chanjo

Chanjo (kutoka kitenzi "kuchanja"; kwa Kiingereza "vaccine") ni dawa ya kibiolojia ambayo inajenga kingamwili dhidi ya ugonjwa fulani.

Dawa ya chanjo huwa na sehemu za vidubini vinavyosababisha ugonjwa fulani. Dawa hutolewa kutoka katika kidubini kilicho hai au kilichokuwa hai. Sehemu zinazotumiwa kwa dawa haziwezi kusababisha ugonjwa lakini zinatambuliwa na mmfumo wa kinga mwilini.

Mara dawa ya chanjo inaingizwa katika mwili, mfumo wa kinga unaanza kutegeneza fingomwili dhidi ya ugojwa huo.

Chanjo ni njia bora zaidi kuzuia magonjwa ya kuambukiza. Kinga inayoenea kutokana na chanjo kwa kiasi kikubwa inawezesha kuepukana na kifua kikuu duniani na kizuizi cha magonjwa kama vile polio, pepopunda, tetekuwanga kutoka duniani kote. Hata hivi karibuni kumekuwa na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 kuna chanjo zilitengenezwa na kuukabili

Tunashauriwa na wataalamu wa afya na wanasayansi wa kimataifa kuwapa watoto wadogo chanjo ili iwakinge dhidi ya magonjwa na maradhi mabaya. Kinga ni bora kuliko tiba.
  1. M

    Hoja ya Humphrey Polepole kuhusu thamani ya fedha manunuzi ya chanjo ya COVID-19 ni mfupa mgumu kwa wanasiasa wachumia tumbo

    Polepole kasema haoni thamani ya fedhha (value for money) kwenye pesa ya kununulia chanjo. Hakuna aliyejitokeza kutetea thamani ya fecha inayonunulia chanjo ya corona isiyo na uwezo wa kumlinda mtu hata kwa miezi 6 tu Hoja ya Polepole ni hii; Bei ya chanjo ni Tsh 51,000/=. Watanzania tuko...
  2. The Assassin

    70% ya wasiotaka chanjo USA wako tayari kuacha ama kufukuzwa kazi kuliko kuchanja

    Marekani imechanja zaidi ya 50% ya watu wake ambao wanastahili kuchanjwa lakini karibu watu milioni 100 wenye sifa ya kuchanja wamegoma kuchanja ama hawajachanja hadi sasa. Kutokana na covid, makampuni mengi ama taasisi nyingi zinahimiza ama kulazimisha wafanyakazi wao kuchanjwa na mengine...
  3. N

    Mashetani wanatumia hadi madhabahu ya kanisa kuzuia watu wasipate chanjo ya UVIKO-19

    SHETANI KAPANDISHA MOLI Ndugu zangu tupo kwenye ulimwengu ambao shetani anatenda kazi sawasawa, ukiona mtu anasimama kupinga chanjo na hana evidence ya upingaji wake jua sio yeye bali ni mashetani yako kichwani yanamuongoza muhimu tumuombee mashetani wanataka kuhakikisha mnakufa kwa ujinga...
  4. Lady Whistledown

    Imani Potofu na Ukweli Kuhusu Chanjo ya COVID19

    Chanjo ya COVID-19 inaweza kuathiri uzazi wa wanawake Chanjo ya COVID-19 haitaathiri uzazi. Ukweli ni kwamba chanjo ya COVID-19 inahimiza mwili kuunda nakala za protini ya spaiki inayopatikana kwenye uso wa coronavirus. Hii "inafundisha" kinga ya mwili kupambana na virusi ambavyo vina protini...
  5. K

    Chanjo: Utamaduni wa uongo wa serikali umetufikisha hapa

    Mpaka sasa vifo vya Corona hazisemwi waziwazi na mnategemea watu wataona vipi umuhimu wa chanjo kama vifo vingi vya corona, watoa taarifa wanaogopa kutangaza wazi na kuishia kusema kwa sirisiri. Haya ndiyo mambo yanayorudisha nyuma mapambano ya huu ugojwa. Huu ni ushauri tangazeni vifo vyote...
  6. Analogia Malenga

    Mrema atoa wito kwa viongozi wa dini kuhamasisha waumini kuhusu chanjo

    WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi mstaafu, Dkt. Augustino Mrema, ameyataka madhehebu na viongozi wa dini nchini kuendelea kuwaelimisha waumini wao umuhimu wa kupata chanjo ya COVID-19 na kuchukua tahadhari za ugonjwa huo kama ambavyo wataalam wa afya wanashauri. Akizungumza jana wakati wa misa...
  7. Suley2019

    Wanasayansi: Kuchanja chanjo zaidi ya moja hakuleti madhara

    Dar es Salaam. Wanasayansi wameondoa shaka kuwa kuchanja chanjo zaidi ya moja ni kujiletea madhara. Wamesema mtu mmoja akipata chanjo tofauti za kinga dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19, haiwezi kumletea madhara, badala yake huongeza ufanisi wa kinga za mwili na kushambulia virusi vya corona...
  8. N

    Angekubali Chanjo na kuchukua tahadhari mapema, mpaka leo huenda tungekuwa naye

    Tupate funzo kupitia hili, Sio kwamba unapokua mkubwa kifedha/kimadaraka ni unaona kila mtu unamzidi akili, hapana Mungu alituumba akatupa akili akatubariki akatufanya tuishi kwa kutegemeana ili kutatua mambo mbali mbali ya duniani. Mungu akawabariki wataalamu mbalimbali, watabibu...
  9. Analogia Malenga

