Kama mashamba ni mengi , ni wazi miti imeongezeka , kwa hiyo, bei lazima ishuke maana ni maliggafi. Kama ni kupata faida lazima uuze mbao kama ilvyo kwa wakulima wa mahindi, anayepata faida ni muuza unga
Ukanda wote wa Afrika Mashariki na Kati si salama, vikundi vya kigaidi vinazidi kupata nguvu za kuijimarisha. Kwa hiyo, yanayotokea huku Msumbiji na tuweka katika hatari ya hata sisi huku TZ hasa mikoa ya kusini. Ni vizuri kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama unapoona dalili za uhalifu...
Kwanza wazo la biashara ni zuril Lakini ulitoka Dar kuja Arusha bila kuw ana taarifa za awali kama vile maharagae hayo yanapatikana Arusha sehemu gani, na kwa bei gani kwa gunia? Vile vile kama kuna gharama zingine mfano, tozo za Halmashauri kama zipo.
Nadhani alitaja umbali kakosea, yaani kilomit 10 hadi Mwanza alfu hamsini 58 hadi Geita. Kuna kitu hakijakaa sawa, inabidi wenyeji wa huko wafafanue ili kuondoa mchanganyiko huu.
Wafugaji wengi hawana malisho ya uhakika kwa mwaka mzima, hivyo, huhama hama kutafuta sehemu za malisho. Kwa vile mifugo inakuwa haina chakula inakimbilia kile penye chakula, na wale wanaowaswaga huwa wana uzembe au wanazidiwa maana ng'ombe huwa ni wengi hususani mifugo ya Maasai. Kunahitajika...
Nakushauri umalize kwanza masomo maana hata huko unakotaka kwenda kunatakiwa watu wenye elimu zao! Kuwa mvumilivu kwa muda umalize masomo , baadaye utapata ajira kulingana na fani (taaluma) yako. Vyombo vya ulinzi pia sasa vinajizatiti kwenye tekechnolojia ambayo ndiyo kila kitu leo hii
Halafu hiyo picha inaonesha askari akiwa amfuga ndevu, huko askari wanaruhusiwa kuwa 'o'. kwa mtindo huo, maadili yanakuwa kidogo au alikuwa mafichoni, hivyo, hajapata wembe wa kunyoa ndevu?!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.