Hodi! Hodi! Hodi! nilibisha mara tatu pasipo na jibu. Mlango ulikuwa wazi na kimya kilitawala nilijongea ndani taratibu nikijua huenda bado wamelala. Au wamehama? nilijiuliza kimoyomoyo, nilikaribishwa na utandu wa buibui, wadudu waliojitengenezea nyumba zao sakafuni na panya waliokimbia huku na...