    Prof. Mkenda: Tuiamini Serikali, tuchome chanjo

    MBUNGE wa Rombo, mkoani Kilimanjaro, Profesa Adolf Mkenda, amewaonya wananchi kuacha mara moja tabia ya kupuuza kuchoma chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 na badala yake kuiamini serikali na wataalam wa afya ili kupunguza kasi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa huo. Profesa Mkenda, aliyasema hayo jana...
  10. U

    Covid-19 hii ni vita ya kiroho zaidi kuliko ya kimwili

    Kuna kitu hapa, hii ni vita ya kiroho zaidi kuliko ya kimwili. Kuna video na picha za matukio mbalimbali tutakua tunayajadiri humu kuhusu hili swala na kuzifafanua kwa ajili ya afya ya kwenu, watoto wenu na WAJUKUU wenu. Vijana wengi hawakubaliani na maamuzi ya wazee na hawana nguvu na mali ya...
  11. beth

    Serikali: Watanzania zaidi ya 325,000 wamepata chanjo hadi sasa

    Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema waliopata Chanjo dhidi ya Ugonjwa wa COVID19 tangu zoezi hilo kuanza kote Nchini hadi sasa ni zaidi ya 325,000 Amesema, "Chanjo ni hiari, lakini Wataalamu wanatuambia usipopata Chanjo ukapata Ugonjwa, utapata madhara makubwa ndani ya mwili wako"...
  12. A

    Polisi wajeruhiwa maandamano ya kupinga chanjo ya Uviko

    COVID-19: Five police officers injured after violence breaks out at anti-vaccine protest in London Ten people were arrested after demonstrators clashed with police in Canary Wharf and South Kensington. Friday 3 September 2021 23:39, UK
  13. Red Giant

    Hoja ya Polepole na hoja ya Gwajima juu ya chanjo ya Covid-19

    Polepole: Moja, Polepole yeye anasema kuwa corona ni ugonjwa uliotengenezwa na big pharma ili yapige pesa. Kuwa mabeberu wanaachana na kuvamia nchi kuiba mafuta na sasa wanatengeneza magonjwa ili kupiga pesa. Pili, Anasema kuwa kasi ya kirusi kubadilika(ku-mutate) inatia shaka, si ya kawaida...
  14. R

    Uhamasishaji matumizi ya Chanjo dhidibya Covid 19 tupewe kazi hii nyepesi sisi Chadema. CCM na Serikali mmeshindwa. Hamna uhalali wa kuihubiri

    Huu ndio ukweli. Sasa umegeuka kuwa aibu hata kwa Mkuu wa Nchi. Haiwezekani mtu yule yule aliyepinga na kutushawishi kutumia matunguli leo anageuka na kutushauri vinginevyo. Hawezi kuaminika hata uwe Waziri, Mkuu wa Mkoa, DED au mkuu wa vyombo vyenye nguvu. Hii kazi ni nyepesi inahitaji weledi...
  15. Shadow7

    Zanzibar: Serikali tayari imeshaingiza chanjo ya Johnson & Johnson ili wananchi wapate chanjo kujikinga na maradhi ya Covid-19

    Waumini waliojitokeza kuitekeleza Ibada ya sala ya Ijumaa katika Masjid Noor, Muyuni wakimskiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alipowasalimia mara baada ya kutekeleza Ibada ya Sala ya Ijumaa. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwasalimia waumini mara baada ya...
  16. Analogia Malenga

    Muungano wa Ulaya kurudisha mamilioni ya chanjo za COVID-19 Afrika

    Muungano wa Ulaya utarudisha mamilioni ya dozi ya chanjo za Johnson & Johnson zilizotengenezwa Afrika Kusini katika bara la Afrika. Mjumbe maalum wa Muungano wa Afrika Strive Masiyiwa amewambia waandishi wa habari kwamba chanjo zote zinazotengenezwa “zitabakia Afrika na kusambazwa Afrika”...
  17. J

    Gwajima, Polepole na Silaa waitwa Kamati ya Maadili ya CCM

    Dodoma. Wabunge watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwamo Mbunge wa Kuteuliwa, Humpherey Polepole watawekwa kikaangoni leo na Kamati ya Maadili ya Wabunge wa CCM kuhojiwa kuhusu masuala tofauti. Wabunge wengine watakaohojiwa leo ni Askofu Josephat Gwajima (Kawe) na Jerry Silaa (Ukonga) ambao...
  18. M

    Kwa hali hii naamini maneno ya Askofu Gwajima kuwa viongozi wamehongwa ili chanjo ije

    Huu ni mkusanyiko wa watu ktk Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam mbele ya Rais 02/09/2021. Halafu bila soni akasisitiza chanjo. Hivi Rais Samia yuko serious na gonjwa hili ama anaongea kuwafurahisha na kuwapumbaza walotoa hela? Wenye akili wameamua kumchana mheshimiwa rais bila woga.
  19. Analogia Malenga

    Kassim Majaliwa: Wanaopinga chanjo ni wale ambao hawajaguswa na corona kwenye familia

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema wanaopinga chanjo ya #COVID19 hawajaguswa na virusi hivyo katika familia zao, wakiguswa watatafuta chanjo. Amesisitiza chanjo sio lazima lakini ni muhimu. Wataalamu waliotumika kuchunguza chanjo ni wataalamu wa ndani ambao hawawezi kutaka kuwauza watu wao...
  20. beth

    Rais Samia: Silazimishi watu kupata chanjo, kila mtu ni mkubwa ana akili yake

    Rais Samia Suluhu Hassan akiwa Zinga, Bagamoyo amesema halazimishi watu kupata Chanjo dhidi ya COVID-19 akieleza, "Kila mtu ni mkubwa ana akili yake. Vituo vipo ukijihisi unataka kwenda nenda, ukiona bado hutaki ni wewe na maamuzi yako" Amesisitiza "Tusidanganyane, COVID-19 ipo na inachukua...
Back
Top Bottom