Kwanini unalala bado? Kwanini unalikumbatia shuka bado? Kumekwisha kucha, jua limekwisha chomoza. Amka sasa eeh mama Afrika maana majukumu yako ni mengi. Watoto wako wanalia njaa zinawauma, wanalia majirani zao wanawaonea, kwanini usiamke uwafariji wana wako...