!!!!!!!

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,702
Hii story inachekesha flan hivi!Ndo maana nimekosa "heading".Unaweza kuwa umeshakutana nayo!Huyu mwizi aliia kwenye nyumba kwa lengo la kuiba,alipokua kwenye korido akielekea chumbani akasikia wanawake wawili mmoja akasema"hii dawa kiboko dada shemeji hachukui raundi,na utajihakikishia mali zote za shem akishakufa leoleo".Mwizi ikabidi achungulie akamuona mwanamke ambae alionekana ndo mke akiweka hiyo dawa kwenye chakula kilichokua kwenye sahani.Mwizi akaenda chumba kinachofuata ili akaibe.Akaingia alipotaka kubeba mlango ukaguswa ili ufunguliwe,akajificha nyuma ya friji,akaingia baba mwenye nyumba akakaa mara chakula kikaletwa na mkewe,akamwambia "jamani mume wangu nimekupikia pilau najua unapenda sana,kula tukalale mapema kwani nina ham na wewe"jamaa akanawa ili ale ile amemaliza kunawa kachukua chakula apeleke mdomoni yule mwizi akakurupuka kutoka nyuma ya friji akasema"braza ukila tu umekufa,nimemwona mkeo akiweka sumu ili ufe arithi mali,mimi nimekuja humu kuiba lakini kitendo hiki kimenifanya niwe na huruma nawe,kama unabisha mwambie ale hata kidogo"jamaa akamwangali mkewe akamwambia hebu kula,mke aligoma kabisa,jamaa akamrushia paka finyango ya nyama akala akafa baada ya dakika 2,jamaa akamwambia mwizi "chukua kinakufaa humu uende mana umeokoa maisha yangu",mwizi akachukua Tv akachapa lapa!
 
BW,irudie tena kama hujapata cha kuchukua hapo!
 
Ujumbe wake:

1. Usifanye mambo ukiwa na imani kuwa upo peke yako. Dhambi haifichiki.

2. Hauwezi kufa kabla ya siku zako kutimia.

3. Hata wezi huwa wana huruma.
 
Nimeipenda hii "mwizi akachukua tv, akachapa lapa" ila kweli huyo mwizi ana huruma kwa roho nyingine, umasikini tu ndo umemfanya awe mwizi..!
 
Ujumbe wake:

1. Usifanye mambo ukiwa na imani kuwa upo peke yako. Dhambi haifichiki.

2. Hauwezi kufa kabla ya siku zako kutimia.

3. Hata wezi huwa wana huruma.

siamini haka kamuzee kama kuna wakati kanawaza right! Leo lazma kuna hacker anatumia akaunt au wamehak kakichwa kako bhana!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom