Jiwe Jeusi la Chato

doullar

Member
Dec 29, 2016
31
13
Lina uzito wa tani, jiwe jeusi la chato
Jiwe jeusi si dini, jiwe halina mvuto
Sasa nikusimulieni, limepataje uzito
Hata mkifika mia, hamlibebi kitoto

Washi walilipinga, kutaka kulisimika
Ya rangi wakayapanga, hili hawakulishika
Mawe yakatoa unga, na ponde yakapondeka
Hata mkifika mia, hamlibebi kitoto

Jiwe wakalisimika, na rangi yake nyeusi
Yakawajaa mashaka, jiwe jeusi jepesi
Imani hawakuweka, wakajiona wakosi
Hata mkifika mia, hamlibebi kitoto

Jua likapiga sana, jiwe likajitanua
Jiwe la mwamba mpana, likamea na kukua
Nafasi likaibana, ufa halikuachia
Hata mkifika mia, hamlibebi kitoto

Habari zikaenea, mashariki nako bara
watu wakalisifia, jiwe ni jiwe imara
wadini wakaombea, gizani lizidi ng'ara
Hata mkifika mia, hamlibebi kitoto

Sasa wamekuja washi, na sururu za uchina
Wadai nao watashi, kung'oa mawe ya kina
Wameanza ulalamishi, jiwe ni jeusi sana
Hata mkifika mia, hamlibebi kitoto

Udom- 0656845335
 
Kweli hakuna jipya chini ya jua. Miaka ya 80 Raisi Mwinyi naye aliandikiwa shairi, moja ya mstari ninaoukumbuka ulisema hivi "Mwinyi ukiwa mkali naona furaha ya kuwa raia"
 
Kweli hakuna jipya chini ya jua. Miaka ya 80 Raisi Mwinyi naye aliandikiwa shairi, moja ya mstari ninaoukumbuka ulisema hivi "Mwinyi ukiwa mkali naona furaha ya kuwa raia"

Mambo mengi hujirudia, ingawa wakati mwingine na kwa namna ya utofauti
 
Unasema uko Udom? na wazazi wako wanalipa ada?hata kuandika hujui!
 
Back
Top Bottom