mwigulu nchemba

Mwigulu Nchemba
Mwigulu Lameck Nchemba Madelu ni mwanasiasa na mwanachama wa chama cha kisiasa nchini Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mwigulu alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango tangu 31 Machi 2021, mpaka July 2023 ambapo wizara hiyo ilivunjwa na kuwa wizara mbili yaani Wizara ya Fedha inayoongozwa na Mwigulu Nchemba na Wizara ya Mipango na Uwekezaji inayosimamiwa na Waziri Kitila Mkumbo.
  1. Mafyangula

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Waziri Mkuu Mwingulu: Wachochezi wote wanalipwa pesa ili kuharibu nchi, wengine juzijuzi tu walikuwa masikini wakiomba na vocha

    “Wanawaambia chomeni nchi yenu, chomeni barabara, chomeni na hospitali. Mkishamaliza kuchoma hospitali anaugua mtoto wako, hospitali ilishachomwa moto, -yeye na watoto wake wako na hospitali palepale pua na mdomo huko ughaibuni walipo, wamejipa haki wao ndio wapenda Tanzania, mpenda Tanzania...
  2. Doctor Mama Amon

    JamiiForums Tanzania Swali kwa Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba: Kuna Tatizo Gani Serikalini Hadi Tunashindwa Kuiambia Dunia Taarifa za Vifo na Majeruhi wa Mwezi Moja Uliopita?

    Mheshimiwa Waziri Mkuu, Jana, tarehe 23 Novemba 2025, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, aliulizwa na waandishi wa habari kuhusu takwimu rasmi za matukio ya vifo na majeruhi vilivyotokea katika wiki ya uchaguzi mkuu 2025, na ambazo zimerekodiwa kwenye vituo vya serikali. Gerson Msigwa...
  3. DuaZaMama

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Waziri Mkuu: Tume ya Uchunguzi ya matukio ya Oktoba 29 ni Tume ya Watanzania

    Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema uundwaji wa tume ya kuchunguza matukio yaliyotokea siku na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 ni hatua muhimu ya kitaifa, akisisitiza kuwa tume hiyo ni ya Watanzania na imeundwa kwa masilahi ya nchi, si kwa malengo ya kisiasa. Ametoa...
  4. DuaZaMama

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Waziri Mkuu Mwigulu: Vituo vya Polisi vilivyochomwa ni mali ya Watanzania wala si Polisi

    Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema kuwa uharibifu wa miundombinu iliyotokea siku na baada ya vurugu za Oktoba 29, 2025 unapaswa kuwa funzo kwa taifa, akibainisha kwamba miundombinu hiyo si mali ya serikali bali ni matokeo ya jasho, kodi na kujinyima kwa wananchi wote...
  5. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Mwigulu: Nchi zenye machafuko sio masikini

    Waziri mkuu wa Tanzania, Mwigulu Nchemba amesema kuwa Tanzania inachonganishwa kutokana na rasilimali zake. Ameyasema hayo wakati wa mkutano wake wa kufanya tathmini ya athari ya machafuko ya wiki ya uchaguzi nchini humo. Tanzania ilishuhudia maandamano na vurugu wiki ya uchaguzi mkuu oktoba 29.
  6. Wakusoma 12

    JamiiForums Tanzania Mwigulu Nchemba kwenye hotuba zako punguza kufokafoka

    Jana nimekuona ulihutubia wananchi huko Singida badala ya kusema maneno ya maana na kuhutubia umoja, mshikamano na haki wewe ukaanza kutoa mapovu. Mara ooo mimi sina biashara, mara hoooo mama yangu Muislamu na blablaa kibao. Mwigulu Nchemba huko watanzania washatoka na huo utapeli wa kutufokea...
  7. Ojuolegbha

    JamiiForums Tanzania Dondoo yaliyojiri wakati wa Mkutano wa hadhara wa Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba

