Lina uzito wa tani, jiwe jeusi la chato
Jiwe jeusi si dini, jiwe halina mvuto
Sasa nikusimulieni, limepataje uzito
Hata mkifika mia, hamlibebi kitoto
Washi walilipinga, kutaka kulisimika
Ya rangi wakayapanga, hili hawakulishika
Mawe yakatoa unga, na ponde yakapondeka
Hata mkifika mia, hamlibebi...