Mtaala wa Madaktari una upungufu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtaala wa Madaktari una upungufu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by yusufummaka, Jul 14, 2012.

 1. y

  yusufummaka Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya migomo ya madaktari kutokea mara kwa mara nchini niliona ni vema niangalie mtaala unaotumika kufundishia wataalamu hawa muhimu. Niliangalia mitaala ya MUHAS, KCMC, na HKMU kwa uchache. Nilichokigundua ni kwamba mitaala yao inakosa masomo ya Leadership and management na entrepreneurship.

  Madaktari wanakosa negotiation skills, critical thinking skills, decesion making skills, conflict management/resolution skills, planing and managing change, delegation, and budgeting and priotization skills. Mbinu za namna zinamuwezesha mwenye nazo kushinda mitego mingi ya kikazi na hata nyumbani.

  Kukosekana kwa taaluma ya basic leadership and management katika mitaala yao kunawaondolea sifa ya kuwa wasemaji wakuu wa wizara ya Afya kwakuwa hawajui zile A-B-Cs za uongozi. Somo la entrepreneurship ni muhimu kwa madaktari ili liwawezeshe kufikiria nje ya box katika kutatua kero mbalimbali za kimaisha.

  Ni jambo la kawaida kuwasikia madaktari kila wakati wakiongea mambo ya wagonjwa wodini, theather, clinics. Yaani kila wakikutana wao ni mambo ya meconium, nimekunywa amniotic fluid, bench deaths, hii inawafanya wawe kama watumwa kwenye zahanati na hospitali za wafanya biashara, hawana muda wa kupunzika wala kuwaza mambo mengine ama kujiajiri wenyewe ndani ya nchi yao, badala yake wanawaza kwenda ng'ambo wakatumikishwe na wazungu kwa manyanyaso makubwa ya kibaguzi.

  Pengo la ukosefu wa taaluma ya uongozi kwenye mtaala lilikuwa linapunguzwa na somo la siasa mashuleni na vyuoni na mafunzo ya JKT ya mwaka mzima. Baada ya mafunzo hayo kutoweka vijana wetu wakiwemo madakatari wakawa nyoronyoro katika vitu vingi.

  Mfano, badala ya kuacha wagonjwa wajifie wenyewe madakatari wangeanza kwa kuchagua strong negotiation team ya watu wenye heshima ndani ya profession na jamii kama waziri wao wa afya, Tughe, Dr. Kebwe, Prof. Pallanjo, prof. D. Mwakyusa, Dr. Yongolo, Kapesa, Sarungi, Kahamba, n.k ili muwatangulize mbele katika safari ya kumuona Mh. Rais kumweleza kero zenu badala ya kuwatanguliza mbele watu junior na wasiofahamika kama akina Dr. Ulimboka.

  Katika vuguvugu hili la vyama vingi ni vigumu kwa mtawala kutofautisha kati ya kero halisi na siasa za upinzani. Kama hata Waziri wako hutaki kuongea naye nani atakushika mkono kwenda kwa Rais?

  Ndiyo maana sisi wananchi (potential patients) hatuungi mkono mgomo huu ingawa malengo ya mgomo wenu mnasema ni kututetea sisi tupate mazingira bora ya kuhudumiwa. Mnatakiwa mtushawishi sisi na watu wa taaluma nyingine kwamba kuna tatizo linalohitaji nguvu ya umma kulitatua. Mfano, kama mngetuambia tuchange nauli ili tutume mtu Uswisi akadai vijisenti vyetu vilivyofichwa huko ili tuje tununue CT scan, hakika tungeunga mkono wengi.

  Ama tuuze majumba ya vigogo waliyoyapata kwa njia za kifisadi ili tukanunue vitanda, wote tungeunga mkono. Ama wote tuungani tuwan'goe madarakani watu wanaotuibia wote tungeunga mkono. Lakini mnapotuambia kuwa nyinyi madakatari mnataka kima cha chini chenu kiwe mil 3,5, how about cleaners, pharmasists, nurses, lab tech, walimu, n.k inamaana mngepewa hela hiyo basi msingegoma kamwe. Acheni utoto...........
   
