Miaka 57 Rais Samia avunja ukimya wa Urusi na Tanzania

Miaka 57 Rais Samia avunja ukimya wa Urusi na Tanzania

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
476
Reaction score
473
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanzania alifanya Ziara ya kwanza Nchini Urusi Oktoba 1969, kipindi hicho Urusi ikijulikana kama (Shirikisho la Umoja wa Kisovieti/USSR). Kipindi dunia ikiwa imegawanyika katika kambi mbili kuu za Vita Baridi. Tanzania ilikuwa imeanza kutekeleza sera za Ujamaa na Kujitegemea baada ya Azimio la Arusha la mwaka 1967. Katika mazingira hayo, ushirikiano na Moscow ulikuwa na sura ya kisiasa na kiitikadi, lakini pia ulikuwa sehemu ya jitihada za Tanzania kupata teknolojia, elimu, wataalamu na msaada wa maendeleo.

Hata hivyo, Mwalimu Nyerere hakujifunga upande mmoja pekee; aliendelea kusisitiza sera ya kutofungamana na upande wowote huku akitafuta marafiki kutoka Mashariki na Magharibi kwa maslahi ya taifa. Baada ya hapo wamepita marais wanne hadi Rais Dkt. Samia alipofanya zara ya pili mwaka huu Juni, 2026.

Ni miaka 57 baadae Rais wa Awamu ya ya sita Dr. Samia Suluhu Hassan amepata Kuvunja rekodi hiyo. Rais Samia amefika Urusi katika dunia tofauti kabisa. Hakuna mgawanyiko wa Vita Baridi uliokuwepo mwaka 1969.

Badala yake, dunia ina ushindani wa kiuchumi kati ya mataifa makubwa yanayotafuta masoko, uwekezaji, rasilimali na ushawishi wa kidiplomasia. Tanzania nayo imebadilika kutoka uchumi
wa ujamaa kwenda uchumi wa soko
unaotegemea uwekezaji wa sekta binafsi, biashara na ushirikiano wa kimataifa.

Katika mazingira haya, ziara ya Rais Dkt. Samia imejikita zaidi katika kuvutia uwekezaji, kupanua biashara, kuimarisha ushirikiano wa teknolojia, nishati, miundombinu na sekta nyingine za uzalishaji.

Tofauti na Mwalimu Nyerere ambaye
alizungumza zaidi katika lugha ya
ukombozi, kujitegemea na mshikamano wa kisiasa, Rais Dkt. Samia anazungumza katika lugha ya ushindani wa kiuchumi, ukuaji wa uwekezaji na fursa za maendeleo.

Ni miaka 57 yenye dhamira ileile ya msingi: kuitafutia Tanzania washirika wa maendeleo katika mfumo wa dunia uliopo.
IMG-20260607-WA0008.jpg
 
Back
Top Bottom