Alliance for Change and Transparency (ACT) (Swahili: Chama cha Wazalendo, lit. 'Party of Patriots') is a political party in Tanzania. It received its permanent registration in May 2014.
Chama cha ACT Wazalendo kimezindua rasmi Operesheni MajiMaji, kampeni maalum inayolenga kuwaamsha Watanzania kulinda thamani ya kura zao kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Operesheni hiyo itafanyika nchi nzima kuanzia Julai 1 hadi Julai 15, 2025, ikiongozwa na viongozi wakuu wa chama hicho...
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, Naghenjwa Kaboyoka amejiunga na chama cha ACT Wazalendo leo Juni 28 Dar es Salaam.
Kaboyoka aliyewahi kuwa Mbunge wa Same Mashariki 2015-2020 amepokelewa leo na Kiongozi wa chama hicho Dorothy Semu kwenye ofisi za makao makuu Magomeni.
Mwaka 2020 Kaboyoka...
Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, anatarajia kuchukuwa fomu ya kukombea ubunge na atawania nafasi hiyo katika jimbo la Temeke.
Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa jana Juni 23, 2025 kwa umma na ACT Wazalendo, Sheikh Ponda atachukua fomu saa tano asubuhi...
Wakuu ACT wanaendelea na arakati za maandalizi kuelekea uchaguzi mkuu 2025 na sasa ni zamu ya Magreth Lutufyo amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya ACT kugombea Ubunge wa Jimbo la Tanganyika. Fomu hiyo amekabidhiwa na Katibu wa jimbo la Tanganyika, Ndugu Emanuel Ntinda.
Wakuu,
Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii instagram wa Chama cha ACT Wazalendo wameweka picha ya kipeperushi yenye maandishi yanayodai Janeth Ritte aweze kuachiliwa huru
Je, kwa njia hii wataweza kweli kufanikiwa kupata uhuru wa Janeth Ritte?
Makamu Mwenyekiti wa ACT - Wazalendo isihaka mchinjita anasema iwapo watashinda kiti cha Urais, jambo la kwanza hawataligeuza Eneo la Tanganyika Packers Kawe kuwa eneo la Mtume Mwamposa kuombea watu wapate kazi bali watarejesha viwanda vilivyokufa na kutengeneza vipya ili watu wengi zaidi wapate...
Hakuna chama kinachoiweza CCM isipokuwa CHADEMA leo Kafulila na Happi wanajipakulia tu minyama mbele ya CHAUMMA na ACT WAZALENDO,
https://www.youtube.com/live/UP89m78r-Uk?si=NhbWNO83GsYHj3xL
katika uchambuzi wa Bajeti Kuu ya Serikali 2025-2026 uliofanywa na ACT Wazalendo, leo wameonesha namna ambavyo bado serikali haijaweka wazi namna wanaenda kulitibu suala la kikokotoo kwa wastaafu nchini.
"Suala la kikokotoo cha Wastaafu kinaendelea kuwa kitanzi kwa watumishi wanaomaliza muda...
Akizungumza katika uchambuzi wa Bajeti Kuu ya Serikali 2025-2026 uliofanywa na ACT Wazalendo, Mwenyekiti wa chama hicho Dorothy Semu amesema,
"Kwa mwaka mwengine tena tunaenda kwenye uchaguzi tukiwa hatuna matumaini makubwa ya haki na msingi ya demokrasia kuzingatiwa. Tumeamua kuingia kwenye...
https://www.youtube.com/live/CSYHcygl-bk
UTANGULIZI
Juni 12, 2025 Serikali iliwasilisha Bungeni Bajeti yake ya mwaka 2025/2026.
Hii ni Bajeti ya Tano kusomwa tangu Rais aingie madarakani na Waziri wa Fedha Mheshimiwa Mwigulu Nchemba. Matarajio yetu ilikuwa kuwa sera za bajeti za mwaka huu...
Katibu Mkuu wa ACTwazalendo Ado Shaibuado amesema kuwa jumla ya wanachama wapya 2567 wamesajiliwa kwenye mfumo wa kusajili wanachama wa "ACT Kiganjani" tangu Mbunge Mstaafu wa Mtwara Mjini Ndugu Maftaha Nachuma awasiliane na uongozi wa Chama kwa ajili ya kutangaza kujiunga.
Ado Shaibu...
Shangwe Ayo, Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa ACT Wazalendo na Waziri Kivuli wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), ametangaza kuwa Polisi wamevamia ofisi za chama hicho na kumkamata Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake Taifa, Janeth...
Hakuna Volume ya magari ya mizigo kwenye Barabara ya Geita Mwanza, na nature ya uchumi wa Tanzania Volume zinatoka Bandarini Dar kuelekea Mikoani na kutoka Mikoani kuelelekea Dar, Sasa mkoa wa Geita una Volume ya mizigo? ya kupitiapale kwenda Dar? hakuna zaidi ya dhahabu labda tusafirishe...
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini na Makamu Mwenyekiti wa chama cha CUF, Maftaha Nachuma amekihama chama hicho na kujiunga na chama cha ACT Wazalendo
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi...
Kada wa ACT Wazalendo, Emmanuel Ntobi ameteuliwa kuwa Naibu Msemaji wa Sekta ya Habari, Mawasiliano na TEHAMA kwenye Baraza Kivuli la ACT Wazalendo. Uteuzi huo umefanywa leo Juni 17, 2025 na Kiongozi wa Chama Dorothy Semu.
TAARIFA KWA UMMA
Kiongozi wa Chama, Ndugu Dorothy Manka Semu leo Juni...
Mwanasheria na Mwanaharakati mashuhuri nchini Wakili Peter Madeleka ametuliwa kuwa Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria katika Baraza Kivuli la Mawaziri la ACT Wazalendo. Uteuzi huo umefanywa leo tarehe 17 Juni na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Dorothy Semu.
Wakili Peter Madeleka akizungumza na Wananchi Jimbo laTemeke, amesema ACT Wazalendo Wakiingia madarakani watahakikisha Polisi wanaostaafu wanaondolewa kikokotoo ikiwa ni sababu ya umasikini amesema pia Polisi wakilinda Kura kila Askari atamiliki Ghorofa na gari Land Cruiser
Wakati akijibu alipoulizwa na mtumiaji mmoja wa X kuhusu operesheni yao ya #lindakura kwamba wanaogopa nani ataiiba alijibu; "CCM na vyombo vya dola! Oktoba"
Zitto anazidi kutoa shule huko X kwa wananchi wanaohoji ni kwa vipi watafanikiwa na operereshin yao ya #lindaKura
"Kwa lugha nyepesi: tutalinda kura kwenye kituo cha kupigia kura kwa kupiga kura, kusimamia ikihesabiwa na matokeo kubandikwa.
hakuna kura bandia itaingia kituoni
hakuna wakala wa...
Sativa amewakalia kooni ACT wazalendo 😂. Kupitia ukurasa wake wa X anaandika
"Kanuni zinasema ukipiga kura NENDA nyumbani. Haisemi ukae mita 200.
Kwahiyo ACT WAZALENDO watalinda kura kutokea nyumbani.🫵🏾😂
KM ADO SHAIBU ebu toa shule kwa vijana wako. Hawakuwepo Dodoma wakati una mwaga wino...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.