Nani kasema wananchi hawautaki. Kwa pacent ngapi? Na huo utafiti umefanyika lini na wapi? Hii nchi ni ya Watanzania siyo ya wakatoliki. Kuna madhehebu mengi pamoja na waislamu. Inakkuwaje TEC wasemee wananchiwote hawautaki nani kawapa kibali cha kuwasemea wasio wakatoliki. Hata Mwenyeezi Mungu...
Mwana FA msomi aliyepata shahada ya uzamili Uingereza na shahada ya kwanza IFM na Mbunge wa Muheza kwa nini asiwe naibu waziri. Acheni dharau pengine huna cv kama yake bado unamdharau
Nadhani una chuki na Makamba. Hii ni international tender. Mpaka mkataba usainiwe toka ilipotangazwa ni zaidi ya miezi minne. Maana yake Makamba ameikuta na kuingia mkataba. Ilikuwa ni mpango wa muda mrefu.
Air Tanzania ilianzishwa baada ya kuvunjika East African Airways ambapo mali zake ziligawanywa kwa nchi wanachama. Mali za Zanzibar zilijumuishwa kwenye mali za URT. Zanzibar ilikuwa mwanachama hivyo ATC ni ya URT.
Sio hivyo tu bro Jana tu Mwenyekiti kasema wanaomba wanachama wachange waongeze wachezaji wawili wa kimataifa. Kwa maana hiyo hawajamaliza usajili. Hii Ni njia ya kucheza na akili za Wana Yanga.
Kwa pwani na Morogoro mke huzikwa kwao hakuna Mila ya kuzikwa kwa mume. Ndiyo maana Iddi Take aliwashukuru wazazi wa Shamsa kwa kuwaruhusu kumzika mke wao kwao. Kwa mikoa ya pwani mke huzikwa kwa mume kwa ridhaa ya ndugu au wazazi wake.
Henu fanya utafiti wako upya. Kumbuka pwani yote kulikuwa na dola ya Kilwa kwenye 1300 hivi. Na wakati mtawala wa Kilwa anaanzisha dola yake alinunua ardhi kwa mtawala mwenyeji. isajorsergio,
Sent using Jamii Forums mobile app
Wanyama walikuwepo ikulu toka enzi ya mwalimu Nyerere. Tukiwa wadogo tulikuwa tukienda kuangalia wanyama. Wakati huo kulikuwa na wavu tu. Na ndiyo mwanzo wa kuletwa tausi wa ikulu toka India. Ila Sasa wameongezwa wanyama wengine.
Titicomb,
Sent using Jamii Forums mobile app
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.