abiria

Abiria (kutoka neno la Kiarabu عبر ˁabara kwa maana ya kuabiri, kuvuka eneo la maji) ni watu wanaosafiri kwa kupanda meli, ndege, gari, basi, pikipiki au treni.

Abiria hutumia vyombo hivyo vya usafiri kama njia ni mbali, au kama hawana usafiri wa binafsi au kama wanapendelea matumizi ya usafiri wa umma kuliko usafiri wao binafsi.

Kwa kawaida wakipanda wanalipia kiasi fulani kama nauli ili mwenye chombo hicho aweze kuwalipa dereva na wahudumu wengine pamoja na gharama za chombo chenyewe na matumizi yake.
  1. peno hasegawa

    JamiiForums Tanzania Ajali za mabasi ya abiria zaanza kuitikisa serikali ya Tanzania

    Kwa kipindi cha awamu ya tano , ajali za mabasi ya abiria Tanzania ilibakia Kurwa historia. Sasa kila kona ya nchi ni vifo vya wapendwa wetu na serikali imepiga kimya. IGP uko wapi?
  2. Rodwell mTZ

    JamiiForums Tanzania Ushauri: Bajaji zilizozuiwa kubeba abiria Mbezi Luisi ziruhusiwe kutokana na wingi wa abiria

    Ninayo heshima kubwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya kukuandikia barua hii fupi. Kwanza kabisa hongera sana kwa kazi nzuri ya kuijenga taifa. Lengo la barua hii ni kuhusu marufuku uliyoitoa dhidi ya bajaji zinazobeba abiria kutoka kituo cha Mbezi Luisi zikiwapeleka...
  3. H

    JamiiForums Tanzania Dereva wa treni ya abiria hupataje taarifa kama kuna dharura au hatari ili aweze kusimama

    Kwenye usafiri wowote kunaweza kutokea hatari au dharura yeyote..Nakumbuka nikiwa Kwenye safari fulani ya gari moshi ilitokea sintofahamu ndani ya mabehewa abiria wakawa wanataka kwenda kutoka nje huku treni iko kwenye mwendokasi lakini bahati nzuri treni ikasimama katikati ya pori na hiyo...
  4. mshale21

    JamiiForums Tanzania ATCL waanzisha kibubu kwa abiria wanaotaka kulipia nauli kidogo kidogo, Wahamasishaji kupewa zawadi

    Dar es Salaam Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imeanzisha mpango wa "kibubu" utakaowawezesha wananchi kulipia kidogo kidogo mpaka atakapo kamilisha malipo ya tiketi yake ya ndege. Katika mpango huo, mwananchi atatakiwa kuweka Sh50,000 kwa mara ya kwanza na kiasi kinachobakia atatakiwa kulipa...
  5. HARRISON ONE

    JamiiForums Tanzania Wananchi na wasafiri wa Mbeya na ushabiki wa mwendokasi wa mabasi ya abiria

    Kuna tabia ya ushabiki wa mwendokasi wa mabasi hasa yaendayo Mbeya ambayo naona siku hadi siku inazidi kukua. Sasa sijui ni ushamba au nini. Kufukuzana huko mtakuja kufa kwa kwa ujinga. Mikoa mingi sasa ina kampuni kubwa za mabasi ya abiria lakini hawana ujinga huo kama wanaofanya mabasi ya...
  6. Bujibuji Simba Nyamaume

    JamiiForums Tanzania Ligi isiyo rasmi, inayoshabikiwa na trafiki na abiria Sauli vs Golden Deer

    Miaka nenda rudi Njia ya Dar es Salaam - Mbeya ndio imekuwa njia ambayo ni gumzo kwa mabasi yake kwenda mbio. Umbali wa safari ni zaidi ya kilometre 800, na njia imekuwa ikipita kwenye Milima mikali, kona kali, mbuga ya wanyama, hali ngumu ya hewa Ikiwa ni Pamela na uwepo wa ukungu mzito na...
  7. kingkongtz

