tcra

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (pia huitwa kwa Kiingereza: Tanzania Communications Regulatory Authority ambapo mara nyingi huitwa kwa kifupi: TCRA) ni taasisi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye majukumu ya kusimamia sekta za mawasiliano na utangazaji.

TCRA Ilianzishwa kwa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na. 12 ya mwaka 2003 kusimamia huduma za kielektroniki na posta na masafa ya mawasiliano nchini Tanzania. Mamlaka ilianza kazi tarehe 1 Novemba 2003 na inafanya shughuli za zilizokuwa Tume ya Mawasiliano Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).

Mamlaka ya TCRA ni kusimamia sekta ya posta, mawasiliano ya kielektroniki na utangazaji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni pamoja na:
  • Kuzifanya shughuli za TCRA kuwa za kisasa kwa kutumia teknolojia sahihi;kuimarisha tafiti zenye ubora katika huduma zinazodhibitiwa, uwezo na umahiri wa watumishi.
  • Kukuza ufanisi; kuaminika na kuhakikisha usalama wa miundombinu ya mawasiliano na matumizi yake.
  • Kukuza ufanisi na unafuu wa huduma za Mawasiliano na kuongeza upatikanaji wa huduma za Posta na TEHAMA katika maeneo yasiyohudumiwa ipasavyo na yale yasiyo na huduma kabisa.
  • Kulinda maslahi ya wadau na kukuza uelewa wa haki na wajibu wao.
  • Kufuatilia utendaji wa huduma zinazosimamiwa na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria na Kanuni kwa viwango vinavyostahili.
  • Kuratibu utekelezaji wa ahadi za kisekta kitaifa, kikanda na kimataifa.
  • Kufikia kiwango cha juu ya kuridhisha wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa TCRA.
  • Kuendelea kuzingatia matakwa ya kisheria na kiusimamizi.

Sera zinazoathiri utendaji kazi wa TCRA ni pamoja na:
  • Sera ya Taifa ya Mawasiliano ya mwaka 1997
  • Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003
  • Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003
  1. P

    JamiiForums Tanzania TCRA mnahamasisha jamii kuchangamkia fursa za uchumi wa kidigiti wakati mnaongoza kukandamiza raia mtandaoni!

    Wakuu, Feb 6 Mkurugenzi Mkuu TCRA Dkt. Jabir Bakari alisema dhima ya serikali ni kuhakikisha jamii inanufaika kwenye uchumi wa kidigiti, uchumi ambao shughuli zote zinategemea TEHAMA, na kwamba ili tuweze kunufaika ni lazima tutengeneza jamii yenye fursa ya kutambua fursa zinazopatikana kwenye...
  2. S

    JamiiForums Tanzania kwani TCRA hawawezi kuangalia namna ya kuzuia namba mpya kutuma ujumbe kwenye namba ambayo haijawahi kuwasiliana nayo??

    Kumekuwa na hili swala la kupokea sms mfululizo kutoka kwa namba zisizojulikana, yaani ukikaa kidogo utaona mara "iyo hela tuma kwa namba hii" mara "mzee nani nani anatibu mvuto, pete ya nini sijui" hujakaa sawa mara "jiunge na chama chetu" mara " mimi mwenye nyumba wako" na nyingine nyingi...
  3. Jaji Mfawidhi

    JamiiForums Tanzania TCRA wafungie ama wasifungie Simu Feki? Kariakoo na Makumbusho imejaa Simu za "kimarekani" na "Korea" feki!

    Wauza simu wa Kariakoo mtaa wa Aggrey , Makumbusho na Mwenge wanaongoza kwa kuuza "copy" ya simu halisi! Hawa wauzaji wanachanganya na simu original na feki kuhadaa wanunuzi ambo wengi wanatoka mikoani na kuamini ni original. Simu yeyote ukikuta ina ki-dude kama maskini tape na haipo kwenye...
  4. K

    JamiiForums Tanzania TCRA pigeni faini Mpesa na Airtel kwa kushindwa kutoa huduma kwa wateja tangua juzi. Wananchi wanashindwa kuburudika na sikukuu

