Mfahamu abiria aliyesafiri peke yake katika ndege ya kuwabeba abiria 360

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,905
6,689
Ndege kutoka Mumbai hadi Dubai ilipaa na kuanza safari ikiwa na abiria mmoja pekee. Mtu aliyesafiri peke yake katika ndege ya kuwabeba abiria 360.

Wanaotokewa na tukio kama hili, huchukuliwa kuwa 'bahati nzuri'.

Mahali: Uwanja wa ndege wa Mumbai

Saa: Kumi kamili

Abiria: Bhavesh Zaveri

Bhavesh, ambaye ni mkazi wa Dubai, alitembelea mji wa Mumbai wiki ya kwanza ya Mei kibiashara. Alikuwa ameshakata tiketi yake ya kurejea siku 10 kabla.

Na kama kawaida yake, huwa anasafiri katika sehemu ya tabaka la wafanyabiashara.

Lakini kwasababu ya corona, ni wazi kwamba ndege hiyo haingekuwa na watu wengi na akaamua kukata tiketi katika sehemu ya watu wa kawaida.

Mei 19 safari yake ilikuwa ni saa kumi na nusu asubuhi. Aliwasili uwanja wa ndege usiku wa manane kulingana na sheria za kimataifa. Wakati anafanyiwa ukaguzi kuingia ndani ndipo alipofahamu kuwa abiria ni yeye peke yake.

Kwa muda, hakukubaliana na hilo lakini baada ya muda akajua kuwa huo ndio ukweli wa mambo ulivyo.

Wamekuwa Dubai kwa kipindi cha miaka 20 na amekuwa akisafiri kutoka Mumbai - Dubai mara nyingi tu lakini hii ndio mara ya kwanza amekutana na tukio la namna hii, kusafiri peke yake.

Akizungumza na BBC huko Dubai, amesema: "Sio kawaida yangu kujirekodi video, lakini safari hii nimejipiga picha na kujirekodi karibu safari yote kwa kutumia simu yangu ya mkononi.

"Nataka safari hii iwe katika kumbukumbu zangu milele. Ilikuwa tajriba ya kipekee katika ndege yoyote ile ya Emirates. Yaani haijawahi kutokea abiria anasafiri peke yake katika ndege yote. Baada tu ya kupanda ndege, wahudumu wote wa ndege walinipokea kwa kunipigia makofi. Rubani alitoka kwenye chumba chake cha kuendesha ndege na kuja kunisalimia. Akanitania."

Gharama
Ndege ya shirika la Emirates ndio ambayo Bhavesh alikuwa anasafiri nayo kutoka Mumbai hadi Dubai, iliyokuwa inabeba watu 360 aina ya Boeing 777.

Sasa pengine unajiuliza, ndege iligharamika kiasi gani?

Mtaalamu wa ndege Rajesh Handa amesema, "Safari ya ndege kutoka Mumbai hadi Dubai inachukua saa moja na nusu. Safari hiyo ingekuwa imegharimu tani 25 za mafuta na gharama yake ni ya juu.

Na bila shaka gharama yake ilikuwa ya juu hasa kwa usafiri wa mtu mmoja.

Ni swali ambalo pia Bhavesh aliwauliza wahudumu wa ndege.

Lakini Bhavesh alikuwa na haya ya kusema:

"Nilifikiria uwanja wa ndege hautakuwa na watu wengi. Abiria kutoka India sasa hivi wamepigwa marufuku UAE kwasababu ya janga la virusi vya Corona. Wanaoruhusiwa ni wenye Viza maalum, wanasiasa na raia wa UAE kusafiri kutoka India hadi Dubai.

Makundi hayo matatu pekee ya abiria ndio wanaoweza kusafiri kuingia Dubai kwa ndege za kibiashara. Ndege ilikuwa imetua Mumbai. Na ingerejea bila abiria. Nilikuwa nimekata tiketi kabla kwahiyo niliruhusiwa kusafiri kwa ndege hii."

Bhavesh ni mfanyabiashara wa madini ya almasi ikiwa ni taaluma yake.
Ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya StarJames Group.
Anaishi Dubai na mke wake na watoto wao wawili.

Video aliyokuwa amepiga inamuonesha akisafiri peke yake katika ndege ya abiria 360 ilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii huko Mumbai na Dubai.

Anaelezea safari yote kama ya kupendeza. Kulingana na yeye, fursa kama hiyo inakuja kwa bahati. Pesa haiwezi kununua furaha.

"Ndege niliyokuwa nasafiria ilikuwa inatoka asubuhi sana kwahiyo, siku ile sikulala vizuri. Sikutaka kulala nikiwa safarini lakini ilifika wakati sikujua kulitokea nini, nikaibwa na usingizi. Nilipofika nyumbani, nilieleza familia yangu tajriba niliyopita "

6.jpg
 
"Ndege niliyokuwa nasafiria ilikuwa inatoka asubuhi sana kwahiyo, siku ile sikulala vizuri. Sikutaka kulala nikiwa safarini lakini ilifika wakati sikujua kulitokea nini, nikaibwa na usingizi. Nilipofika nyumbani, nilieleza familia yangu tajriba niliyopita "View attachment 1800097
Me pia nina bahati sana juzi nilipanda difenda peke yangu huku nimezingirwa na maaskari wenye silaha nzito!
 
Yan hapo shirika linajikuta nauli aliyolipa huyo jamaa haitoshi kuwalipa ata flight attendants wawili
 
Huku bongo land daladala tu ikiwa na abiria wachache inafaulisha ndo iwe ndege kwa abiria mmoja ? Duuuuuh kwa kweli biashara ni ngumu pande hizi za hii Melanin
 
Ebu tusaidie ku convert hizo an 25 za mafuta ni sawa na lita ngapi.
Uwezo wa ndege kuruka na kutua unategemea sana uzito. Mafuta ni sehemu ya huo uzito. Ili hesabu iwe rahisi wanaamua kujaza mafuta kwa uzito. Mfano ton 25(hizo ni Lita 31,200) kwahio rubani anapiga hesabu zake kwa kuzingatia uzito. Pia anajua ndege yake inachoma ton ngapi za mafuta kwa saa.
 
Nafikiri hapo kwenye umbali kwa masaa ni matatu na kidogo
Tani 25 za mafuta duuh!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Hiyo habari km ilivyoletwa nimeisoma jana BBC km ilivyo
Hvyo mleta mada kaleta km ilivyo
waulizeni BBC
 
Back
Top Bottom