Mussa D Mayagila
Member
- Jul 3, 2022
- 47
- 81
Kidokezo,
Wakati fulani nimekua nikijiuliza maswali magumu yenye majibu mepesi, na nimekua nikitoa majibu mepesi katika maswali yenye majibu magumu. Ni kwa sababu ni hulka yangu kufikiri na kuyatazama mambo kwa jicho la tatu na mlango wa sita wa fahamu.
Kiu ya binadamu mdadisi siku zote ni kutaka kujua kila jambo lenye utata linalojitokeza katika maisha yake ya kila siku.Aghalabu ndio maana leo hii Dunia inajiuliza baadhi ya maswali magumu.
Nani aliwaua Abraham Thomas Lincoln na John Fritzgerald Kennedy?
Nani alipanga mfanano wa miaka ya matukio hadi mauaji ya John Fritzgerald Kennedy na Abraham Thomas Lincoln?
Je, ni kweli Abraham Thomas Lincoln hakufa ila alipelekwa kuishi kwenye mahandaki ya siri huko Argentina?
Na Adolph Hitler je?
Vipi kuhusu Black budget pale USA?
Vipi kuhusu kitendawili cha JESUITS na BLACK POPE pale Vatican?
Mara nyingi jibu iepesi linalotajwa na wengi kuhusiana na maswali ya aina hii ni moja tu CONSPIRACY na Kuamini ni hadithi za kutungwa.
Aina hii ya maswali ndiyo ilinichochea kufatilia visa vya wanahabari wawili waliotikisa maslahi ya watu f'lani Africa na Marekani familia zao zikaishia kuomboleza.
Genesis.
Sometimes in Black African.
Usiku wa taeehe 27 November 2016, simu ya Mr.Robert Kimani iliita katikati ya usiku mzito wa giza la kifikra lililobeba kila aina ya alamu kumtahadharisha dhidi ya gari aina ya TOYOTA LAND CRUISER 200 SERIES V8 yenye namba ''MISS-711"ambalo lilikua likimundama kwa zaidi ya wiki mbili.
Naliita giza la kifikra kwa vile sijui ndio kujiamini sana kutokana na umahiri wake wa kupangua matukio kadhaa ya kumpokonya uhai au lah!?Sina hakika kama intelijnsia yake ilimuambia hakuna tishio lolote dhidi ya nafsi yake au ndio ule msemo wa siku yako ikifika imefika?Sijui kabisa ila ninachojua gari hii ilibeba hatma ya pumzi yake iliyokua ikiwindwa kutoka 2005 hadi wakati huo.
Kwa kipindi cha miaka 11 huyu bwana kupitia makala zake katika gazeti moja la The Investigator alikua akiwafumbua macho wananchi juu ya kile kilichokua kikiendelea chini ya kapeti ndani ya chama cha Constitutional Movement Unity (CMU), naweza kusema alichagua kuwa kiherehere kwa sababu kuu mbili.
1.Bias(upendeleo)
2.Kiinua mgongo
Ilifika wakati kipimo cha uvumilivu kilipungua na kuwalazimu wahusika kusafiri kiasi cha maili zaidi ya 1220 kumtafuta mtu atakaefanya kazi ambayo Idara nyeti ilishindwa kwa miaka hiyo 11 kiasi kwamba alinatizwa jina la utani na baadhi ya wapenzi wa makala zake na kumwita ''The mastermind" kutokana na kupangua matukio sita ya kupokonywa uhai.
Uandishi wa habari za kiuchunguzi haujawahi kua mwepesi kwa mwandishi huru asieegemea upande wowote au kwa yule aliegemea upande wenye maslahi nae, lakini hawa wote hua hawako salama.Hii inatokana na ukweli kwamba habari waandikazo hua ni tishio la maslahi ya wanaoandikwa.
Usiku huu ulikua na alamu zote kwa Bw.Robert Kimani kua roho yake iko mashakani lakini bado alipuuza ushauri wa mhariri wake wa kutoenda kuonana na Sheikh.Abdullah Mbarouk Shabaan katika hoteli hii.
Kuna nyakati nikifikiria nahisi Mhariri wake alikua na ABC ya nini kinaenda kumkuta mtendakazi wake ila hakutaka kumpa onyo la moja kwa moja akamuacha, nasema hivi kwa sababu siku zote anguko la mtu huletwa na watu wake wa karibu.
Wiki moja kabla ya usiku huo.
Narudi.......
Sehemu ya 02, post 13
Sehemu ya 03, post 30
Sehemu ya 04, post 37
................................................................
Mussa Daniel Mayagila
(iamindustrious)
There is story in everything