Abiria (kutoka neno la Kiarabu عبر ˁabara kwa maana ya kuabiri, kuvuka eneo la maji) ni watu wanaosafiri kwa kupanda meli, ndege, gari, basi, pikipiki au treni.
Abiria hutumia vyombo hivyo vya usafiri kama njia ni mbali, au kama hawana usafiri wa binafsi au kama wanapendelea matumizi ya usafiri wa umma kuliko usafiri wao binafsi.
Kwa kawaida wakipanda wanalipia kiasi fulani kama nauli ili mwenye chombo hicho aweze kuwalipa dereva na wahudumu wengine pamoja na gharama za chombo chenyewe na matumizi yake.
Wezi kila siku wanabuni mbinu pya ili kutimiza nia zao ovu, huyo kwenye video alijidai mfanyakazi wa basi la Abood na kudai tiketi kisha iliyokuwa kwenye simu akajifanya anaenda kukagua akaondoka na simu
Kuna uzi flan ulianzishwa na mdau flan akiponda biashara ya kumkabidhi mtu bajaji ya abiria akuletee 20000/day kwamba ni biaashara kichaa na ya kijinga sababu kubwa ikiambatanishwa na bei ya bajaj kuwa ghari kulinganisha na kinachoingia,sasa hapa pia nilitaka kufahamu,vipi kuhusu GUTA (pikipiki...
Wakazi wa Kigamboni kwa muda mrefu tumekuwa tukitumia Vivuko vipya ambavyo ni vya Azam maarufu kama SeaTax kazi yao ni nzuri, lakini kuna hii Kampuni N-CARD ambayo imekuwa ikihudumia upande wa hizi card zinazotumika kukata ticket ili uweze kuvuka.
Kinachonishangaza kwa kipindi cha digital...
Kuna magari kadhaa makubwa ya mizigo inadaiwa ni kutoka Rwanda yamepata ajali eneo la Mto Kikafu katika Barabara ya Moshi - Arusha na kufunga njia kwa zaidi ya Saa 10 sasa, kukiwa hakuna mpishano wa magari.
Hali hiyo imesababisha mabasi yasimame kwenye foleni kwa urefu wa zaidi ya Kilometa 20...
Habari za majukumu.
Kumekuwa na utaratibu wa abiria wanaokata ticketi online katika kampuni ya GEITA EXPRESS kutozwa gharama za ziada mbali na nauli ilivyoandikwa kwenye mfumo wa ukataji tiketi.
Kwanini hakuna usawa wa gharama za kupata tiketi kwa abiria wanaokata ticketi online na wale...
Anonymous
Thread
abiria
company
express
geita
kampuni
kero
kubwa
kutoza
mabasi
nauli
online
tiketi
Tanzania ni sehemu pekee ambapo biashara inaweza kufa kutokana na uwepo wa wateja wengi. Kama hali ilivyo kwenye mabasi ya mwendokasi, ndicho kinachoonekana hapa SGR.
SGR inahujumiwa waje wapewe wakezaji - na safari hii watapewa Warusi si wachina wallahi!
LEO JIONI Treni hii limeharibika RUVU PORINI huko. Abiria wameambiwa Washuke Waanze kutembea na kwamba kuna Treni inakuja kuwachukua. Wataanza na abiria wa VIP—abiria wametembea zaidi ya KILOMITA 6 hakuna...
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema limepata changamoto kwenye mfumo wa umeme karibu na Stesheni ya Ruvu mkoani Pwani, hali iliyosababishwa na mvua inayoendelea kunyesha nchini.
Akizungumza na Swahili Times, Afisa Habari wa TRC, Fred Mwanjala amesema kwa sasa mafundi wako eneo la tukio...
Ni asubuhi leo desemba 9, 2025 katika maeneo ya Tegeta Kibao jijini Dar es salaam, Askari Polisi wakifanya ukaguzi wa kila gari yakiwemo mabasi yanayotokea Kaskazini (Arusha, Moshi na Tanga).
Adha ya usafiri kutoka jiji la Dar Es Salaam kwenda Mikoa mingine nchini bado imekuwa kitendawili ambacho kila Mwisho wa mwaka hasa mwezi wa 12 kinakosa kutenguliwa. Inaelezwa kuwa kwa mwezi wa 12 kwa mwaka huu 2025 Ongezeko la abiria limekuwa mara dufu na mapema sana(kuanzia Disemba 01, 2025)...
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limewakamata madereva watano wa magari ya kubebea wagonjwa kwa tuhuma za kubeba abiria kinyume cha sheria.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, SACP Alex Mkama, amesema madereva hao waliokuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Kagera wamekamatwa kufuatia...
Baada ya siku 21 tangu kusitishwa kwa huduma ya mabasi yaendayo haraka katika barabara ya Mbagala kuelekea Gerezani na Kivukoni kufuatia uharibifu uliotokea wakati wa maandamano ya Oktoba 29, huduma hiyo imeanza rasmi kurejea leo kwa kubeba abiria.
Katika baadhi ya vituo vya Kilwa Road, mabasi...
Wakuu,
Serikali za kiafrika zina changamoto sana, kwamba bila kushinikizwa na vitisho haziwezi kujisimamia?
Au ni kwa sababu ya uchaguzi, kwamba ukipita wakishapata "ridhaa ya wananchi" tutarudi kukekule?
Hii inaweza kuwa danganya toto, watu wasihadaike maana hawa ccm wanajulikana kwa kuhadaa...
Hii siyo kwamba mtoto anaringishiwa nyonyo wakuu? Jana Ajira elfu 41, leo Mwendokasi Mbagala inaanza kubeba abiria kuna vimatukio flani hivi kama vya kupoza moto.
===
Ni rasmi mabasi yaendayo haraka (BRT) awamu ya pili barabara ya Mbagala (Kilwa), yameanza majaribio leo, Msemaji wa Serikali...
Kutokana na hizi changamoto ambazo zinazidi kuwa kubwa za usafirishaji wa abiria kwa njia ya mwendokasi, nimewaza ni kwa nini wenye mabasi ya coaster ya private (yale yasiyo na rangi maalumu za ruti), yasichukue hizi fursa za kusafirisha abiria hawa?
Maana yangu ni kwamba, chukulia wewe una...
Abiria ambao walikuwa kwenye usafiri wa daladala Eicher T 798 EDZ walijikuta katika taharuki baada ya gari hilo ambayo walikuwa wanasafiria kutoka Masaki kwenda Gongolamboto kuwaka moto kwa chini.
Moto huyo uligundulika na Wananchi ambao wapo nje ya gari hiyo na kusaidia gari hiyo kusimama na...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.