Watu 7 wameuawa katika machafuko ambayo inaelezwa yanahusisha Wanamgambo katika eneo la Kaskazini mwa Msumbiji. Umoja wa Mataifa (UN) umesema watu 10,000 wamekimbia.
Machafuko hayo yametokea eneo la Cabo Delgado lenye gesi ambako Wanamgambo hao walianzisha uasi tangu mwaka wa 2017 na tangu...
Mabaki ya kale 13,000 ya kitamaduni yamegunduliwa kutoka katika mashimo sita kwenye eneo jipya la kazi ya ufukuaji katika eneo la mabaki ya kale la Sanxingdui nchini China.
Taasisi ya Utafiti wa Mabaki ya Kale na Akiolojia ya Mkoa wa Sichuan ilitangaza hayo katika mkutano wake na wanahabari...
Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi, yaliyosababishwa na mvua kubwa ya mwezi Aprili imefikia 461 huku watu 90 bado hawajulikani walipo miezi miwili baada ya mafuriko mabaya zaidi kuukumba mji wa Durban
Waziri Mkuu wa serikali ya jimbo la KwaZulu-Natal kusini...
Wahisani wachina wanaendelea kuwapa matumaini wanafunzi vijana wanaosoma kwenye shule ya Mcedo Beijing iliyopo kwenye eneo la makazi ya mabandaduni la Mathare mjini Nairobi.
Watoto hao wanaotoka kwenye mazingira magumu wamejiunga na shule hiyo kutokana na hisani ya wachina na sasa wanaweza...
Waziri akiwasili kwa ajili ya kuongea na wawakilishi wa Tanzania walioshiriki Zoezi la Ushirikiano Imara.
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) ameshiriki hafla ya ufungaji wa zoezi la kimedani la ‘Ushirikiano Imara’ lililofanyika Jinja Nchini Uganda...
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Dkt. Selemani Jafo amewataka Watanzania kuthamini bidhaa zinazotengenezwa nchini na wazawa ili kuwapa moyo wabunifu na kuinua uchumi wa nchi.
Ameyasema hayo Juni 10, 2022 Jijini Dodoma wakati alipomwakilisha Dkt. Philip Mpango, Makamu wa...
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara ya siku 3 nchini Oman mara baada ya kualikwa na kiongozi wa nchi hiyo.
Ziara hiyo itaanza Juni 12 mpaka Juni 15. Hii ni ziara nyingine ya Rais Samia katika kile anachokiita kuifungua nchi kiuchumi.
Idadi hii inatajwa kuongezeka kutoka zaidi ya watu milioni tatu mwaka jana huku zaidi ya watoto 900,000 walio chini ya umri wa miaka mitano wamegundulika kuwa na utapiamlo.
Inaelezwa kuwa sehemu kubwa ya mikoa ya kaskazini-mashariki, inakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana viwango vya chini...
Kwa mara ya pili baada ya wiki mbili, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitembelea ngome za jeshi kwenye mstari wa mbele - kwanza katika mkoa wa Kharkiv, na sasa katika sehemu hatari zaidi za mkoa wa Donbass na Zaporizhia. Wataalamu wa Ukraine na nje ya nchi wana hakika kwamba, licha ya...
Vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) vimeishutumu Rwanda kwa kutuma vikosi maalum kwa kujificha katika ardhi ya nchi hiyo, huku mzozo unaoendelea baina ya nchi hizo ukichochea ghasia mashariki mwa nchi hiyo.
Jeshi la DRC lilidai kuwa wanajeshi 500 waliovalia sare za...
Maeneo mengi nchini humo yamekumbwa na kukatika kwa umeme baada ya muungano wa sekta ya Nishati kugoma kupinga kurekebisha sheria inayosimamia sekta ya nishati ambayo ni pamoja na kuondoa vikwazo vya ushindani wa zabuni kwa miradi ya nishati mbadala.
Takriban wahandisi 900 kati ya 1,100 wa Bodi...
Chama tawala nchini Nigeria kimemchagua kiongozi wake wa kitaifa Bola Tinubu kuwa mgombea wake wa urais kwa uchaguzi ujao wa 2023 ambapo atashindana na kiongozi wa upinzani Atiku Abubakar kumrithi Rais Muhammadu Buhari katika Uchaguzi Mkuu wa Februari 2023
Katika kura za mchujo Tinubu (70)...
Nimeona na baadhi ya maeneo uwekaji wa vibao vya barabara na mitaa namna ambavyo imeacha maswali kwa wananchi, binafsi nimeyakuta haya Masasi hasa vijiji vya Masasi Dc.
Wakati zoezi linaanza nilifikiri pengine utaratibu mpya wa kupata majina na vibao elekezi vya mitaa na barabara lingefanyika...
Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema Tanzania ni salama na haina tishio lolote la usalama, pia Masauni amesema hakuna sababu ya Mtanzania yeyote ikiwemo viongozi wa CHADEMA waliopo nje ya nchi kutorudi Nchini ili waje kutumia fursa zilizopo za maendeleo pia kushiriki kutoa mchango wa...
Na Yohana Mangala, Dar es Salaam
Methali moja ya kiswahili inasema ‘Mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe’ ndivyo tunavyoweza kusema kwenye utendaji kazi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo anafanya kazi kubwa ya kujenga taifa na kuleta...
Suala la utoaji mimba usio salama limekuwa gumzo siku za hivi karibuni na takwimu zinaonesha vifo vitokanavyo na uzazi husababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo utoaji wa mimba usiosalama.
Takwimu zinaonesha katika kila Wanawake 100,000 kunatokea vifo 454 mpaka vifo 556 (Taarifa kutoka...
Wizara ya Mambo ya Nje nchini humo, imethibitisha kuahirishwa kwa ziara ya Waziri Sergei Lavrov nchini Serbia kwa sababu ya majirani watatu wa Serbia (Bulgaria, Macedonia na Montenegro) kuzuia ndege yake kutumia anga yao.
Serbia inadaiwa bado kuwa na mahusiano mazuri na Urusi licha ya nchi...
Mh Waziri Mkuu nashangaa sana kusikia ukilalama siku ya Mazingira duniani huko Dodoma na kutupia mpira wananchi eti wao ndio wapambane kudhibiti utililishaji wa maji ya sumu toka kwenye migodi. Hii ni ngumu sana.
Chanzo na tatizo ni January alipokuwa ofisi ya Makamu wa rais Mazingira. Hapa...
Majaji nchini Tunisia wanatarajiwa kugoma kwa muda wa wiki moja na kufanya maandamano ya kupinga hatua ya rais kuwafuta kazi wenzao 57.
Rais Kais Saied aliwafukuza kazi majaji 57 wiki hii baada ya kuwashutumu kwa ufisadi na kuwalinda magaidi, na pia mnamo mwezi Februari alivunja Baraza Kuu la...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.