HALI YA ULINZI NA USALAMA WA MIPAKA YA NCHI
Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2023/24, haIi ya mipaka ya Nchi yetu yenye urefu wa jumIa ya kiIomita 5,923.41, ambayo inahusisha eneo Ia nchi kavu na eneo Ia maji, imeendeIea kuwa shwari. Mipaka hiyo ni baina ya Tanzania na Burundi, Jamhuri ya...