    𝗗𝗢𝗡𝗗𝗢𝗢 𝗬𝗔 𝗬𝗔𝗟𝗜𝗬𝗢𝗝𝗜𝗥𝗜 𝗪𝗔𝗞𝗔𝗧𝗜 𝗪𝗔 𝗠𝗞𝗨𝗧𝗔𝗡𝗢 𝗪𝗔 𝗛𝗔𝗗𝗛𝗔𝗥𝗔 𝗪𝗔 𝗪𝗔𝗭𝗜𝗥𝗜 𝗠𝗞𝗨𝗨 𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗪𝗜𝗚𝗨𝗟𝗨 𝗡𝗖𝗛𝗘𝗠𝗕𝗔, 𝗨𝗟𝗜𝗢𝗙𝗔𝗡𝗬𝗜𝗞𝗔 𝗞𝗔𝗧𝗜𝗞𝗔 𝗨𝗪𝗔𝗡𝗝𝗔 𝗪𝗔 𝗕𝗢𝗠𝗕𝗔𝗗𝗜𝗔, 𝗦𝗜𝗡𝗚𝗜𝗗𝗔 ▪️Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawasalimia Wana Singida na anawapongeza kwa kazi kubwa ya ujenzi wa Taifa. ▪️Mradi wa SGR ni wa kimkakati una manufaa kwa...
  8. baz kaiza

    JamiiForums Tanzania Hii ya Mwigulu Nchemba inaweza kua propaganda Mkandarasi toka 2018 Tumepigwa ionekane Serikali ipo kazini

    Hii ya Mwigulu vs Mkandarasi inaweza kua propaganda kali sana kwamba mkandarasi toka 2018 hii ni propaganda kabisa
  9. DuaZaMama

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Mwigulu Nchemba ayakana mabasi ya Esther,asema Hana hata biashara ya Noah

    Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameeleza masikitiko yake kuhusu tabia ya baadhi ya Watanzania kuvumisha uongo, ikiwa ni pamoja na kumvumishia kufanya biashara ya mabasi. Tumefikishwa pabaya sana. Watu wamejipa haki yao, wamekuwa ndugu zake na Mungu, ni ‘wakweli’, na wengine wote...
  10. The Magnifico

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Mwigulu Nchemba: Pesa za "Kununua Vijana na Kuwarundika" zilitoka kwa wasioipenda nchi yetu, Tanzania ni mali ya wananchi wote

    Waziri Mkuu Mh. Mwigulu Nchemba amehoji pesa za kuwakusanya vijana na kuwandamanisha zilitoka wapi? Na amewaasa vijana kuipenda nchi yao maana ni mali ya wote na ina utajiri wa kutosha, Tanzania si mali ya vyama vya siasa wala viongozi. Akizungumza katika ziara yake Ikungi, mkoani Singida, Dkt...
  11. DuaZaMama

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Waziri mkuu Mwigulu: Wanaotaka mchome nchi yenu hawapo hapa wapo nje

    WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwigulu Nchemba, amewasihi watanzania kulinda nchi yao kwa kudumisha amani, na kusisitiza kuwa wengi wanaochochea haya mambo hawaishi nchini wapo kwenye mataifa mengine. Ameyasema hayo leo Novemba 21,2025 alipokuwa ziarani mkoani Singida.
  12. Ojuolegbha

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Waziri mkuu Dkt. Mwigulu aagiza mkandarasi kukamatwa na kuzuiwa hati yake

    Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameelekeza Jeshi la Polisi na Uhamiaji kuhakikisha wanamkamata na kuzuia hati ya kusafiria ya mkandarasi anayejenga mradi wa Kituo cha ukaguzi cha Pamoja kilichopo Muhalala mkoani Singida. Dkt. Mwigulu amesema kuwa...
  13. President of China

    JamiiForums Tanzania Waziri Mkuu Mwigulu afika na mkewe kanisani Usharika wa Kisasa Dodoma na ulinzi mkali, afikisha salamu za Rais Samia Amani

