Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, amesema chama hicho hakitasita kuchukua hatua dhidi ya watumishi wazembe wanaosababisha migogoro kwa wananchi.
Amesisitiza kuwa lengo la utumishi wa umma ni kutoa huduma bora kwa wananchi, si kujinufaisha...