britanicca
Platinum Member
- May 20, 2015
- 18,437
- 50,405
Usiniulize nini kitatokea.
Uliza tu mbona nyota za mwezi wa kumi na mbili zinang'aa tofauti mwaka huu.
Kuna tai aliyezoea kuruka juu ya milima,
Sasa anaota anaruka tena. Kila usiku anahesabu nyota kwa kidole kimoja.
Walisema mlima umemfunika,
Kumbe mlima ni kivuli tu. Kivuli hakiwezi kumzuia tai kuruka milele.
Tisa ni namba ambayo wazee hawaitamki kirahisi.
Tisa ni siku ambayo mto utabadilisha mwelekeo wake bila kelele.
Tisa ni siku ambayo jiwe litalijua jina lake la zamani.
Mzee wa nyumba kubwa anadhani amefunga upepo kwenye chupa,
Kumbe upepo umeshakuwa wimbo mdomoni mwa watoto.
Andika hii moyoni, usiandike kwenye karatasi:
Mwezi ukikamilisha safari yake, mlango utajikumbuka wenyewe.
Waliokuwa wakicheka watanyamaza kama usiku wa manane, Waliokuwa wakisubiri watainua mikono bila kusema neno.
Usiseme umeambiwa.
Sema tu ulisikia ndege akiimba usingizini.
09/12.
Britanicca