Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wanafamilia ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipozuru katika Kijiji cha Mwitongo Butiama Mkoani Mara...
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime anatoa neno kwa wazazi kuwaendea Watoto wao kwenye kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu.
Misime ameyasema hayo leo Oktoba 10, 2025 wakati akizungumza na kituo cha East Afrika redio.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime ametoa wito kwa Watanzania kuwa watulivu na kuepuka kuchochea vurugu au fujo siku ya kupiga kura, Oktoba 29. Ametoa tahadhari kwa wote wanaopanga kuvuruga amani, akisisitiza kuwa hata kama mgombea wako hajashinda, ni muhimu...
Mgombea ubunge wa jimbo la Buhigwe, Frank Ruhasha alipokuwa anazungumza na wananchi wa Kata ya Buhigwe - Bweranka, alisema:
"Hauwezi ukawa mbunge wa ccm alafu upambane na matatizo yanayoletwa na CCM, wapo wana ccm waliotaka kushughulika na wana CCM wenzao wakawekewa vikwazo.
Magufuli alipokuwa...
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Songwe, Fatuma Hussein, ameendelea na kampeni za Jimbo kwa Jimbo mkoani humo, ambapo akiwa katika Jimbo la Mbozi amewataka wananchi kuendelea kuiamini CCM kwa kuwa imeleta wagombea wenye hofu ya Mungu, wachapa kazi na wapenda...
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu tayari amepandishwa kizimbani kwenye chumba namba moja (1) cha Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam leo, Ijumaa Oktoba 10.2025 kwaajili ya kuendelea na kesi ya uhaini inayomkabili
Kesi hiyo ambayo inasikilizwa kwa mfululizo Mahakamani...
Katibu wa NEC, itikadi, uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Kenani Laban Kihongosi amesisitiza umuhimu wa amani Wilayani Busega Mkoani Simiyu pamoja na kujitenga kutumika kisiasa kwa ajenda za kuvuruga amani ya Tanzania hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu...
Mgombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (#CCM) Jimbo la Arusha mjini Paul Makonda akiwa Mkoani mara kumuombea kura mgombea wa Chama hicho nafasi ya urais Samia Suluhu Hassan amewaomba wananchi wa mkoa huo kukataa kuungana na wanaosema hawatopiga kura na wakiwaambia na wao wasiende kupiga kura...
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kasulu Mjini kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Martina Mturano, amejinadi mbele ya wananchi wakati wa ziara za kampeni zilizoongozwa na aliyekuwa Kiongozi wa Chama hicho, zilizofanyika katika eneo la Stendi Mpya, Kasulu Mjini mkoani Kigoma, Oktoba 8, 2025
Mturano...
Akizungumza katika kipindi cha Malumbano ya hoja cha ITV Oktoba 9, 2025 msemaji wa jeshi la Polisi nchini David Misime amekuwa kuwa katika kipindi cha uchaguzi na mchakato wake kunaendelea vizuri na kwa ujumla hali ya nchi iko vizuri na usalama wakutosha.
Kwa lugha Rahisi msemaji yeye haoni...
Hayo mambo kwakweli ni ya aibu, huwezi kulazimisha watu wakupende.
Mbeya hiyo leo inadaiwa wakiwa wanapokea hela ndo wakajaze mkutano. Kila mtu Elfu 10. Hizo ni hela za walipa kodi,Samia anachota analipia nyomi ili atengeneze picha ya kwamba anakubalika. Alafu wananchi ndo wanaongezewa makodi...
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema katika kipindi cha miaka mitano ijayo atahakikisha anawafikia wajasiriamali wadogo mahala walipo kwa kuwapatia mitaji midogo.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na...
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime ametoa wito kwa Watanzania wote kutokutoa nafasi kwa watu wanaohamasisha uhalifu, migogoro au vurugu. Ametoa rai ya kutumia njia bora kama maridhiano, mazungumzo na uvumilivu katika kutatua tofauti.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Arusha Mjini Poul Makonda ametuma salamu Kwa vyama vya upinzani ambavyo vimegomea uchaguzi ambapo amesema wametia mpira kwapani lakini wao Chama Cha Mapinduzi(CCM)wanaendelea na michakato ya uchaguzi Mkuu 2025
Makonda ameyasema hayo Musoma Mjini Mkoani Mara kwenye...
Aliyekuwa mgombea Ubunge kupitia Chama cha ACT Wazalendo Jackson Kangoye amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa mkutano wa kampenzi za mgombea Urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan zilizofanyika Musoma Mjini Oktoba 9, 2025.
Soma: Tarime Mjini; Mgombea wa ACT-Wazelendo, Jackson Kangoye...
Mgombea wa kiti Cha Urais Kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Kuna watu wanawasaidia wagombea wa vyama vya upinzani ili kuikomoa CCM
Dkt. Samia ameyasema hayo Musoma Mjini Mkoani Mara kwenye mwendelezo wa Mikutano yake ya Kampeni za uchaguzi Mkuu 2025...
Katika video inayosambaa mitandaoni ikionyesha kundi la wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika harakati za kushusha bendera za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika maeneo mbalimbali ya Musoma.
Kwa mujibu wa maelezo yanayosikika kwenye video hiyo, hatua hiyo inadaiwa...
Hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Chama cha ACT Wazalendo chini ya Bodi ya wadhamini pamoja na Luhaga Mpina kupinga uamuzi wa kuenguliwa na Tume Huru ya Uchaguzi kugombea kiti cha Urais,itasomwa leo saa nane Mchana Mahakama Kuu Masjala Kuu Dodoma.
Waandishi wa Habari mnakaribishwa kuhudhuria...
Msanii wa Bongo Fleva Rashid Makwiro almaarufu Chid Benz akifanya mahojiano na shirika la habari la BBC ameeleza sababu ya yeye kutojihusisha na siasa kama ilivyo sasa wasanii wengi wamejikita huko wakihudhuria na kushiriki Mikutano ya Kampeni za Vyama vya Siasa
Chid Benz amesema kwasababu...
Mgombea ubunge wa Rufiji wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mohamed Mchengerwa amewasilisha maombi ya wananchi wa jimbo hilo kwa mgombea mwenza wa urais wa chama hicho, Dk Emmanuel Nchimbi la Rufiji kuwa mkoa ili kurahisisha huduma.
Mchengerwa ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.