    JamiiForums Tanzania Waendesha bodaboda mnakera kulazimisha watu kupanda pikipiki zenu

    Kwema ndugu zangu, Bodaboda wana tabia za ajabu sana sijui kwanini. Unaweza ukawa unatembea unashangaa wanakupigia honi. Au upo njiani unatembea unashangaa boda huyu hapa "oya braza wapi" sasa nabaki najiuliza ina maana mimi sijui napokwenda au? Leo nimeshuka kwenye gari akaja boda na...
  8. KITAULO

    JamiiForums Tanzania Treni yapata ajali Morogoro ikiwa na abiria 1370 ‘Dereva amefariki, kuna Majeruhi’

    Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema Treli ya Abiria imepata ajali saa tatu asubuhi July 22, 2021 baada ya Lori kuigonga Treni hiyo katika eneo la Kambi moa Godegode, Morogoro na kupelekea majeruhi 21 ambapo Wanaume ni 13 na Wanawake 8 na kifo cha Dereva wa Lori ambaye jina lake ni Gerald...
  9. Faana

    JamiiForums Tanzania Suala la Kushusha abiria wote Mbezi Litazamwe upya

    Nawasilisha maoni haya kwa Mamlaka husika, leo asubuhi nimeshuka Magufuli terminal kwa bus na kushushwa kama watawala walivyoamuru, tukiwa wengi tu, tukavuka kwenda upande wa pili kutafuta daladala za kwenda mjini, kiukweli, nimejifunza ule usemi wa "mwenye shibe hamtambui mwenye njaa" una maana...
  10. GENTAMYCINE

    JamiiForums Tanzania Kwanini ukipanda Basi la Mikoani linaloendeshwa Kasi (Spidi) sana utayaona yafuatayo kutoka kwa abiria waliolipanda?

    1. Jina la Baba Mungu hutajwa mno? 2. Sura (Nyuso) za Huruma hutawala mno? 3. Waliochwa Majumbani hukumbukwa mno? 4. Kuombana Magazeti kunapungua mno? 5. Maombi ya Kuomba Kukojoa (Kuchimba Dawa) hupungua mno? 6. Abiria wengi hujifanya wamelala (tena kwa Kufumba Macho) ila Breki ya Basi...
  11. EINSTEIN112

    JamiiForums Tanzania Waubani Linyama, dereva wa basi ambaye picha yake ina-trend mtandaoni kwa sasa

    Huyu jamaa ndio mwamba wa GOLDEN DEER [emoji1662][emoji1662][emoji1662] T 712 DPK anayezisumbua SCANIA za SAULI [emoji1631][emoji1631] za DAR - MBEYA - TUNDUMA Ametrend sana wiki hii akiwa na memes mbali mbali
  12. L

    JamiiForums Tanzania Reli ya Kisasa ya SGR yaleta mabadiliko katika sekta ya uchukuzi wa shehena na abiria nchini Kenya

    Ikiwa ni zaidi ya miaka minne sasa tangu reli ya kisasa ya Mombasa-Nairobi nchini Kenya kuanza kutumika, sekta ya uchukuzi wa shehena na abiria imepata mabadiliko makubwa na kusaidia ukuaji wa uchumi na ajira. Kufikia sasa, zaidi ya abiria milioni tano wamefaidika na uchukuzi wa bei nafuu...
  13. Erythrocyte

    JamiiForums Tanzania Napinga hoja ya RC Makalla ya kulazimisha Mabasi yote ya Mikoani kupakia na kushusha abiria Stendi ya Magufuli pekee

    Amos Makalla ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mfadhili wa zamani wa bendi ya FM ACADEMIA ya Kinondoni, bila kufanya utafiti wowote ule leo ametoa amri ya kulazimisha mabasi yote ya mikoani kuanzia safari zao kwenye kituo kikuu cha mabasi ya mikoani cha Mbezi Luis, kinachoitwa kituo cha...
  14. Trubarg