    Wadau mitandao ya Airtel na Voda ina sumbua wateja sababu haiwezi kupokea pesa kutika Bank nk au kutuma pesa Matokeo yake wananchi wanakula sikukuu kwa shida. TCRA piga fain au fungueni Hawa jamaa kwa siku tatu Hadi waingeze ubora na umakini. Vitendo wanavyofanya wanmzarau Rais Samia?.Mbona...
  5. Mkalukungone Mwamba

    JamiiForums Tanzania Kamanda Muliro asisitiza Ulomi amekufa kwa ajali, asema ndugu sio TCRA

    Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro, amesisitiza kuwa kifo cha mfanyabiashara Daisle Ulomi aliyetoweka katika mazingira yenye utata Desemba 11, 2024 akiwa kazini kwake Sinza Kijiweni, kimesababishwa na ajali na si vinginevyo. “Ukiniambia simu ilisoma wao ni watu...
  6. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania TCRA: Matapeli wa "Tuma kwa Namba Hii" tumewapunguza

    Vitendo vilivyoripotiwa vya ulaghai kwenye mitandao ya simu vimepungua kwa asilimia 28 kati ya Juni na Septemba mwaka huu, kutokana na hatua kali za serikali na kampeni za kuongeza uelewa wa watumiaji. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt Jabiri Bakari, alifichua...
  7. Replica

    JamiiForums Tanzania Apigwa faini ya milioni 5 kwa kutumia laini ya simu iliyosajiliwa na jina lisilo lake

    Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Ernest Lwila (30) kulipa faini ya TSh5 milioni au kutumikia kifungo cha miezi sita gerezani, baada ya kupatikana na hatia kwa kosa la kutumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la mtu mwingine. Pia, mahakama hiyo imemuachia huru mshtakiwa huyo...
  8. 0

    JamiiForums Tanzania Ipi sababu ya TCRA kuomba maoni ya wanachi kwa ujio wa Starlink? Hii haiwezi ikawa njia ya kuikataa?

    Nimeona huko TCRA wanaomba maoni ya wanachi kwenye kupitisha kibali cha Starlink kufanya kazi Tanzania Ipi sababu ya kufanya hivi na Je, hii haiwezi ikawa njia ya kuja kuikataa Starlink na kusingizia wananchi ndio wameikataa. Hatujawahi ona TCRA ikiomba maoni ya wanachi kwa makampuni kama...
  9. M

    JamiiForums Tanzania TCRA ishirikiane na Shirika la Mawasiliano la Kenya kuwasaka matapeli hawa wa mitandaoni

    Ni wito kwa TCRA ishirikiane na Shirika la Mawasiliano la Kenya kuwasaka matapeli hawa wa mitandaoni. Huu utapeli wa mtandaoni umevuka mpaka kutoka kuwa wa Kitaifa sasa ni utapeli kimataifa. Namba za simu zifuatavyo ni baadhi ya zinazotumiwa na matapeli, +254794812691 (Alex Kairi), +254102269805...
  10. M

    JamiiForums Tanzania TCRA simamieni namba za simu zilizosajiliwa zisipate usajili mpya

    Salam kwenu. Naona sasa imekuwa kero sana kwa makampuni ya simu kuamua kuzifanyia usajili upya namba simu kwa kigezo hazijatumika kati ya miezi 3 hadi 6. Leo nimemtafuta mtu kwa namba ta tigo ambayo tulikuwa tukiwasiliana kwa muda mrefu isipokuwa siku za karibuni. Naastaajabu anapokea mtu...
  11. H

    JamiiForums Tanzania Jumbe za matangazo na taarifa za serikali zimekuwakero kwetu wateja TCRA jitafakarini

    Habarini, Kwakweli sasa imekuwa kero kwa jumbe za matangazo,promotion,taarifa,nk kutoka serikalini, makampuni, taasisi, wafanyabiashara,nk yaani kwa siku mmiliki wa simu/line anapokea zaidi ya jumbe 20. Kulingana na sheria ya mitandao huu ni usumbufu na kuingilia uhuru wa mteja kwani makampuni...
  12. Mtoa Taarifa

    JamiiForums Tanzania TCRA: Utapeli wa "Tuma kwa Namba Hii" umepungua sana nchini

    Akizungumza kupitia Power Breakfasta leo Oktoba 30, 2024, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma amesema "Kwenye utapeli kabla na baada ya zoezi la usajili wa laini za simu tofauti ipo kubwa sana. Ukiangalia ripoti ya Robo mwaka ya performance ya mawasiliano kwenye takwimu za mawasiliano...
  13. Raia Fulani

    JamiiForums Tanzania Kwa hiyo TCRA kazi yenu ni kuuza masafa tu?

