(Kijana)
Jioni ya leo siwezi kulala na njaa tena.Nitafanya kila namna nipate chakula. Nguvu nazo zimeanza kuniishia, sijui kama nitafanikiwa kutoka salama lakini siwezi kulala njaa na leo. Kuomba watu wameshanichoka, kazi hata za vibarua zimekuwa ngumu kupatikana nikae nife na njaa? Hapana...