Adha kubwa tuipatayo abiria tunaosafiri na mabasi ya mikoani

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Serikali yetu hebu tusaidie wanyonge na hii tabia inazidi shamiri sna kwa wale ndg zetu wanao safiri mikoa ya mbali #Dar_to_mwnza, #Dar_to_mbya, #Dar_to_kgma, #Dar_to_Arusha kuna tabia na utaratibu wa mabasi walio jiwekea bila kuhofia abiria wao na sio rafiki kabisa wanapaki mabasi yao sehemu ya chakula bei zao ziko juu bila kujali abiria wao mifukoni mwao kuko vipi.

Chakula cha kawaida sana unakuta elfu 7 elfu 8 na kuendelea wakati hicho chakula hakina hadhi ya kuuzwa bei hiyo halafu kidogo sana. Hivi wanadhani kila mtu anapesa ya kumudu hiyo pesa?

Jana nilikuwa natoka Arusha kuja Dar tulipo fika sehemu ya chakula nilitamani kulia niliongozana na mom mmoja mwenye watoto wa 3 alivyoambiwa chakula cha bei ya mwisho ni elfu 7 alikuwa mnyonge sana na alikuwa na elfu 5 tu ikambidi anunue soda na biscuit roho iliniuma sana. Sasa ombi langu, serikali itoe sheria kwa mabasi yote yawe yanasimama kwenye mji ulio na huduma kwa wote sio kutupeleka maeneo ambayo wana masilahi nayo. Inaumiza sana.

Tusambaze hii kwa ma group mengi tusikike tusiwe wajinga kwa tetesi nilizo sikia dereva akipeleka basi sehemu ya hotel hupata huduma ya chakula bure yeye na watumishi wote wa gari na posho wanapewa kwa week au mwezi sasa iweje maslahi yao yatutese abiria?

Tupaze sauti kwa viongozi #Wabunge na viongozi wote wa juu kuwa hii ni 2021 inakera sana
 
Dah.. Sijui nikwambie nini Mkuu, wazo lako zuri ila halitekelezeki, wenye hela nao wakisema "bus zinasimama kula sehemu local sana tunataka sehemu zenye chakula kisafi kisichodhuru tumbo" ITAKUAJE?

Then next time weka paragraph.
 
Kabisa mkuu. Hoja yako ina mashiko sana. Hawa wamiliki wa hizi sehemu za chakula wanaibia pakubwa sana abiria. Vichips vya 5,000 huwezi hata kushiba. Mshikaki wa 5,000 hata haufanani na hiyo bei. Bei zao zimekaa kuwaumiza abiria. Wanafanya hivyo wakijua lazima ule tu kwa sababu huna sehemu nyingine ya kwenda kula. Serikali tafadhali wasaidieni hawa wanyonge.
 
Zamani tulipokua tunasafiri na OTC toka Dar kwenda Nairobi tukiwa wadogo, bi mkubwa alikua akitengeneza chapati za kutosha na nyama ya kuku, mkate na chai ya rangi kwenye chupa ya chai.

Kipindi tukifika Korogwe sisi tunaenda kukojoa Mara moja na kurudi ndani ya Basi na kula mikuku na chapati.

Sasa wamama wa siku hizi muda mwingi wako bize na kujirembua badala ya kuingia jikoni na kutengeneza hata ndizi za kuchoma au chapati.

Bure kabisa.
 
Hivi mleta mada lengo lako huwa ni kusafiri au kula njiani hotelini? Naona kula umekuvalia njuga kama ndio lengo lako kuu la kusafiri. Kwenu huwa huli au?
 
Wanafanya hvo Kwa sababu uwekezaji wanaofanya ni mkubwa Sana mkuu, na wateja ni hao hao wa kwenye mabasi, hakuna mteja mwingine, na mda wa menu ni ule ule Kati ya sa sita na sa Tisa, ukipita huo mda msosi unalala na lazima ulipe wafanyakazi. Kodi na expenses zingine. Ushauri andaa tu menu yako fresh home utaenjoy sana.
 
Mbona bei ya kawaida sana, kuliko kwenda kula vyakula sehem za ajabu alafu uje uendeshe mfululizo na kuumwa na tumbo kwa kuogopa kutoa 7000. Na kama unaona ghali safiri na chakula chako kutoka nyumbani utaepuka gharama.
 
Pia mda wa kuchimba dawa pamoja na kununua msosi huwa hautoshi. Kwa mfano, dakika 10 tu. Lakini ukienda sehemu ya kuchimbia dawa unakutana na foleni la kufa mtu, na wakati huo huo mama ana watoto ambao anatakiwa awasimamie kuchimba dawa kisha ndiyo akafanye manunuzi ya misosi.

Ndiyo maana kuna bahadhi ya abiria huwa wanaachwa (baada ya zile dk 10 kuisha) na basi na wakati huo huo dereva akijulishwa kwamba kuna abiria kaachwa, wao huwa hawajali na kuzidi kuchochoea mafuta.

Hili lilitokea ktk basi la abood (Mwanza-Dar) na Chumas (Tabora-Mwanza).
 
Wanafanya hvo Kwa sababu uwekezaji wanaofanya ni mkubwa Sana mkuu, na wateja ni hao hao wa kwenye mabasi , hakuna mteja mwingine, na mda wa menu ni ule ule Kati ya sa sita na sa Tisa, ukipita huo mda msosi unalala na lazima ulipe wafanyakaz, kodi na expenses zingine. Ushauri andaa tu menu yako fresh home utaenjoy Sana.
Hao wawekezaji wakubwa si watafunga sasa hotel zao kwa kukosa wateja?
 
Zamani tulipokua tunasafiri na OTC toka Dar kwenda Nairobi tukiwa wadogo, bi mkubwa alikua akitengeneza chapati za kutosha na nyama ya kuku, mkate na chai ya rangi kwenye chupa ya chai.
Kipindi tukifika Korogwe sisi tunaenda kukojoa Mara moja na kurudi ndani ya Basi na kula mikuku na chapati.
Sasa wamama wa siku hizi muda mwingi wako bize na kujirembua badala ya kuingia jikoni na kutengeneza hata ndizi za kuchoma au chapati. Bure kabisa
Sisi tulikuwa tunabeba ile mikate ya ngano ya mviringo inapikwa kwa kienyeji, au wali kwenye sado, Arusha to Mbeya au Mbeya to Arusha enzi hizo 1996,1997,1998,1999
 
Andaa chakula chako nyumbani funga kwenye foil safiri nacho, kuna abiria wengine pia kwa hadhi yao hawawezi kula hizo sehemu unazozitaka wewe

Unakula mshikaki wa mia tano unaharisha wiki nzima na kujitibu kwa elfu ishirini.
 
Back
Top Bottom