Kutokana na hali ya kupanda kwa bei ya mafuta duniani, inayochangiwa na mvutano unaoendelea huko Iran, wadau wa sekta ya usafirishaji nchini wanakumbwa na changamoto kubwa za uendeshaji.
Mnamo tarehe 08 April 2026, LATRA iliitisha kikao na wadau wa usafirishaji kwa lengo la kujadili hali hiyo...
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafirishaji Ardhini (LATRA), Habibu Suluo, amesema kuwa kupanda kwa bei ya Mafuta ya sasa haiathiri nauli hivyo nauli zitaendelea kubaki vile vile.
Suluo ameongeza kuwa nauli zinaweza kupandishwa ikiwa bei ya Mafuta itapanda kwa kiwango kikubwa...
Niwaombe mamlaka ya LATRA waingilie kati maana costa za Moshi Arusha wamejipangia nauli wanavyo taka hii imekuwa ghali kuliko. Naomba Latra wafuatilie hili au wapange nauli halali kama inavyo takiwa. Shukran
Nimeona tangazo LATRA inataka kukaa na wadau ili nauli zipande heti! Hii Nchi hawa viongozi hawana huruma na wananchi au? Mafuta yashaanza kushuka huko duniani, wao wanawaza kupandisha nauli.
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) leo itaanza mchakato wa kupokea maoni ya wadau kuhusu uwezekano wa kufanya mapitio ya nauli za usafiri wa umma, baada ya kupanda kwa bei ya mafuta na wadau kulalamika kunachangia kuongezeka kwa gharama za uendeshaji kwa watoa huduma.
Taarifa ya umma...
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Habibu Suluo, ametoa rai kwa wasafirishaji nchini kutokuchukua maamuzi ya kupandisha nauli bila kufuata utaratibu uliowekwa kisheria, akisisitiza umuhimu wa utulivu huku mamlaka ikiendelea kufuatilia mwenendo wa gharama za...
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imewataka wadau wote wa sekta ya usafirishaji nchini, kutopandisha nauli kwa kigezo cha kupanda kwa bei za mafuta na badala yake wafuate utaratibu rasmi utakaowekwa na watakaopandisha hawatasita kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Akitoa kauli hiyo...
HAWA JAMANAA WANA HUDUMA MBOVU 🤮🤮🤮 ..
NIMELIPIA BUS LUXURY VIP NAULI 85,000 KUTOKA BARIADI KWENDA DAR, BUS IMEFIKA IMECHELEWA, KUINGIA NDANI KUNA JOTO AC HAWAWASHI .. VUMBI NJIANI MTU UMETOKA MZIMA UNAFIKA NA MAFUA ..
UKIULIZA KWANINI HAMUWASHI AC, UNAJIBIWA ITAWASHWA .. NA SASA TUMEFIKA...
Anonymous
Thread
best
bus
dar
dar es salaam
huduma
huduma mbovu
latra
line
mbovu
new
route
tarime
Salaam Wakuu,
Naona LATRA imeamua kula sahani moja na Madereva, Safari hii itakuwa kumbakumba nguo kuchanika.
Ipo hivi;
Kuanzia mwezi wa nne 2026, kama wewe ni Dereva na haujajisajili LATRA, Au unenunua vyeti feki, Madereva mnaonunua barua za uhakiki na hamna vyeti, madereva wanaonunua...
Tanzania bora ukamatwe na Polisi sio LATRA. Kwanza hawahongeki, hawazoeleki, hawaonei wala hawana huruma.
Hata haya mambo ya Foleni wakiachiwa kazi LATRA, mambo yatanyoka.
Afisa huyo wa LATRA akikukamata, atakusalimia kisha atakuomba kukukagua.
Mfano kwa wanaobeba abiria, atakagua...
Sasa kumekuwa na uhuni wa MABASI yote ya MIKOANI kutoza nauli kubwa bila nauli husika kwendana na viwango vya huduma.
Basi linatangazwa kama VVIP ila nje ya Bus kuwa jipya na choo ndani hamna jipya zaidi. Viti vimebanana mno wala havipo comfortable.
Juzi nimelipia ticket 2 kwaajili ya wazazi...
Route mpya ya Mbezi hadi Kidimu Mkombozi Kibaha imeanza. Hatimae Latra wameikumbuka Kibaha na kuanzisha route mpya inayotoka Mbezi Luis hadi Kidimu Mkombozi kupitia Loliondo imeshaanza. Wakazi wa Kibaha kwa sasa watapata unafuu wa usafiri kuelekea mjini, pia mji utaendelea kukua kwa kasi. Latra...
Siku za hivi karibuni inapofika majira ya Saa Tatu na Usiku niligombana na kondakta wa daladala wakati natoka Kawe kwenda Segerea, alidai nauli ni ni Sjilingi 1,000 badala ya Shilingi 800, akisema kwa sababu ni usiku. Baada ya kuvutana akasusa nauli yangu.
Hii si mara ya kwanza, imekuwa kawaida...
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesema kwa sasa nauli ya mpito kwa mabasi ya mwendokasi kwa baranara ya BRT 1 Kimara, Morocco pamoja na ile ya BRT 2 inayohusisha Mbagala hadi Kivukoni itakuwa ni shilingi elfu moja baada ya mapendekezo yaliyoletwa na DART.
Akizungumza baada ya...
Kama inavyosomeka hapo juu, jana na_scan kadi yangu pale Ubungo Maji naona 1000 imekatwa. Nauliza mhudumu inakuaje ananiambia nauli 1000.
Abiria mwingine naye ananiambia tangu usafiri umerudi ndio nauli wanayokatwa. Naambiwa hiyo haijawahi hata tangazwa.
Sasa Hawa LATRA wanafanya kazi gani...
Hqbari wakuu.
Nimenunua bajaj kutoka kwa mtu, sasa nataka kubadili jina la umiliki, kwa maana kadi isome jina langu. Mwenye anafahamu taratibu na gharama za kubadili kadi anijuze.
Pia hii bajaj haina bima nataka niikqtie bima, hivyo anaejua gharama za bima kubwa kwa upande wa bajaj anijuze pia...
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) itatoa vibali kwa daladala kwa njia ya Kimara ili kusaidia usafiri kutoka eneo hilo, awali abiria wa eneo hilo walitegemea usafiri kutoka kwenye mabasi yaendayo haraka maarufu Mwendokasi.