Abiria wafurika Mbezi - Magufuri, sababu ni ipi

Abiria wafurika Mbezi - Magufuri, sababu ni ipi

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
433
Adha ya usafiri kutoka jiji la Dar Es Salaam kwenda Mikoa mingine nchini bado imekuwa kitendawili ambacho kila Mwisho wa mwaka hasa mwezi wa 12 kinakosa kutenguliwa. Inaelezwa kuwa kwa mwezi wa 12 kwa mwaka huu 2025 Ongezeko la abiria limekuwa mara dufu na mapema sana(kuanzia Disemba 01, 2025) jambo ambalo limekuwa na majibu tofauti tofauti kutokana na mitazamo tofauti tofauti.



Wapo wanaodhani ni kwa sababu ya kile kinachoelezwa kuwa vuguvugu la maandamano Disemba 09, 2025 na hofu ya kutaka kwenda mikoani, wengine ni kutokana na shule kufungwa, lakini pia watu kuhitaji kwenda likizo za mwezi wa 12 vijijini na mikoa yao waliyozaliwa.

Katika maelezo ya abiria tuliowahoji na kurekodi na hata ambao hawakurekodiwa wametueleza sababu tofauti tofauti huku kilio cha kupandishwa kwa nauli kikisikika kwa wasafiri wanaoenda mkoa wa Morogoro wakidai nauli kupandishwa kutoka 13,000/= hadi 20,000/= Moja ya wasafiri anaeenda msibani Morogoro Bi. Aisha amesema "toka saa moja niko hapa ukiuliza magari wanakuambia Morogoro 25,000/=, Morogoro na hapa nauli 25,000/=?"

Mzee Mboya ametueleza kuwa abiria wengi wanawaambia wanasafiri kutokana na baadhi ya kampuni za usafirishaji kuarifu kuwa hazitasafirisha kuanzia tarehe saba mpaka tarehe kumi mwezi wa kumi na mbili.

Baadhi ya abiria wamelalamikia kukutana na kadhia ya kupewa tiketi feki na kutapeliwa na baadhi ya watu wasio waaminifu, hii ni kutokana na uhitaji mkubwa uliopo huku wengine wakilazimika kukubaliana hata pale watapoambiwa nauli ya juu tofauti na kawaida ili waweze kusafiri tu.

Jambo TV imezungumza na Bi Rukia Abdi Kibwana kutoka LATRA ambae ni Afsa Mfawidhi kituo cha mabasi Mbezi Magufuli ambapo amesema mamlaka hiyo imeshatoa vibali vya muda mfupi kwa wasafirishaji ili kubeba abiria hasa kupeleka mikoa ya Morogoro,Tanga ambayo ina uhitaji mkubwa.
 
Shule na vyuo vimefungwa,
Mbona ni kawaida kipindi hiki Miaka yote!
 
Waendelee kukaa hapo D9 iwakute hapo, watasahau walikua wanaenda wapi.

Ma basi na stendi itawaka.
 
Back
Top Bottom