SoC04 Je, ni kweli vijana hawana nguvu za kiume?

Tanzania Tuitakayo competition threads
May 19, 2024
13
7
Katika jamii yetu ya kitanzania, kwa siku za hivi karibuni kumeibuka janga la taifa.
Nalo si jingine ni janga la upungufu wa nguvu za kiume, NGUVU ZA KIUME NI NINI? huu ni uwezo alionao mwanaume wa kushiriki ipasavyo tendo la ndoa, na kuweza kumpa mimba yule mwandani wake.
HEBU TUANGALIE JE, KUNA UKWELI JUU YA JAMBO HILI?

1-SABABU ZA KIUTANDAWAZI.
Kwenye mitandao mingi ya kijamii, kumeibuka matangazo mengi ya madawa, yakijinasibu kuwa wanatibu tatizo la nguvu za kiume, huku wengine wakiuza dawa maarufu hapa mjini, kwa jina la MKONGO kuwa ni kiboko ya tendo la ndoa, labda tujiulize kabla ya kuibuka kwa matangazo haya, chanzo kilianzia wapi?

Nb;Picha hii ni kwa msaada wa GOOGLE.

2-KUTAZAMA PICHA ZA NGONO MITANDAONI.
Tatizo lilianzia hapa, ambapo vijana wengi wamekuwa ni waraibu wa kuangalia picha za ngono, maarufu kama picha za X, watazamaji wengi wamekuwa wakitamani kufanya, kama vile wafanyavyo wale wanao waona kwenye video hizo, bila kufahamu kuwa zile ni picha za maigizo zisizokuwa na uhalisia kamili wa tendo, ndiyo maana wakati wa maigizo hayo anakuwepo Muongozaji(DIRECTOR), wachukua Picha(CAMERA MEN) zaidi hata ya wanne, kwahiyo hakuna uhalisia wa moja kwa moja, ila kwa kutokufahamu hilo. Ndipo vijana wakaingia kwenye huo mtego bila wao wenyewe kujua.
Lakini sio hivyo tu,,,

3-ULAJI HOLELA WA VYAKULA.
Si kweli moja kwa moja, kuikubali hoja ya kuwa vijana hawana nguvu za kiume, maana unapoikubali utajikuta unaanza kutumia hayo madawa yanayouzwa mitandaoni, ambayo wakati mwingine hayajapitishwa kwenye maabara ya mkemia mkuu wa serikali, kwaajili ya ukaguzi kuthibitishwa kama ni halali kutumiwa na binadamu, jambo kubwa ni kukubali kula vyakula kwa kuzingatia mlo kamili, tukizingatia kula vizuri nguvu zipo tu kwa uhakika, kula vizuri si kula vyakula vya gharama kubwa hapana, kula vizuri ni kuwa na mchanganyiko wa aina mbalimbali wa vyakula,matunda na unywaji mzuri wa maji, hapo tutaondokana na hii kasumba ya ati vijana hawana nguvu za kiume.
Pia ipo sababu nyingine,,,,,

Nb;Picha ni kwa msaada wa Google.

4.ULEVI ULIOPINDUKIA NA UVUTAJI WA SIGARA.
Ni kweli kabisa vitu hivi viwili, ndivyo vinavyoingiza zaidi mapato/kodi kubwa kwa serikali, lakini wenyewe watengenezaji wanasema utumiaji uliopitiliza wa bidhaa hizo ni hatari kwa Afya yako, na mojawapo wa athari hizo ni kuathiri mfumo mzima wa damu, na mapafu hivyo mtumiaji wa bidhaa hizo kupata athari nyingi, hebu jiulize kwanini ukanunue hizo zinazoitwa Dawa za kuongeza nguvu za kiume, wakati dawa unayo wewe mwenyewe Acha matumizi ya Pombe na sigara, kisha urijali wako utakuwa imara zaidi, maamuzi ni ya kwako kuacha, au kuendelea kisha madhara yaendelee kuwa makubwa zaidi, bado nitaendelea kuamini kuwa Upungufu wa nguvu za kiume hautibiki kwa madawa, ila unatibika kwa utayari wa alieathirika kuacha tabia fulani fulani zinazo athiri hali hiyo.
Je ni hivyo tu?
Nb;Picha ni kwa msaada wa Google.

5-VIJANA WENGI KUKOSA AJIRA.
Baada ya kuonekana upatikanaji wa ajira rasmi, kuwa mdogo wengi wao wakajiingiza kwenye eneo hili, baada ya kuonekana kuna fursa wengi wao wameanza kujiita madaktari, wakiuza dawa mitandaoni wakizipa jina la Dawa za miche asili kabisa, yawezekana wapo waliothibitishwa na wizara ya afya sikatai, ila mimi nazungumza na hawa watafuta fursa, ambao nina amini kwa uwepo wao kwa wingi ndiyo wamesababisha ionekane kuwa hili tatizo ni kubwa, na vijana wengi wakaingia mtegoni, wakatekwa kiakili(Mentality) kukubaliana na hayo, hii isipowekwa sawa wengi wataendelea kubugia haya madawa, wakidhani wanapona kumbe wanatengeneza tatizo lingine ndani ya miili yao, serikali kupitia wizara ya afya msikae kimya hali ni mbaya sana huku kitaani.

