Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,865
- 3,801
Bei ya miti hasa ya"Pine" imeporomoka mno mashambani, ingawa bei za mbao mijini hazijashuka. Huwezi amini ekari moja ya miti (Iliyostawi vizuri) ya miaka 10 ni kati ya mil.1.2 hadi 1.5. Siku za nyuma ekari moja ingeweza kuuzwa mil.5. au zaidi.
Visingizio vya wafanyabiashara ni kupanda kwa gharama za usafilishaji na miti kuwa mingi.
Ieleweke kuwa Miti ina gharama nyingi kuanzia ununuzi wa shamba, kusafisha shamba , kuandaa mashimo, ununuzi wa miche, gharama ya upandaji, na kusafisha miti hasa miaka 5 ya mwanzo. Hapo hapo kuna hatari (Risk) ya moto " Wild fire". Mfano msimu huu wa 2021baadhi ya maeneo ya Kilolo na Mufindi zaidi ekari 1000 zimeungua kwa moto.
Wale wazee wa kuaminishwa na "motivational speakers" kwamba miti ni utajiri tambueni kwa sasa kilimo cha miti ni umaskini tena wa muda mrefu. Fikiria unasubiri kwa miaka zaidi ya 10 aaafu unaambulia kijihela ambacho ni mshahara wa mtu wa mwezi mmoja. This is insane!