Uwalimu sio sawa na ubunge, uwalimu ndio dira ya taifa, matokeo ya kuingiza watu kwenye kazi ya ualimu eti kwasababu combinations zimegoma sio sahihi. Tunapata walimu wasio na moyo wala uwezo wa kufundisha. Kufundisha ni kipaji vikichanganyika na uweledi.
Kurudisha heshima ya mwalimu ni pamoja na kupata walimu wenye division III na kwenda juu.
Mwl lazima awe role model ya kila kitu, kama mwalimu alikuwa kilaza darasani enzi zake unafikiri atapata ujasiri na mbinu gani za kumfanya mwanafunzi apende kusoma? hata hivi vyuo vya ualimu lazima...
Namuunga mkono bw. Kavulata kwa hili, walimu wetu wanatakiwa waende wakajiendeleze wafikie angalau diploma na 1st degree ili hadhi yao ipande kwenye jamii ambayo siku hizi ina mavyuo vikuu kibao. Masisha ya mwalimu wa 250,000 yanakuwa magumu kwakuwa amekopa sana kwenye vyombo vya fedha...
Utasema ni takwimu uchwara lakini uwe mwangalifu kabla hujaziita jina hilo: Asilimia 93 ya watoto wa walimu wa shule za msingi wanasoma kwenye shule za serikali, 74% ya watoto wa walimu wa shule za sekondari wanasoma shule za serikali, asilimia 58 wa watoto wa walimu wa vyuo vya certificates and...
Nimakosa kutaka kuweka kitasa kipya kwenye mlango ulioliwa na mchwa (mbovu), kaa kitako, tafakari na amua kuchonga mlango mpya ili viendane na kitasa kipya unachotaka kuweka. Mlango umeoza kila kona kwanini unahangaika kutaka kuwekewa kitasa kipya? kitawekwa wapi?. Hata kama utagoma huwezi...
Kumeibuka biashara jijini DSM ya kila kona ya jiji kuwashwa moto na kukaanga chips mitaani. Wauza chips na mishikaki hawa hawafahamiki nani kawawapa kibali bila ya kufahamu kama afya zao na mazingira ya biashara vinakidhi haja ya kuwauzia wenzao vyakula. Biashara hii inawatia wananchi kwenye...
Kuwaacha baba na mama yako nchini waliokusomesha kwa kuchoma vitumbua bila mhudumu wakiumwa na kwenda kupasua majipu ya wanyaRwanda ni kutafuta laana la maisha. Job satisfaction haitokani na mshahara mkubwa peke yake bali pia na physical and socio-psychological balanced environment. Nchi za...
Siku ni kitu cha kawaida kuzikuta siri nyeti za serikali mikononi mwa wasiokuwa serikalini. Zipo school of thought mbalimbali za namna ziri hizo zinavyofika mikononi mwa wasiohusika lakini nimeiamini ile falsafa ya "like desolve like". Inasemekana vyama vyetu vya siasa vya upinzani vimejikita...
Ajali ya meli ya Zanzibar iliyofyeka watu wetu wengi huenda ingezuiwa kama tungekuwa na kituo mahili cha hali ya hewa nchini. Maana siku ya ajali hata mtu asiyemtaalam wa hali ya hewa angeweza kujua kuwa kuna upepo mkali baharini
Kama mwanamichezo na mpenzi wa Yanga naahidi kwa moyo wangu wote kwamba sintakujasikiliza kipindi cha spoti cha Radio One. Sababu: Nilipoteza muda wangu mwingi kusubiri kipindi cha michezo cha radio one cha tarehe 16.07.2012 ili kusikia matokeo ya uchaguzi wa Yanga uliofanyika jana. Mshangao...
Baada ya migomo ya madaktari kutokea mara kwa mara nchini niliona ni vema niangalie mtaala unaotumika kufundishia wataalamu hawa muhimu. Niliangalia mitaala ya MUHAS, KCMC, na HKMU kwa uchache. Nilichokigundua ni kwamba mitaala yao inakosa masomo ya Leadership and management na entrepreneurship...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.