JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 631
- 960
Je, unatumia dawa za kupunguza maumivu kabla ya chanjo ili kuepusha athari (side effects) zake?
Shirika la Afya Duniani (WHO) linaonya kuwa inaweza kupunguza ufanisi wa chanjo.
WHO inasema kuwa athari za kawaida za chanjo kama vile maumivu ya kichwa na uchovu mara nyingi hutokea kwa kiasi kidogo
“Kutumia dawa za kupunguza maumivu kama vile paracetamol kabla ya kupokea chanjo ya COVID-19 kuzuia athari (side effects) zake haifai. Hii ni kwa sababu haijulikani jinsi dawa za kutuliza maumivu zinaweza kuathiri namna chanjo inavyofanya kazi. Hata hivyo, unaweza kuchukua paracetamol au dawa zingine za kupunguza maumivu ikiwa utapata athari kama vile homa, maumivu ya kichwa au maumivu ya misuli baada ya chanjo.” Inasema WHO
Pia shirika linashauri kuwa ni vema kuwasiliana na mtoa huduma ikiwa kuna wekundu au maumivu yanayoongezeka katika eneo ulilochomwa chanjo baada ya masaa 24, au ikiwa athari hizo haziondoki baada ya siku chache.
=====
"Taking painkillers such as paracetamol before receiving the COVID-19 vaccine to prevent side effects is not recommended. This is because it is not known how painkillers may affect how well the vaccine works. However, you may take paracetamol or other painkillers if you do develop side effects such as pain, fever, headache or muscle aches after vaccination." -- World Health Organisation