 2. r

  raymg JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 845
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapo kwenye red .....ama kweli jambo usilorijua n ucku wa giza! una maana gan unaposema dactari c critical thinker, na hana good decision making? kwa taarifa yako tu bila kuwa na sifa hizo basi hutaweza kutibu kabsa kwenye nchi kama TZ ambayo haina hata vifaamhimu vya kufanyia kazi.

  Dactari 1:30000 patients, kila cku unatoka job saa 12 hadi cku ya sikukukuu utapataje mda wa kufanya hicho unachokiita ujaclimari, hata kama n kufuga kuku huwez! hii n tofautna kaz zngine ambao wanatoka saa tisa na nusu.

  Hao unaowataja kua na busara....wamekuwepo tangia madai haya yaanze miaka ya 60s...ww unawaita wenye busara kuna hata mmoja umeckia akitetea haya? Huyo Dr. Kebwe amekua naibu mganga mkuu BMC, RMO, na sasa n mbunge wa serengeti anajua vzuri matatizo yaliyopo but nashangaa jana kwenye kipimajoto anaongea sera za vtabuni ambavyo havipo kwenye uharisia kazni.

  Uctumie neno sisi.....wenzako wameelewa nashangaa bado wewe ambaye naamin utakuwa kiasi furan umesoma kuliko bibi yangu unaongea vitu vya kipuuzi namna hii fualitilia Doctor's strike ya israel, ureno ambayao wananchi waelewa wamelimaliza hili mapema.
  kweli BOTHA hakukosea.....BLACKS CANT THINK BEYOND THERE NOSE, & CANT PLAN BEYOND ONE YEAR......
   
 3. K

  Kiyoya JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,280
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  No one will notice what you do untill you don't do it-tunashukuru kwa ushauri Dr!
   
 4. K

  Kiyoya JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,280
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  Sawa kabisa
   
 5. K

  Kiyoya JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,280
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 160
  No one will notice what you do untill you don't do it-tunashukuru kwa ushauri Dr!
   
 6. mawazo mbishi

  mawazo mbishi Member

  #6
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 3
  Ni mtazamo mzuri, ila sifahamu kama uliangalia course content za commuinty health course katika hiyo mitaala.

  Prof Yongolo alikuwa mmoja wa wajumbe waliokuwa kwenye majadiliano, na pia ni miongoni mwa madaktari waliokwenda kumuona Rais ikulu.

  Napenda kukukumbusha kuwa mshahara wa Dr mwaka 2005 ulikuwa Sh 157,000 na ukitoa makato ya kodi na mengine alikuwa anabakiwa na Sh 110,000, baada ya mgomo wa mwaka elfu 2005 mshahara uliongezwa na kuwa 403,000, ila ujue mishahara ya watumishi wote wa sekta ya afya iliangaliwa upya kwa hiyo mishahara ya watumishi wengine wa sekta afya pia iliongezwa ili iwiane na hiyo ya kada ya tabibu.

  Nadhani tuna matatizo ya msingi kwenye sekta ya afya, mfano mdogo tu, famasi ya muhimbili haina dawa, kwa hiyo wagonjwa wanaopata huduma muhimbili wanalazimika kwenda kununua dawa kwnye maduka ya dawa ya nje. Ukiwa mgonjwa unayetumia bima ya afya utaandikiwa dawa na kujaza fomu yako ya bima, ukienda famasi wanakuambia hakuna dawa wanakupa fomu ambazo unazirudisha kwa daktari azijaze, kisha unatakiwa uende kwenye maduka ya dawa ya nje, sasa utakuta umendikiwa dawa 4 ukienda kwenye famasi ya nje unakuta wanazo 3, na huwezi kupata hizo 3 bila kuacha hizo fomu na ukichukua hizo tatu hautakuwa na fomu tena kwenda kuchukua hiyo dawa nyingine.


