Nini Jukumu la Mkemia Mkuu, TMDA na TBS katika kuhakiki ubora wa mafuta, vitambaa, keki na maji ya upako?

Douglas Majwala

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
665
1,000
Katika Huduma za Kiroho mbalimbali ndani na nje ya nchi kumekuwa na shuhuda za hadharani kabisa kuhusiana na matumizi ya bidhaa za upako kama mafuta, maji, vitambaa, bangili, keki nk. Nyingi za shuhuda hizi zimekiri nguvu iliyomo ndani ya bidhaa hizi ikiwemo nguvu ya kufisha baadhi ya maisha/uhai kama wa jamii za wanyama kama paka, panya, mbwa nk. Mzalishaji Asili (Original Producer) wa bidhaa hizi huenda anakuwa amekaguliwa na taasisi hizo lakini mkono wa pili wa kuzichakata (kuzipa nguvu ya upako) nao unastahili kukaguliwa ili kujiridhisha na nguvu hiyo ya upako inakuwa na nyongeza gani ama kisayansi au kiroho inayoweza kufisha uhai wa wanyama?

Hii nadhani kama serikali kupitia taasisi hizi za udhibiti na Huduma husika zikishirikiana zinaweza kuiweka jamii katika mazingira salama zaidi ambayo huenda yakaziongezea Huduma hizi wafuasi wengi kutokana na kwamba wafuasi hawa watakuwa na uhakika na usalama wa bidhaa hizo. Binafsi siamini kama ni lazima paka, panya, mbwa nk wafe ndiyo eti nguvu za MUNGU zidhihirike, nguvu za MUNGU zinajitosheleza hazihitaji kusaidiwa na kitu kiwacho chote na wala haziaminiwi kwa ulazima wa paka, panya, mbwa nk kufa (Imani ya Tomaso). Sasa yafuatayo yanafikikirisha sana:-

1. Mipaka ya Mkemia Mkuu, TMDA na Shirika la Viwango inaanzia wapi na kuishia wapi?

2. Kama Huduma hizi zimesajiliwa je, taasisi za Mkemia Mkuu, TMDA na Shirika la Viwango haziwezi kuzifikia na kuzipa huduma stahiki kwa mujibu wa sheria za nchi zinazoratibu viwango na usalama wa bidhaa?

3. Kwanini tuendelee kuishi katika kusitasita juu ya bidhaa hizi? Huku nyumba zingine za Ibada zikizipinga na kule nyumba zingine za Ibada zikiziunga mkono bidhaa hizo?

4. Je, kama bidhaa hizi zikiendelea kukosa ithibati ya taasisi hizo za udhibiti siyo kwamba zinawezakuwa na nguvu ama kama au zaidi ya sumu ya panya?

5. Mbona bidhaa-wakfu (za ibada) kutoka Israel unakuta zina ithibati ya viwango na usalama wake na zinasambazwa duniani kote, kwa hapa Tz inashindikana nini?

6. Kama bidhaa hizi zingepata ithibati ya taasisi hizo za udhibiti siyo kwamba Huduma hizi zingejipatia soko pana la ndani na nje ya nchi kwa kuziuza hadi nje ya Tz?

7. Kwanini ndani ya nchi moja kuwe na double-standards za bidhaa-wakfu katika Huduma zilizosajiliwa kisheria?

HEBU TUTAFAKARI HILI JAMBO KWA HEKIMA KUBWA NA KULITAZAMA KWA JICHO LA ZIADA.
 
Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
1,919
2,000
Acha kuziingiza taasisi zetu kwenye mambo ya kiroho, nenda kapime wewe kama umeona hayana quality. Mkemia mkuu na TBS wa mafuta na maji ya upako ni Yesu mwenyewe, ova
 
Douglas Majwala

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
665
1,000
Acha kuziingiza taasisi zetu kwenye mambo ya kiroho, nenda kapime wewe kama umeona hayana quality. Mkemia mkuu na TBS wa mafuta na maji ya upako ni Yesu mwenyewe, ova
Kama nchi je, hatuna sheria yoyote inayoratibu uagizaji, uingizaji na utumiaji wa kemikali hatari na salama za uzalishaji mali na utoaji huduma? Sheria hiyo kama ipo mipaka yake inaishia wapi? Argue with evidence!
 
