Katika historia ya mataifa yote yaliyojikomboa kiutawala, sauti ya wananchi ndiyo iliyovunja minyororo ya uonevu na ukandamizaji. Lakini hapa Tanzania, tunaishi katika kipindi ambapo ukimya wa wananchi umegeuka kuwa baraka kwa watawala dhalimu. Viongozi wanakiuka haki, wanatumia vibaya madaraka...