  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ina mashine nne za dialysis, na kuna wagonjwa wanne tu wanaopata dialysis pale, hospitali ya rufaa mbeya ina mashine 2 za dialysis ambazo ni za zamani. na hazitumiki sasa hivi. Regency wana mashine nyingi za dialysis kuliko hospitali zote za serikali Tz, na wanapata hela nyingi kutoka mfuko wa bima ya afya ya taifa, ambayo inalipa karibu Sh 200,000 kwa kila session ya dialysis na mgonjwa nahitaji sessions tatu za dialysis kwa wiki.

  Embu jiulizehivi serikali yetu haina uwezo wa kununua hizo machine na kuziweka kwenye hospitali za rufaa, ili kupunguza adha kwa wananchi na pia kupata pesa zinazotokana na michango yetu. Hata hizo machine za dialysis tulipewa msaada kutoka Norway na marehemu Prof Bjarne Iversen, ni machine ambazo zilikuwa zimetumika kwa muda na hospitali yao ilikuwa inanunua machine mpya na za kisasa zaidi ndiyo akatupatia hizo machine na alitupatia machine saba, lakini ni 4 tu ndiyo zinafanya kazi kwa sasa.

  Kwa taarifa tu macine mpya ya dialysis ni dola 11,000 mpaka 15,000, unadhani nchi hii haina uwezo wa kununua hizi machine na kuziweka mpaka hospitali za mikoa?!

  Leo ukienda muhimbili unahitaji CT scan huwezi kufanya, na bei yake ni sh 50,000, lakini utalazimika kwenda Agha Khan ambapo bei yake ni Sh 350,000, na hata Bugando machine ya CT scan imeharibika, kwa hiyo wagonjwa wote wanalazimika kuja Dar na kufuata hizo huduma kwenye hospitali binafsi.

  Umesikia hata X ray kwenye hospitali za mikoa hazifanyi kazi, tulipewa taarifa kwenye vyombo vya habari, hspitali ya Bombo haina Xray, sasa wanawatibu vipi wagonjwa bila kuwa na vifaa vya uchunguzi.

  Nadhani kuna matatizo makubwa kwenye mfumo wetu wa sekta ya afya, kimsingi hata hao unaosema ni juniour sidhani kama ni junior maana Dr Ulimboka aligraduate mwaka 2004, na classmates wake ndio madaktari bingwa wanaotoa huduma katika hospitali zetu. Nadhani kama mitaala yetu ina shida basi walioathirika na hiyo mitaala ni madaktari wanaofanya kazi wizara ya afya kama CMO na wakurugenzi wa huduma ambao hawajaishawishi serikali iboreshe huduma za afya. Hata Prof Mwakyusa alikuwa waziri lakini bado mazingira ya kufanya kazi si bora.
   
 7. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Huhitaji elimu ya uongozi au elimu ya ujasilia mali kutambua kwamba huduma za afya zinabakwa na mafisadi huku wakiwatumia watu wapuuzi kama wewe kuwatetea!

  Viongozi dharimu ambao daima kwa utupu wa akili zao na udhoofu wa kufikiri, daima hudhani kuongeza idadi ya majengo bila ubora wa huduma za afya ni utatuzi wa matatizo ya sekta ya afya katika nchi yetu.

  Mambo yanapokuja wekwa wazi na wanaofaham hali halisi, basi watawala dharimu huwatuma wasomi uchwara kuja kuwatetea kwa kutumia nadharia zilizoshindwa kabla ya kuanza kama hizi za kwako. Pole sana msomi unayetumikishwa bila hata kujua unatetea ushetani unaoguguna hata waliokuzaa!
   
 8. a

  albinomzee Member

  #8
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 13, 2012
  Messages: 35
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Hakuna wa kuja kukuconvice kama unavyotaka,ila fanya yafuatayo panda bodaboda onayoendeshwa bila kuzingatia sheria za usalama barabarani pata ajali mbaya ya kichwani na uombee kulazwa moi.ukifanikiwa kupona mzima au na ulemavu wa maisha nahisi sio tu utawaunga mkono utaandika kotabu pia juu ya madai yao.umenisoma nyang'au wewe????
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Jul 14, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  ....................Nothing!!