Mtukutu wa Nyaigela

JF-Expert Member
Sep 4, 2018
3,781
2,000
Katika Huduma za Kiroho mbalimbali ndani na nje ya nchi kumekuwa na shuhuda za hadharani kabisa kuhusiana na matumizi ya bidhaa za upako kama mafuta, maji, vitambaa, bangili, keki nk. Nyingi za shuhuda hizi zimekiri nguvu iliyomo ndani ya bidhaa hizi ikiwemo nguvu ya kufisha baadhi ya
Unaongelea hizi tasisi zinasubiri maagizo kutoka juu. Fanya mambo mengine mkuu usije ukaambiwa wewe ni gaidi kuliko Osama.
 
wajingawatu

JF-Expert Member
Jan 20, 2013
1,546
2,000
Katika Huduma za Kiroho mbalimbali ndani na nje ya nchi kumekuwa na shuhuda za hadharani kabisa kuhusiana na matumizi ya bidhaa za upako kama mafuta, maji, vitambaa, bangili, keki nk. Nyingi za shuhuda hizi zimekiri nguvu iliyomo ndani ya bidhaa hizi ikiwemo nguvu ya kufisha baadhi ya maisha/uhai kama wa jamii za wanyama kama paka, panya, mbwa nk. Mzalishaji Asili (Original Producer) wa bidhaa hizi huenda anakuwa amekaguliwa na taasisi hizo lakini mkono wa pili wa kuzichakata (kuzipa nguvu ya upako) nao unastahili kukaguliwa ili kujiridhisha na nguvu hiyo ya upako inakuwa na nyongeza gani ama kisayansi au kiroho inayoweza kufisha uhai wa wanyama?

Hii nadhani kama serikali kupitia taasisi hizi za udhibiti na Huduma husika zikishirikiana zinaweza kuiweka jamii katika mazingira salama zaidi ambayo huenda yakaziongezea Huduma hizi wafuasi wengi kutokana na kwamba wafuasi hawa watakuwa na uhakika na usalama wa bidhaa hizo. Binafsi siamini kama ni lazima paka, panya, mbwa nk wafe ndiyo eti nguvu za MUNGU zidhihirike, nguvu za MUNGU zinajitosheleza hazihitaji kusaidiwa na kitu kiwacho chote na wala haziaminiwi kwa ulazima wa paka, panya, mbwa nk kufa (Imani ya Tomaso). Sasa yafuatayo yanafikikirisha sana:-

1. Mipaka ya Mkemia Mkuu, TMDA na Shirika la Viwango inaanzia wapi na kuishia wapi?

2. Kama Huduma hizi zimesajiliwa je, taasisi za Mkemia Mkuu, TMDA na Shirika la Viwango haziwezi kuzifikia na kuzipa huduma stahiki kwa mujibu wa sheria za nchi zinazoratibu viwango na usalama wa bidhaa?

3. Kwanini tuendelee kuishi katika kusitasita juu ya bidhaa hizi? Huku nyumba zingine za Ibada zikizipinga na kule nyumba zingine za Ibada zikiziunga mkono bidhaa hizo?

4. Je, kama bidhaa hizi zikiendelea kukosa ithibati ya taasisi hizo za udhibiti siyo kwamba zinawezakuwa na nguvu ama kama au zaidi ya sumu ya panya?

5. Mbona bidhaa-wakfu (za ibada) kutoka Israel unakuta zina ithibati ya viwango na usalama wake na zinasambazwa duniani kote, kwa hapa Tz inashindikana nini?

6. Kama bidhaa hizi zingepata ithibati ya taasisi hizo za udhibiti siyo kwamba Huduma hizi zingejipatia soko pana la ndani na nje ya nchi kwa kuziuza hadi nje ya Tz?

7. Kwanini ndani ya nchi moja kuwe na double-standards za bidhaa-wakfu katika Huduma zilizosajiliwa kisheria?

HEBU TUTAFAKARI HILI JAMBO KWA HEKIMA KUBWA NA KULITAZAMA KWA JICHO LA ZIADA.
Hivi unawaamini au unaiamini nembo ya tbs au Tmda? Je juice zilizopitishwa na tbs na zinauzwa sana kila mahali ni salama, kiafya?
 
Douglas Majwala

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
665
1,000
Hivi unawaamini au unaiamini nembo ya tbs au Tmda? Je juice zilizopitishwa na tbs na zinauzwa sana kila mahali ni salama, kiafya?
Hata waganga wa kienyeji wana sheria yao inayowaratibu na products zao. Wengine wasiporatibiwa unadhani usalama wa nchi utakuwaje? Mwaka 1983 taifa chini ya Mwl Nyerere ilivunja dini moja iliyoingia nchini (Tabora) ambayo mfumo wa ibada yao ni kusali wakiwa watupu. Hakuna kitu duniani ambacho serikali haiwezikidhibiti
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom