Naomba kueleweshwa suala la ndege ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ya Tanzania Bara kupokelewa Zanzibar

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
948
2,857
NAOMBA KUELEWESHWA SUALA LA NDEGE YA WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI YA TANZANIA BARA KUPOKELEWA ZANZIBAR.

ZAA = Zanzibar
TAA = Tanzania BARA

Naomba kueleweshwa kwa Uhuru wa mawazo "the right to express my opinion under Article 18 of the Constitution of Tanzania of 1977" kuanzia zamani hakuna pa kuongelea hadi zama za G55 ,Mchungaji Mtikila na sasa kwenye social media utapata mengi kuhusu malalamiko ya watanzania bara.

Tafuta habari ya ndege kupokelewa Zanzibar kisha soma maoni au nenda kwenye Political platforms mbalimbali,

Hoja sio MATUMIZI
Bali swala la Ujenzi na uchukuzi sio la MUUNGANO
Kwanini swala sio la MUUNGANO likafanyike Zanzibar??
Lini swala lisilo la MUUNGANO la Zanzibar litafanyika Tanzania BARA??
Ukiondoa Waziri wa Ndani Ulinzi Nje hakuna Waziri mwingine yeyote anahusika na chochote kule Zanzibar.

Pia TGFA na ATCL hawahusiki lolote kule Zanzibar sababu wapo Chini ya Wizara ya Ujenzi na uchukuzi isiyo ya MUUNGANO
Hapa MAMLAKA za Viwanja vya ndege Zanzibar wanayo yao
Usajili wa vyombo VYA usafiri wao
Kila kitu cha Ujenzi na uchukuzi chao wao wenyewe pekee DAIMA DUMU,

Ni vizuri wajue kuwa hizo ndege ni za Wizara ya Ujenzi na uchukuzi ya Tanzania BARA huko Zanzibar ni MAPOKEZI tu
Wasije anza sema SMZ imenunua ndege hizo
 
Unaweza kukuta ndege tayari zimeingizwa kwenye mambo ya muungano, si sisi wenyewe ndo tumekalia usukani bhanaa.

Hata sUala la mzanzibari kuwa waziri wa uchukuzi halijakaa sawa maana hilo siyo jambo la muungano, na ukifuatilia unaweza kukuta hata ma-DED ambao ni wazanzibari....
 
Unaweza kukuta ndege tayari zimeingizwa kwenye mambo ya muungano, si sisi wenyewe ndo tumekalia usukani bhanaa...
Tuukuze utanzania zaidi kuliko kukuza mgawanyiko.Mimi kwangu sioni tatizo.Ndege zetu zinaruka katika anga la Tanzania ikiwemo Zanzibar.

Ndege hizi zinamilikiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio Wizara ya Uchukuzi na Ujenzi.Pia Rais wa Zanzibar ni mjumbe wa baraza la mawaziri katika serikali ya jamuhuri ya Muungano.
 
Tuukuze utanzania zaidi kuliko kukuza mgawanyiko.Mimi kwangu sioni tatizo.Ndege zetu zinaruka katika anga la Tanzania ikiwemo Zanzibar.Ndege hizi zinamilikiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio Wizara ya Uchukuzi na Ujenzi.Pia Rais wa Zanzibar ni mumbe wa baraza la mawaziri kataika serikali ya jamuhuri ya Muungano.
We huwajui vizuri Wazanzibar. Wao cha kwao ni cha kwao na cha kwetu ni chetu
 
NAOMBA KUELEWESHWA SUALA LA NDEGE YA WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI YA TANZANIA BARA KUPOKELEWA ZANZIBAR...

EDD6571D-E8E0-433C-AF65-8DEBE111105F.jpeg
 
Zabayanga Ndiyo Anasimamia Muungano Nategemea Aseme Neno.

Kulikoni Hili Jambo Ndege.

Nimemkumbuka Ibrahim Msabaha Akiwa Waziri Sakata La Richmond.

Alipobanwa Huko Bungeni Akasema Wazi Hajui Lolote Ila Yeye Ni Kondoo Wa Kafara, Hapo Akasema Kizaramo (Bangusiro) Anapangusiwa.

Hili Jambo La Ndege Baadaye Kuna Kitu Tu
 
Unaweza kukuta ndege tayari zimeingizwa kwenye mambo ya muungano, si sisi wenyewe ndo tumekalia usukani bhanaa. Hata sUala la mzanzibari kuwa waziri wa uchukuzi halijakaa sawa maana hilo siyo jambo la muungano, na ukifuatilia unaweza kukuta hata ma-DED ambao ni wazanzibari....
isee kama ni amri yangu zanzibar ningefanya tu jiji then wizara zote zingekuwa sawa na ningeamisha watu wengi sana hasa walaimu na maness na askari wazanzibar wangekuja huku na wa huku wangeenda kule hii ingesaidia kuondoa ile hali ya sisi wazanzibar sijui nini nini...ingepotea kabisa..
 
Unaweza kukuta ndege tayari zimeingizwa kwenye mambo ya muungano, si sisi wenyewe ndo tumekalia usukani bhanaa. Hata sUala la mzanzibari kuwa waziri wa uchukuzi halijakaa sawa maana hilo siyo jambo la muungano, na ukifuatilia unaweza kukuta hata ma-DED ambao ni wazanzibari....
Utaambiwa Kesh ya kununua imechangiwa na Watanzania wote. Hakuna la zaidi ya kuipa pride Zenji si unajua mwamba ngozi!
 
isee kama ni amri yangu zanzibar ningefanya tu jiji then wizara zote zingekuwa sawa na ningeamisha watu wengi sana hasa walaimu na maness na askari wazanzibar wangekuja huku na wa huku wangeenda kule hii ingesaidia kuondoa ile hali ya sisi wazanzibar sijui nini nini...ingepotea kabisa..
Hii ndo move aliyoshindwa kuicheza Nyerere pamoja na kuwa na upper hand kwenye negotiations zilizopelekea integration na zanzibar.....babu sijui alikuwa anawaza nini. Sasa unajikuta unatumia pesa nyingi ku-run serikali inayohudumia watu milioni moja unaipa status ya nchi wakati ungeweza kuipa status ya mkoa na kuondoa hizi kelele kelele zinazoendelea sasa.
 
Back
Top Bottom