  Jambo hali halikuanza siku moja kwa kukurupuka kama unavyotaka ieleweke. Limeanza siku nyingi sana na kabla ya kufikia hapa wamekutana na serikali mara nyingi na kushafanya majadiliano mengi sana, ambapo serikali iliendelea kuwawekea ngumu. Ilifikia mpaka wakataka waziri wa afya na katibu wake mkuu watimuliwe pale wizarani.

  Hao unawaita watu wenye heshima kwa nini hawajawahi kushughulikia swala hili wakati wakiwa na madaraka, au hata kuweka neno la kuwasapoti mbele ya umma tu kama ambavyo dr. Kigwangala alivyowahi kufanya bungeni wakati fulani.
   
 10. s

  suezan Member

  #10
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  mimi naomba nikuulize swali la kwanza hivi kweli wewe ni mtanzania au raia wa wapi? huu mgomo hdi umeanza doctors walikua wamesha toa mapendekezo yao na kuyawasilisha serikalini bada ya serikali kupuuzia ndo mgomo ulipo anza. sasa ulitaka watumie njia gani zaidi ya hiyo labda wewe utujulishe hapa ndugu yangu. ny the way hadi kuwakataa waziri wa afya na hao uliowaona wewe ndio wenye busara ni baada ya kuona hawawasaidfii chochote, sasa huyo wazitri akikupeleka kwa raisi ndio atabadilisha chochote wakati ameshindwa kukusaidia awali??, by the way wewe kana Dr. Ulimboka ulikua haumfahamu sasa madaktari wana mfahamu saana na kumuheshimu kuliko unavyo dhani.
  afu kuhusu hayo masomo yako uliosema sijakuelewa hata kidogo, viongozi wote wenye umri mkubwa wamepitia hilo jeshi unalosema wewe sasa nini kikubwa na cha aajabu walichofanya???
  kabla ya kumtukana mtu na kusema criticitical thinking jiulize wewe kwanza is that crittical thinking?? umeniudhi na kunidissapoint sana na nina wasiwasi na wewe
   
 11. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  out of all this amorphous article, could you please elaborate more what skill means?.
   
 12. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu Yusufummaka, aidha hukufanya uchunguzi yakinifu au ulifanya uchunguzi uliopotoka!
  - Leadership and Management madaktari wanasoma
  Community Medicine, subcourse ni leadership, conflict
  management etc
  -lakini kuna kozi za Saikolojia, Sociology nk ambazo ni lazima ujifunze kuhusu leadership. Wakati wakiwa masomoni huenda ktk wilaya mbalimbali kusimamia na kujifunza...na ndio maana huwa wanakuwa DMO, RMO, mawaziri, etc.

  -critical thinking:- Sidhani kama unaweza kumchukulia mtu aliyena ufaulu wa juu ktk masomo kama anashindwa kuanalyze vitu(Kama ukitaka kwa kigezo cha elimu), lakini ukitumia maamuzi magumu yanayofanyika kwa wagonjwa kutokana na mazingira duni(ukitumia kigezo cha uzoefu)

  kuchagua watu kwenda kutatua mgogoro:
  nadhani hujaelewa chanzo na hatua mbali mbali za mgomo hadi mwisho wa "uchunguzi wako"..kwani vikao vilishafanyika vingi hadi kufikia hatua ya Kamati ya Bunge kukutana(kwa kutumia pesa nyingine) lakini kutotoa taarifa hadi leo hii bungeni!!