    Huwa nawatazama kwenye tv mmenawiri mnapendeza kweli. Mnaongelea masafa/frequency kila leo. Kuna ishu ya hawa wapigaji wa mitandao. Wapo wengi ila leo nitaongelea hawa wa mesejo za "ile hela tuma kwenye namba hii". Ni kero kero sana. Wapo pia wale wanaopiga kujifanya wafanyakazi wa mitandao...
  14. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania Polisi yakiri changamoto za Mikopo Mtandaoni, TCRA yajiweka kando yasema "haituhusu"

    UCHUNGUZI wa Nipashe umebaini baadhi ya namba za simu zinazotumika kudhalilisha wakopaji hazina utambulisho wa Tanzania, yaani ZIP CODE +255. Katika ufuatiliaji wake, mwandishi alibaini kuwa kwa siku mtu mmoja anaweza kupigiwa simu na watu 10 tofauti wakizungumza jambo tofauti juu ya mkopo...
  15. S

    JamiiForums Tanzania TCRA, acheni kujitetea kuhusu mikopo ya mtandaoni; je, hamna uwezo wa kuagiza makampuni ya simu kutosajili lipa namba wanazotumia kupokea marejesho?

    Watanzania, tufike mahali tujiulize swali hli dogo tu: Mikopo ya mitandaoni hutolewa kwa wateja kutumiwa hela kwenye simu zao na zaidi marejesho hutumwa kwa haya makampuni kwa kutumia lipa namba za mitandao ya simu. Sasa kama mpaka wanakuwa wamesajili lipa namba kwenye menu ya mitandao ya simu...
  16. Mkalukungone Mwamba

    JamiiForums Tanzania TAMWA na TCRA waandaa Tuzo za Umahiri za Waandishi wa Habari 'Samia Kalamu Awards 2024'

    Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wameandaa tuzo za umahiri kwa waandishi wa habari Watanzania zinazojulikana kwa jina la “Samia Kalamu Awards 2024.” Zoezi la kutoa tuzo hizo linatarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu 2024...
  17. P

    JamiiForums Tanzania TCRA toeni adhabu kali kwa baadhi ya redio na TV

    Kumekuwa na wimbi kubwa sana la uanzishaji wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini jambo ambalo ni zuri sana. Ila kutokana na jinsi vyombo hivi vingi vya habari haswa redio na TV zinavyofanya kazi zake nyingi hazina tija katika jamii. Redio na TV nyingi zimekuwa ni wakala wa kuharibu jamii...
  18. P

    JamiiForums Tanzania TCRA toeni adhabu kali kwa baadhi ya redio na televisheni

    Kumekuwa na wimbi kubwa sana la uanzishaji wa vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini jambo ambalo ni zuri sana. Ila kutokana na jinsi vyombo hivi vingi vya habari haswa redio na TV zinavyofanya kazi zake nyingi hazina tija katika jamii. Redio na TV nyingi zimekuwa ni wakala wa kuharibu...
  19. Chachu Ombara

    JamiiForums Tanzania ACT Wazalendo: Kufungiwa kwa Gazeti la Mwananchi Mtandaoni ni kuminya Uhuru wa Habari

    KUFUNGIWA KWA GAZETI LA MWANANCHI MTANDAONI NI KUMINYA UHURU WA HABARI ACT Wazalendo tunapinga vikali kufungiwa kwa gazeti la Mwananchi Mtandaoni na kuitaka Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuondoa zuio hilo ili gazeti liendelee kutoa huduma ya habari kwa umma...
  20. D

    JamiiForums Tanzania TCRA Polisi wako wapi watu wanaibiwa kupitia hii mikopo mtandaoni? Jerry Silaa msaidie Rais

    Kuna wimbi kubwa sana la matapeli likitumia majina ya watu maarufu km Mohamed Dewji(MO), Tulia Ackson, Jokate Mwegelo n.k. Hawa watu ni matapeli na wana mtandao mkubwa, unakuta kwenye comments wanashukuru kuwa wamepata mikopo kumbe ulaghai ili uiingie mkenge. Namna ya kukuingiza mkenge...
Back
Top Bottom