TANZANIA YANGU niitakayo kwa miaka 5 hadi 25 ijayo, ni ile ambayo ina amini kuwekeza kwa vijana wenye nguvu, kijana aaminiwe atengenezewe mazingira mazuri, ya kupata nafasi kwenye vyombo vya kimaamuzi vya kinchi, punguzeni wazee wekeni vijana wa kutosha, ili hao vijana wasaidie kutoa elimu kwa vijana wenzao waliojisahau kwa kuwa waraibu kwenye maeneo kadha wa kadha, ili waone kumbe inawezekana, UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME KWA KIJANA, ni sawa sawa na KIJANA ALIYEKOSA AKILI YA KUJISIMAMIA, ukiweza kujisimamia binafsi(Self control), basi ni rahisi sana kuepuka tabia zitakazokupelekea kujiingiza kwenye mazingira hatarishi kwa afya yako.
pic-mitandao.jpg
949f13c1df30a468b76afab5b994011b_XL.jpg
cigarette-and-liquor-696x397.jpg

TANZANIA NI KIJANA NA KIJANA NI TANZANIA.
 
watazamaji wengi wamekuwa wakitamani kufanya, kama vile wafanyavyo wale wanao waona kwenye video hizo, bila kufahamu kuwa zile ni picha za maigizo zisizokuwa na uhalisia kamili wa tendo, ndiyo maana wakati wa maigizo hayo anakuwepo Muongozaji(DIRECTOR), wachukua Picha(CAMERA MEN) zaidi hata ya wanne, kwahiyo hakuna uhalisia wa moja kwa moja, ila kwa kutokufahamu hilo.
Ni kama wakati wa zoezi la kulenga shabaha wanafunzi wengi walioenda JKT walidhani watapatia risasi zote kuuuuuuuuumbe mmmh. Sio kosa lao maana hata leo watu kibao tu wanaamini akipewa bunduki atampiga jambazi risasi ya kichwa. Sawasawa na video za ngono.
UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME KWA KIJANA, ni sawa sawa na KIJANA ALIYEKOSA AKILI YA KUJISIMAMIA, ukiweza kujisimamia binafsi(Self control), basi ni rahisi sana kuepuka tabia zitakazokupelekea kujiingiza kwenye mazingira hatarishi kwa afya yako.
Akili mtu wangu, yaaani kila mmoja akitambia hili tutapona. La sivyo ni kuyumbishwa tu na wajasiriamali wa hofu zetu na kutojiamini kwetu
 
Nafkiri pia aina ya Wanawake unaoweza kubahatika kukutana nao kingono..

Kuna baadhi yao aisee kama si mtu ngangari aah unanyoosha mikono mapema..

Utatwanga, ponda, gongelea, kandamiza vyote hivyo mtu anakuangalia tu jicho kavuu..🥺

Nafkiri matumizi ya madawa hasa ya Uzazi wa Mpango kwa Wanawake yanaleta shida sanaa siku hizi.. Wanaume wanajiona hamna kitu kumbe tatizo ni Mwanamke.
 
Yah nayo pia inachangia sana Kiongozi...
 
Ni kama wakati wa zoezi la kulenga shabaha wanafunzi wengi walioenda JKT walidhani watapatia risasi zote kuuuuuuuuumbe mmmh. Sio kosa lao maana hata leo watu kibao tu wanaamini akipewa bunduki atampiga jambazi risasi ya kichwa. Sawasawa na video za ngono.

Akili mtu wangu, yaaani kila mmoja akitambia hili tutapona. La sivyo ni kuyumbishwa tu na wajasiriamali wa hofu zetu na kutojiamini kwetu
Tuko pamoja sana Kiongozi wangu, hii ndiyo Tanzania tunayoitaka...
 
Nafkiri pia aina ya Wanawake unaoweza kubahatika kukutana nao kingono..

Kuna baadhi yao aisee kama si mtu ngangari aah unanyoosha mikono mapema..

Utatwanga, ponda, gongelea, kandamiza vyote hivyo mtu anakuangalia tu jicho kavuu..🥺

Nafkiri matumizi ya madawa hasa ya Uzazi wa Mpango kwa Wanawake yanaleta shida sanaa siku hizi.. Wanaume wanajiona hamna kitu kumbe tatizo ni Mwanamke.
Na huu ndo ukweli mtupu wamekubuhu kupita Kia's kwakweli skuhz wala hakuna kuangaika na uvaaji wao pia n tatizo
 
Na huu ndo ukweli mtupu wamekubuhu kupita Kia's kwakweli skuhz wala hakuna kuangaika na uvaaji wao pia n tatizo
Hali ni mbaya sana...ila kwa Tanzania tuitakayo, yapo mambo kadhaa kama nilivyoandika, yakizingatiwa tunaweza kupiga hatua zaidi
 
Back
Top Bottom