Roho ya kukataliwa: Chanzo/asili na madhila yake

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,638
697,929
Kama wewe si mmojawapo basi kwa vyovyote kuna mtu unamfahamu mwenye hili tatizo. Anaweza kuwa ndugu jamaa ama rafiki. Ni jambo baya na lenye kutatiza mno. Watoto wa mtaani wanasema KIMAVI.

Mind you sizungumzii ile kuchukiwa na mtu mmoja mmoja kwa sababu zisizoeleweka. Huwezi kupendwa na kila mtu.. Ni lazima haters wawepo. Ni watu wasiokupenda tu. Na huweza hata kujenga uadui mkubwa na wewe.

Pia sizungumzii ishu za kisiasa, umaarufu, mali, mafanikio na uongozi. Kwakuwa hapa kuna watu automatically hawapendi kuwaona wengine wana maisha mengine positive tofauti na wao. Kushindwa kwako ndio furaha yao. Kadiri unavyofanikiwa kimaisha ndio maadui huongezeka.. Kwahiyo singumzii kwa muktadha huu pia.

Nazungumzia kuhusu wale ambao kiasili bila kujali kama wanacho ama hawana.. Ni watu wenye nyota iliyofifia ama kufa kabisa... Hawapendwi at the first place... Hata kama hawajaongea chochote, hata kama hawajafanya chochote... Kwa mfano unafika mahali penye mkusanyiko wa watu.

Mara zinapigwa kelele za mwizi bila hata hujajua nini kimetokea unakuwa mtuhumiwa wa kwanza... Anakuja chizi mahali mko wengi lakini anakunasa kibao wewe... Mnapita mahali kuna mbwa anawaacha wengine wote na kukuandama wewe.. Yaani ni karaha mwanzo mwisho.

Hakuna kitu kinachokosa chanzo... Ama asili.... Mimba zinapotungwa huwa kuna vita ya kumgombea kiumbe atakayezaliwa.. Hapa kuna nguvu hasi na nguvu chanya.. Hii hutokea pia wakati wa kujifungua... Hii vita hutokea sehemu hizo mbili... Kumbuka mada ya manii zilizokosea njia, je kuna mimba za bahati mbaya?

Nguvu chanya ndio yenye nguvu zaidi, ni uumbaji uliokusudiwa na Maulana, ndio uumbaji wa nyota inayowaka lakini shetani na mawakala wake( wanga, wachawi na mabaradhuli) hupenda kufanya shindano na Maulana.. Kumbuka alishafanya hivyo pale Eden basi tambua hata leo hii anaendelea hajaacha.

Hapo sasa kuna mambo mawili nyota yako inaweza kuwaka kwa njia chanya.. Utapendwa na karibia kila mtu kwa upole ucheshi, huruma, kujitoa kwako nk nk... Nyota yako ikiwaka kwa njia hasi utaogopeka na kila mmoja kwa matendo yako mabaya ya kikatili ya kutisha na ya kibaradhuli kabisa.

Sasa nyota yako ikisimama kwenye 0 yaani sio hasi wala sio chanya ndio roho ya kukataliwa inapozaliwa... Yaani shetani alijaribu kukupoka kwenye chanya lakini akaishia kukuangusha njiani... Hapo ni tabu tupu.

Sasa basi kama nilivyoeleza hapo juu shetani na mawakala wake daima ni watu wa mashindano... Hivyo akikukosa wakati wa kutungwa mimba, akikukosa wakati wa kuzaliwa, akikukosa wakati wa makuzi atakutafuta tu popote mpaka akupate! KIAJE!?

1. Kipindi cha balehe... Unapoingia hatua ya ukubwani.. Hatua ya kujitambua... Unaanza kutafakari maisha yako ya nyuma , wazazi ama walezi au ndugu waliokukuza.. Unaingalia jamii na kuhisi kutengwa... Hapa ukikosea tu na kumpa shetani nafasi umekwenda na maji.. Ataanza kukuonyesha vitu vidogo vidogo mno.. Atakuonyesha kuwa nyumbani hupendwi kama fulani, shuleni mwalimu fulani hakupendi... Marafiki nao unahisi hivyo hivyo... Taratibu unaanza kujichukia na kujiona hufai.. Unajenga inferiority complex, unajitenga na jamii na tayari roho ya kukataliwa inazaliwa.

Wazazi na walezi... Tuwe makini sana na hatua hii kwa vijana wetu.. Tuwasaidie waweze kuivuka salama...

2. Baada ya balehe ni kipindi cha ndoto nyingi... Kuota mafanikio, kuota umaarufu, kuota utajiri, kupendwa nknk... Hapa napo shetani hachezi mbali.. Ataanza kukuonyesha agemate wako walivyo na maisha mazuri na mafanikio... Na sometimes sio kwamba uko vibaya bali ni ile roho ya kutaka zaidi... Hapa sasa ndio unaingizwa rasmi kwenye ulimwengu wa maagano ya kuboost nyota bila kujua
Hiki ndio kipindi cha kutafuta ndele ya mvuto kwenye mapenzi, Pete za bahati, hirizi za mafanikio..