    Waziri Mkuu Mwigulu afika na mkewe kanisani Usharika wa Kisasa Dodoma na ulinzi mkali, afikisha salamu za Rais Samia Amani https://youtu.be/wEZdUyMljiQ?si=f7KAhBCRRdLsfD70
  14. L

    JamiiForums Tanzania Hii ndio CV nzito na ya kutetemesha ya Dkt Mwigulu Nchemba Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

    Ndugu zangu Watanzania, Napenda kuwaleteeni Wasifu mzito na wa Kutetemesha Wa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Daktari Mwigulu Lameck Nchemba au waweza kumwita Mr Clean ikiwa na Maana ya mtu safi ,muadilifu asiye na makandokando wala kashifa ya aina yoyote ile. Au...
  15. tonicimmobility

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Rais Samia amtaka Mwigulu Nchemba kufuata nyayo za Majaliwa

    "Umepokea kijiti kutoka kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimwa Kassim Majaliwa ambaye amefanya kazi nzuri kufanikisha tunayotamba nayo leo, tukitamba na vituo vya shule, vituo vya afya, Mahospitali ya Rufaa ya Kanda. Kila tunachotamba nacho leo yeye alikuwa nyuma yangu kuhakikisha mambo yanakwenda...
  16. Ojuolegbha

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Mwigulu Nchemba: Rais Samia amejitambulisha kama Rais anayetaka matokeo ya haraka yanayotatua matatizo ya Watanzania

    Akiwa anazungumza leo Dodoma Tanzania Waziri Mkuu Mteule Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alisema "Rais Samia amejitambulisha kama Rais anayetaka matokeo ya haraka yanayotatua matatizo ya Watanzania"
  17. Mkalukungone Mwamba

    JamiiForums Tanzania Kwa nini polisi inapost kauli za Mwigulu? Wanaingiaje kwenye maswala ya bunge na waziri mkuu?

    Kwenye IG ya Polisi Tanzania wanaposti hotuba za waziri mkuu mteule Mwingulu Nchemba kwa misingi ipi? Mbona wanaleta mambo ya Polisiccm na siasa za uchawa. Yani tumeshindwa kuelewa Basi kama walitaka kumpost wangetengeneza post ya kumpongeza kuliko kufanya uupuzi wao kama huu. Na hii si mara...
  18. Ileje

    JamiiForums Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amezawadiwa kwa kufanikisha kuuza bandari na rasilimali za Taifa kwa Waarabu

    Kilichofanyika ni kutoa asante kwa Mwigulu Nchemba na kumpa Uwaziri Mkuu! Mwigulu anafahamika kwa kiburi cha madaraka (arrogance) na kujikomba kwa wakuu wake. Kinachofuata ni kutapanya mali na rasilimali za nchi kwa fujo bila huruma. Watanzania na hasa Watanganyika tuna kila sababu za kutowapa...
  19. M

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Baada ya Dkt. Mwigulu Nchemba kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu, bashiri Baraza la Mawaziri litakavyokuwa

    Leo Novemba 13, 2025, Dkt. Mwigulu Nchemba ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Waziri Mkuu wa JMT. Kama ilivyo ada, anapoteuliwa Waziri Mkuu ndio mwanzo wa kuunda Baraza la Mawaziri ili kumsaidia Rais. Soma > Dkt. Mwigulu Nchemba apendekezwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri...
  20. S

    JamiiForums Tanzania PostGE2025 Uteuzi wa Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu unatuma ujumbe kwa watanzania kuwa KAMA MBWAI NA IWE MBWAI

    Serikali nzima haitakiwi, Samia na Mwigulu ndiyo kabisaaa, hawatakiwi na watanzania. Maandamano ya 29.10 yalichochewa na mambo mawili: kuzuia uchaguzi na kuukataa uteuzi wa Samia kama mgombea urais wa Tanzania Katika maandamano hayo mabasi ya Ester yanayodhaniwa kuwa ni mali ya Mwigulu Nchemba...
Back
Top Bottom