Zaidi ya kuiangusha CCM, nini jibu la matatizo yetu?

Zaidi ya kuiangusha CCM, nini jibu la matatizo yetu?

The Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
11,099
Reaction score
13,706
Huwa nasikia watu wakilalamika na kutuhumu wakoloni kwa kutuletea matatizo. Hata hivyo, tukiwa wakweli, mengi ya matatizo yetu yamesababishwa na watawala wetu uchwara na waroho. Wakoloni waliondoka miaka zaidi ya 60 iliyopita. Ajabu, bado tunawafuata na kuomba mikopo na misaada toka kwao.

Tukipewa, tunashukuru. Ila huwa tunasahau kitu kimoja muhimu na rahisi he who pays the piper calls the tune. Kwa kimakonde kibovu amlipaye mpiga zumari huchagua wimbo. Wakitukosea tunawaita mabeberu sijui kwanini si madume au hata madudu kwa vile wote si wa kiume tu.

Kwa hiyo basi, kwa Tanganyika, chanzo cha matatizo yetu ni CCM. Kadhalika, jawabu la matatizo yetu ni kuondoa na kuandika katiba mpya itakayowalinda wananchi na si watawala. Tuwe na katiba inayowawajibisha watawala wetu ambayo haitatunyang'anya mamlaka ya kuwafukuza kama vile mwajiri amfukuzavyo muajiriwa pale anaposhindwa kukdhi matakwa ya ajira yake.

Kwa wale waliojiajiri kwenye ofisi za umma kama hawa wa sasa, hao ndiyo usiseme. Tuwapige chini na kuanza upya.

Baba yenu nawasilisha.
 
Back
Top Bottom