    JamiiForums Tanzania Nchi hii watembea kwa miguu na abiria hatuna haki kabisa

    Nchi hii wanaothaminika ni wamachinga pekee watembea kwa miguu na abiria hawana haki kabisa na inawezekana wamefutwa kabisa kwenye kamusi ya wanyonge. Haiwezekani vituo vyote vya daladala na sehemu za watembea kwa miguu kuwa ndiyo sehemu ya kusimika biashara za hao wanaoitwa wanyonge. Siku...
  15. Shujaa Mwendazake

    JamiiForums Tanzania Ajali Morogoro: Gari liliwekewa Mashada ya Maua na abiria waliomboleza ili kukwepa Doria ya Polisi

    Basi linadaiwa kusababisha ajali jana mkoani Morogoro lilibeba mashada ya maua, dereva aliposimamishwa kwa mwendo kasi alidai Wanawahi Msibani Taarifa za kuaminika kutoka kwa abiria ni kuwa gari hilo halikubeba maiti na abiria wote waligeuka waombolezaji kila gari liliposimamishwa. Na taarifa...
  16. cpb

    JamiiForums Tanzania Natafuta njia nzuri ya kusafirishia abiria

    Ndugu zangu niko na gari aina ya Raumu nataka nitumie walau nijipatie riziki naomba mwenye kujua sehemu ambayo ina njia nzuri alafu kuna changamoto ya usafiri anielekeze humu nikafanye hapo kazi. Gari yangu ina uwezo wa kubeba abiria kuanzia 5 Hadi nane hivi hata kama ni rough road walau pawe...
  17. Kurzweil

    JamiiForums Tanzania Mamlaka za Usafiri Dar hazijali muda wa abiria

    Habari wanaJF, Hoja hii ni mahsusi kwa watumiaji wa usafiri wa Daladala wanaotumia Mabasi ya Mbezi - Kawe na Mbezi Makumbusho pia wale wa Makumbusho - Mbezi na Kawe - Mbezi. Angalieni huu mzunguko; Unatoka Mbezi/Kimara unasimama Taa za Ubungo, ukivuka unasimama tena taa za TCRA kisha unakunja...
  18. Sam Gidori

    JamiiForums Tanzania Pakistan: Zaidi ya watu 30 wafariki baada ya treni mbili za abiria kugongana

    Treni mbili za abiria zimegongana nchini Pakistan mapema siku ya Jumatatu na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 30, huku wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa. Treni moja, Millat Express ilitoka nje ya reli kabla ya kugongwa na treni nyingine, Sir Sayed Express. Haijafahamika mara moja...
  19. Kiume3000

    JamiiForums Tanzania Kwanini madereva wa mabasi ya mikoa wanasimamisha gari za abiria hotel za bei mbaya?

    Serikali yetu hembu tusaidieni sisi wanyonge na hii tabia ya madereva inazidi shamiri sna kwa wale ndugu zetu wanao safiri mikoa ya mbali #Dar_to_mwnza, #Dar_to_mbya, #Dar_to_kgma, #Dar_to_Arusha kuna tabia na utaratibu wa mabasi walio jiwekea bila kuhofia abiria wao na sio rafiki kabisa...
  20. Ben Zen Tarot

    JamiiForums Tanzania Mfahamu abiria aliyesafiri peke yake katika ndege ya kuwabeba abiria 360

    Ndege kutoka Mumbai hadi Dubai ilipaa na kuanza safari ikiwa na abiria mmoja pekee. Mtu aliyesafiri peke yake katika ndege ya kuwabeba abiria 360. Wanaotokewa na tukio kama hili, huchukuliwa kuwa 'bahati nzuri'. Mahali: Uwanja wa ndege wa Mumbai Saa: Kumi kamili Abiria: Bhavesh Zaveri...
Back
Top Bottom