katika ile kampuni kuanzia siku hiyo ni mali ya Boss wa nchi.

Ile pesa walalahoi wanayomdai awalipe ili kesi ifutwe kuepusha kutiwa hasara zaidi.

Kwa kuwa amehusika na mauaji ni lazima alipe fidia ili vyombo vya ulinzi visimsumbue sababu ushahidi alikuwa nao kuwa mawaziri wake hawajafa vifo vya kawaida na Uzuri alishakiri na hapo alirekodiwa.

Muwekezaji mpaka anatoka hizi ofisi alikuwa ameshatia U$D.200M, alipotoka wiki moja baadae wananchi wakapewa pesa yao kama Bilioni14 hivi kesi ikafa kifo cha mende lakini sirini muwekezaji aliongezewa miaka 10 ya kuendelea kuchimba ili kufidia mamilioni ya Dollar aliyopoteza ila asilimia 30 za mapato alipewa Boss wa wakati huo ambae nae aligawana na mtu wa dili Mr.Rashid Marangwe na Waziri wa fedha(Boss wa zamani)

Naam Boss wa sasa aliachwa?Aachwe ili iweje? Mwezi mmoja baadae akajiuzulu sio kwa hiyari, akapokonywa vyeo vyote serikalini na chamani na kubaki joblesi tu, alipewa onyo kali akijitoa ufahamu na kuanza kuropoka kifo ni mali yake ikabidi anyuti tu!

Sirini akaanza kufatilia ajue ilikuja kuwaje pesa ikapotea na yeye hakuhusika!?

Naam, nadhani sasa mmelewa kwa nini Boss wa sasa alishughulika ipasavyo na Mr.Rashid Marangwe na Robert Kimani kwa kuwa ushiriki wao kwenye hili sakata la 1998 na baadae 2005 wakageuka maadui wa Boss wa sasa.

Naomba turudi ule usiku wa dhahma.

Narudi....

_____________________________________
Great Industrious
iamindustrious
There is a story in everything

Sent from my CPH2385 using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: K11

Aminia babake, haramu haionjwi, Na pesa Ndio mungu pekee mtawala duniani.Sio mbinguni lakini.
 
Back
Top Bottom