Sitasikiliza tena RADIO ONE kipindi cha sports saa 1.30 usiku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitasikiliza tena RADIO ONE kipindi cha sports saa 1.30 usiku

Discussion in 'Sports' started by yusufummaka, Jul 16, 2012.

 1. y

  yusufummaka Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama mwanamichezo na mpenzi wa Yanga naahidi kwa moyo wangu wote kwamba sintakujasikiliza kipindi cha spoti cha Radio One. Sababu: Nilipoteza muda wangu mwingi kusubiri kipindi cha michezo cha radio one cha tarehe 16.07.2012 ili kusikia matokeo ya uchaguzi wa Yanga uliofanyika jana. Mshangao: Maulidi Kitenge na mwenzie hawakutangaza nafasi ya Mwenyekiti alishinda nani, badala yake walitoa matokeo ya nafasi ya makamu mwenyekiti na wajumbe wengine. Hakiya mungu njaa itatuumiza, kumbe vyombo hivi vya habari haviko huru namna hii? Kitenge ni mtangazaji anayeheshimika na anayependwa na wanamichezo wengi, lakini leo nimempuuza kupita maelezo na anajipalia makaa ya moto kwenye taaluma yake. Yanga ni club ya watu wengi, ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo kuliko Manji na Mengi, hawa wanapita tu. Hivi kitenge una akili timamu? Hivi ulitegemea John Jambele angeweza kumshinda Manji katika uchaguzi ule? Manji size yake ni Mh. R. Mengi sio Jambele we vipi!!!. Kitendo cha kutowafahamisha wasikilizaji wako nani kashinda nafasi ya mwenyekiti kiliwafanya watu wasonye na kupoteza imani na kipindi chako na hatimae na Radio one.

  Siku nyingine nakuomba umshawishi Mengi achukue fomu agombee sio kumtumia mtu size ya Jambale, hiyo ingekuwa hadithi ya Daudi na Gorieth wa bibilia. Yanga Oyeee!!!!
   
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Lazima redio ifungwe hadi wewe umeisusia.
   
 3. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  hata mimi wameniboa kishenzi.
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Madhara anayoleta manji kuwa mwenyekiti wa yanga ni makubwa...
   
 5. m

  matambo JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  mtawalaumu bure watangazaji wakati hawana makosa na kama ni makosa basi anayo bwana wenu yusufu manji, yeye ndiye alikataa kwa kuweka pingamizi mahakamani kwa baadhi ya vyombo vya habari visiandike masuala yake, na kwa taarifa yako sio vyombo vya IPP MEDIA tu ila hata gazeti la Mwananchi na lenyewe huwa haliandiki jina lake bali huwa wanaandika mfanyabiashara maarufu wa Dar es Salaam maana na wao walikatazwa kumuandika, kama unabisha fuatilia Mwananchi na Mwanaspoti kesho uone kama wataandika jina la Yusufu Manji
  BTW, radio siku hizi ni nyingi sana kwani lazima usikie habari za bwana wako kupitia Radio One tuu?
   
 6. Nawaza

  Nawaza Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 3
  AOf course ni issue ya kishamba, mi pamoja ni Simba lakini sioni
  mantiki yaani ni kheri wasingetangaza, lakini kuanza kutangaza nafasi
  ya M/Mkiti ni dhahiri ni vita binafsi.

  Lakini binafsi simlaumu Kitenge coz anakidhi matakwa ya bosi wake,
  mashaka yangu ni heshima ya Mengi, natia mashaka heshima yake kupotea
  siku za usoni kwa vitu vidogo kama hv.
  Kumchukia Manji haimaanishi kuwanyima haki wana Yanga kupata habari,
  ningemuelewa kama angesema hawatangazi kabisa kuliko hvyo wanavyofanya hata mtt mdogo anajua.
   
 7. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  manji alivishitaki vyombo vya habari vya ipp..labda hawatakiwi kumtaja, radio one wanakuwaga na visilani vya kijinga sana nakumbuka kuna kipindi walisusa kutagaza habari za simba..
   
 8. d

  deecharity JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  sasa rafiki angu mwenzio pale anatetea ugali wa wake zake wawili akijifanya mjuaji vmwana vtalishwa na manji?
   
 9. E

  Entare3 Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yusuph umekuwa driven na emotions....ukasahau kufuatilia sababu zilizomfanya Kitenge asimtaje Manji.
  Kwa kuwa umeshajibiwa basi tuliza mzuka,Manji haandikwi na chombo chochote cha IPP Media na itaendelea kuwa hivyo hadi mahakama ielekeze vinginevyo.
  Lkn hata wasingetangaza matokeo tulikuwa tumeshayajua.
  Jiandaeni kuona jinsi Yanga inavyokufa maana Manji sio mtu wa kuiongoza club yenu kabisa.
  Naona giza mbele
   
 10. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Mimi nimeangalia 5 sport ya eatv nikamuona Patrick Nyambera akitangaza habari ya makamu mwenyekiti bila kutaja nafasi ya mwenyekiti ila sikujua sababu. Kumbe ni mambo ya MANJI VS MENGI!
   
 11. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nadhan sasa umesoma comments umeelewa co unakurupuka tu.kitenge ni mwajiliwa pale na wala si mmiliki wa kampun ya ipp,so siku zote mwajiliwa huwa ana tii matakwa ya mwajili wake.
   
 12. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  radio sio km JF kwamba kila kitu unataja tu bila hata mipaka.
   
 13. Blood Hurricane

  Blood Hurricane JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 1,151
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Radio One imejaa Uyanga mtupu. Maulid Baraka na Omary Katanga. Mtu kama Maulid wake wawili wa nini sasa!!! Ndio maana anakuwa na akili za kushikiliwa.
   
 14. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Shinikizo la tajiri aka Mengi.
   
 15. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kama ni kweli kuna tatizo ...tena kubwa hapo...sidhani kama kumlaumu Kitenge ni sahihi...hili lipo juu yake...sikutegemea kama Mengi anawezza kuact kitoto hivi...inasaidia nini sasa??
   
 16. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #16
  Jul 17, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  ww subiri arifu.....waganga njaa mamaae wamefurahi but ww subiri....tz baaado sana
   
 17. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  imebidi nicheke tu
   
 18. M

  MLETAHOJA Member

  #18
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ulitaka apoteze kibarua kwa ajili yako? Au wewe unaweza kuacha kwenda kazini kwa sababu ya kusherehekea birthday ya mkeo umpendaye halafu usifutwe kazi? Kuweni wakweli. Na kama matokeo uliyajua ulitaka uyasikie tena ya nini? Nakupongeza Kitenge kwa kufuata maelekezo ya bosi wako.
   
 19. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,886
  Trophy Points: 280
  Wewe ni mshabiki wa timu gani?


  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 20. samstevie

  samstevie JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama upande wa pili Clauds wamejaa simba tupu, Ibrahim Masoud ''maestro", shafii dauda, Jeff Lea na Ndimbo.
   
Loading...