Wataalam wa kusafisha nyota nknk... Ukikubali kuuingia huu mkenge UMEKWISHA... utaenda kwa mganga kutafuta ndele.. Hakwambii madhara anakupa tuu.. Utaanza kuwa na mvuto utapendwa na kila mwanamke kuanzia chizi mbaya mzuri mlemavu mrefu kwenda chini, kipipa nknk wote watakuwa wako mpaka unakereka.. Ila mganga kakuficha kitu kimoja... Ndele ina life span.. Ikiisha utachukiwa mpaka na siafu.. Mapete ya bahati, hirizi za mafanikio, kusafisha nyota vyote hivi vina kikomo cha matumizi.

3. Maisha ya ukubwani sasa... Hapa umepambana na changamoto za maisha umefeli na kufaulu... Umepita kwingi na kufanya mengi.. Umeshawahi kujaribu hata option no 2 ya mapete na mahirizi na kusafisha nyota.. Ukapata mafanikio ya muda.. Lakini baadae ukaanguka vibaya kabisa... Kwa Neema tu ukaweza kusimama tena sasa unataka kurudi hewani... Hapa hutaki tena njia ya giza...unataka njia ya nuru lakini kumbuka shetani bado yuko nawe hakuachi.

Badala ya kukuacha uende njia sahihi.. Anakuelekeza kwa mitume na manabii wanakohubiri mafanikio na utajiri wa vitu viharibikavyo... Unarudi kule kule kwa wapiga ramli na waganga wasafisha nyota.. Unauziwa maji ya baraka vitambaa nk.. Unaanza kuhangaika kwenye masinagogi ya hawa watu na mwisho unakufa bila kupata ulichotarajia.

Rafiki mpendwa pambana na hali yako, usimwache muumba wako hata nukta moja.. Hakuna binadamu aliyezaliwa na mwanamke anaweza kusafisha nyota yako ikasafishika milele.. HAKUNA.. hakuna mganga atakayeweza kukupa mafanikio yasiyo na maagano HAKUNA... hakuna Pete ya bahati isiyokosa mawaa HAKUNA... jaribu kuivua siku moja uone shughuli yake.

Usifuate mkumbo ila kama ukiona mambo hayaendi na kweli kabisa unajiona wewe mwenyewe una roho ya kukataliwa.. Basi simama na Mungu wako kwa imani yako huku ukijitakasa na chumvi... Ile asilia.. Chumvi haina gharama. Chumvi haina maagano.. Chumvi haina madhara... Itumie kawaida kwa kuogea ni chaja bora isiyochuja.

Nakuombea.

Jr future pastor
 
Kweli haya mambo yapo.... Unakuta mtu hapendwi na kila mtu... Kama ni mwanafunzi wenzake watamchukia bila sababu.. Kama ni mipango inaharibika bila sababu za msingi.

Mungu atusaidie tu ndugu yangu maana dunia hii ina mambo.

Hivi haya mambo ya nyota kuchafuka ni kweli yapo.? Kuna kipimdi mtu unajaribu kila njia kufanikisha jambo flani la kiuchumi inashindikana. Unabadilisha biashara/mradi nao unashindika kwa kila namna na njia utakayotumia.

Ni kweli nyota zinaweza haribiwa au kuibiwa na wachawi, ndugu au wafanyabiashara? Na inakuwaje?
 
Kweli haya mambo yapo.... Unakuta mtu hapendwi na kila mtu... Kama ni mwanafunzi wenzake watamchukia bila sababu.. Kama ni mipango inaharibika bila sababu za msingi.

Mungu atusaidie tu ndugu yangu maana dunia hii ina mambo.

Hivi haya mambo ya nyota kuchafuka ni kweli yapo.? Kuna kipimdi mtu unajaribu kila njia kufanikisha jambo flani la kiuchumi inashindikana. Unabadilisha biashara/mradi nao unashindika kwa kila namna na njia utakayotumia.

Ni kweli nyota zinaweza haribiwa au kuibiwa na wachawi, ndugu au wafanyabiashara? Na inakuwaje?
Yote hayo yanawezekana kabisa lakini isiwe ndio chanzo cha kwenda kutafuta ufumbuzi gizani.. Tatizo ni kwamba siku hizi tumepotoka na kupotea kabisa.. Hatusomi maandiko kwa tafakuri... Na hasa ukizingatia hizi kampeni za kupinga uwepo wa Mungu na kukosoa misahafu yake basi ni shida tupu

Maisha lazima yawe na changamoto na hizo changamoto lazima uzikabili wewe mwenyewe na Mungu wako.. Vingine vyote vitakuwa bandia.. Waganga wa kienyeji manabii na mitume, mapete ya bahati hirizi nk

Unapopitia hizi changamoto mkumbuke Ayubu.. Mahali alipokuwa kafika, madhila aliyopata na hatimaye kuweza kusimama tena.. Kwa dunia ya leo watu wangekunywa sumu.
 
supernatural is real... Poverty is phenomenon... A myth...!!!
Dude go see a doctor if you think poverty is a myth. Unless you live on a different planet there’s no way you haven’t seen poverty with your own eyes even in the developed world. Saying supernatural is real but poverty is a myth you must be drunk.

Supernatural is something created by lazy assholes who wanted something to blame for everything that went wrong in their damn lives, and others supported that bs because it worked well with their own agendas, then comes the stupid followers who accepted that bs without questioning, that’s one of the reasons some societies today still live like they are in the 18th century.

You want proof? Lets not go far, just have a look at all those who love your supernatural bs, most of them poor or plain ignorant with zero plan in life, always looking to hide in some stupid fantasy. The truth hurts sometimes but someone has to say it
 
Back
Top Bottom