  Inawezekana hujui mambo yalivyo sasa na unapaswa kukumbuka udaktari bila vitendo(practise) haiwezekani, ndio maana ilikuwa ngumu hata kuleta wastaafu(inahitaji kusoma na kujikumbushia kila leo) .Ni kweli umependekeza madaktari wazuri ktk kutatua mgogoro lakini unapaswa kujua wengi wao hawapo hospitalini(wanafanya kazi za utawala-vyuoni na serikalini)

  Bila 3.5mil!!
  -hakuna dai lililosema bila pesa hiyo hawarudi kazini, ila ilikuwa ni pendekezo lao, na hivyo upande wa pili ulipaswa kuja na pendekezo pia ili kujadili na kukubaliana. Ila upande wa pili unapokuja na kusema kuwa haiwezekani bila sababu, na kwa hoja kwamba hapo ndio mwisho wa mjadala, ushindani lazima utatokea!

  Kuwaeleza Umma:
  Hapa uelewa kuna makundi,
  - Wanaodhani wanajua madai kwa kusikiliza taarifa potofu
  -Wanaotaka kuelewa madai ya msingi
  -Wanaoelewa madai lakini kuyapotosha/kupinga kwa
  ushabiki
  -Wanaojua madai ya msingi na kuwatia moyo madaktari
  katika kuyadai.

  Uelimishaji:Ni ngumu sana kuelewesha waTZ wote kwa sababu zilizo wazi na pia ni ngumu kufanya hivyo kupitia vyombo vya habari na majukwaa kwani upande wa pili hautaki madaktari wakutane!!
   
 13. Nachingwea

  Nachingwea Senior Member

  #13
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 173
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35


  Hakika ni uharoo... u know what i mean!!!
   
 14. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135


  Hapo kwenye red, umenikumbusha mbali sana, kuhusu ile speech ya BOTHA kwa Black African south, lakini mkuu, na wewe pia ni Mwafrika, so you can not think beyond your nose and you can noy plan beong one year... What goes arround, comes back around, au vipi!
   
 15. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  prof yongolo na kahamba walikuwemo kwenye kamati, sasa nashangaa huyu doctor kajaje na kuongea pumba hapa. Hivi unajua kwamba ulimboka ndo aliyeendesha vuguvugu la 2005? Hivi unajua mph huwa wanasoma leadership and management? Au ye anataka mpaka mtu akasome kozi za wakata viuno? No one quotes silence! Ni bora kukaa kimya kuliko kuandika maelezo ya kitu usichokielewa.
   
 16. Bufa

  Bufa JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 4,167
  Likes Received: 3,372
  Trophy Points: 280
  Wish I could like this thread like 1000times, umenisemea yote niliyokua nawaza. Sasa shida inakuja kwa wabongo wanaowaunga mkono migomo ya madaktari bila hata kujua ni nini madatari wanagomea, pale ni mtu anaomba aongezewe mshahara wake sio kuboresha huduma mahospitalini hiyo ni kama subsidiary tu kwao.
   
 17. d

  davidfrance82 Member

  #17
  Jul 15, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Community medicine(including DMO weeks),psychology,sociology,psychiatry(tunawafundisha wagonjwa social skills nk ila wasiwe deviants kwenye jamii......)...na development studies for God's sake
  Hujui unachokieleza
   
 18. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  yusufummaka

  Your analysis lacks critical thinking too.
  Why do you think a person who has ability,
  to listen,
  to observe,
  to touch, to think, to analyze and prescribe best medicine available unaided;
  lacks critical thinking???

  Are you real thinking critically??
   
 19. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #19
  Jul 15, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  nahisi umekosea jukwaa kama mwenzio mleta sredi!
   
 20. Bufa

  Bufa JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 4,167
  Likes Received: 3,372
  Trophy Points: 280
  Nilijua tu utatokea mtu kama wewe ambaye kazi kukubali kila kitu madaktari wasemayo bila hata kujua tija yao, siku madatari wakisema tunataka wake zenu nadhani kuna watu kama nyie mtakubali coz mmeaminishwa na mmeamini kwamba taaluma ya udaktari tu ndio taaluma sahihi na yenye kuendesha nchi na inabidi wasikilizwe kila wasemalo na muda wowote wasemao na inabdi litimizwe instantly.
   
Loading...