Daraja la Mto Wami kulikoni Serikali inalifumbia macho? Tunasubiri vifo ndio tukurupuke?

MAFIE JR

Senior Member
Feb 20, 2016
117
92
Wadau,

Napenda kutoa wazo au ushauri au msukumo au kuishawishi serikali kwamba daraja hili la mto Wami sasa linatutia aibu na lijengwe kisasa sasa maana kwa miaka hii 50 ya Uhuru hatupashwi kuona magari yakisubiriana kupishana juu ya daraja

Mheshimiwa Rais wangu na Serikali yako embu fanyeni jambo juu ya hili daraja sasa maana ni kiungo muhimu kwa mikoa hii ya Kaskazini na nchi jirani na ni kiungo muhimu kwa uchumi wetu.Hili daraja likitengenezwa kisasa litasaidia mapato kwa nchi yetu. Litatoa hofu kwa watumiaji maana palivyo panatisha na ikizingatiwa kule chini kuna mamba haswa.

Najiuliza kama serikali imeweza kujenga daraja la Kigamboni tena juu ya bahari je hili la Wami ni nini mpaka ishindwe nikijaribu kufanya tathmini ya macho naona kama ku-cross pale hakuna hata mita 500 so hata gharama yake ya ujenzi yaweza kuwa ndogo zaidi kuliko ile ya daraja la Kigamboni au daraja la Mkapa kule Kusini.

Kuna manufaa makubwa yanayoweza kupatikana kwa ujenzi huu both Economically, Socially na hata politically.

Shime Serikali ya awamu ya tano embu fanyeni mabadiliko katika daraja hili lililopo kilomita kadhaa kutokea Chalinze kuelekea Arusha na mita chache ukishavuka eneo la mafunzo ya Kijeshi Msata (kwa wasiolijua).

Serikali ya CCM chini ya Jemedari wangu Rais Magufuli najua mtanisikiliza wazo langu na mtalitendea kazi.

Mafie Jr
 
Nimependa UZI wako ila nimesikitika kidogo hapo uliposema " mita chache ukishavuka eneo la mafunzo ya Kijeshi Msata ". Mkuu usiamini Watu humu kwani kwa UBUNIFU na aina mpya ya UJASUSI uliopo duniani kwa sasa unaweza ukajikuta hicho ulichokisema tayari umesharahisisha Kazi za Watu. Vitu vingine tena hasa maeneo NYETI kama hayo epuka sana kuyaweka hadharani namna hiyo. Naomba radhi kama maelezo yangu haya yatakukwaza ila nirudie tu kukusihi tena kuwa USIAMINI kila Mtu humu Mtandaoni na hata hapo ulipo dunia ya sasa IMESHAHARIBIKA na Watu hadi Mataifa wanawindana / yanatafutana.

Ni kweli hilo daraja la Wami linatia AIBU ila huwezi jua yawezekana limeachwa hivyo lilivyo ili pengine liwe moja ya Kivutio cha Kale cha Watalii wa ndani ( sisi Wabongo na Wazungu ) na kumbukumbu kwa Watoto wetu akina Samora na Isabela na Vizazi vyao pia vijavyo.

Msichokijua juu ya hilo daraja ni kwamba huwa kuna mambo ya " Kiswahili " sana hapo yanatendeka kama Matambiko ya Kabila fulani maarufu kwa miaka 10 iliyopita ambapo kwa Wenyewe Madereva wanaopita hapo kuanzia usiku wa Saa 4 wanasema kama haupo " fiti " kwa " miziziology " na Wewe unaweza hilo Daraja usilione au ukashtukia tu umeangusha Gari.

Na kama haitoshi Mto Wami ndiyo Mto ulio na KINA kikubwa sana ambapo mara zote maji yake ukiyatizama kwa juu yanaonekana yametulia ila chini yake yanaenda kwa SPIDI kubwa mno. Kwa rekodi nilizo nazo hakuna Gari hapo ambalo limewahi kutumbukia na likaokolewa na nakumbuka Miaka ya 1993 hadi 1994 kuna Hiace moja ilizama hapo na ikapotea ghafla tu na Watu waliokuwa wakijiona ni Waogoleaji wazuri na Wao wakaamua kupiga " mbizi " kwa minajili ya kuliokoa lile Gari lakini na Wao walijikuta wakiwa ni " wasindikizaji " wazuri wa ile Gari ( namaanisha WALIKUFA ) na maiti zao hazikupatikana kabisa.

Na Wajuvi wa masuala ya Mito wanakuambia ni kheri udakwe na Mamba wa Mto Ruaha kuliko Mamba wa Mto Wami jibu wanalo wenyewe.
 
Gentamycine: Salute bro....niligundundua hilo kosa baada ya kupost....ila najua wazee wa kazi watanisamehe najua wana uwezo mkubwa wa kupambanua mambo hili watalifunika maana hata mimi ni mzalendo NA naamini katika maslahi ya nchi kwanza....

Makosa na upungufu wa mada nisamehewe mimi
 
Nimependa UZI wako ila nimesikitika kidogo hapo uliposema " mita chache ukishavuka eneo la mafunzo ya Kijeshi Msata ". Mkuu usiamini Watu humu kwani kwa UBUNIFU na aina mpya ya UJASUSI uliopo duniani kwa sasa unaweza ukajikuta hicho ulichokisema tayari umesharahisisha Kazi za Watu. Vitu vingine tena hasa maeneo NYETI kama hayo epuka sana kuyaweka hadharani namna hiyo. Naomba radhi kama maelezo yangu haya yatakukwaza ila nirudie tu kukusihi tena kuwa USIAMINI kila Mtu humu Mtandaoni na hata hapo ulipo dunia ya sasa IMESHAHARIBIKA na Watu hadi Mataifa wanawindana / yanatafutana.

Ni kweli hilo daraja la Wami linatia AIBU ila huwezi jua yawezekana limeachwa hivyo lilivyo ili pengine liwe moja ya Kivutio cha Kale cha Watalii wa ndani ( sisi Wabongo na Wazungu ) na kumbukumbu kwa Watoto wetu akina Samora na Isabela na Vizazi vyao pia vijavyo.

Msichokijua juu ya hilo daraja ni kwamba huwa kuna mambo ya " Kiswahili " sana hapo yanatendeka kama Matambiko ya Kabila fulani maarufu kwa miaka 10 iliyopita ambapo kwa Wenyewe Madereva wanaopita hapo kuanzia usiku wa Saa 4 wanasema kama haupo " fiti " kwa " miziziology " na Wewe unaweza hilo Daraja usilione au ukashtukia tu umeangusha Gari.

Na kama haitoshi Mto Wami ndiyo Mto ulio na KINA kikubwa sana ambapo mara zote maji yake ukiyatizama kwa juu yanaonekana yametulia ila chini yake yanaenda kwa SPIDI kubwa mno. Kwa rekodi nilizo nazo hakuna Gari hapo ambalo limewahi kutumbukia na likaokolewa na nakumbuka Miaka ya 1993 hadi 1994 kuna Hiace moja ilizama hapo na ikapotea ghafla tu na Watu waliokuwa wakijiona ni Waogoleaji wazuri na Wao wakaamua kupiga " mbizi " kwa minajili ya kuliokoa lile Gari lakini na Wao walijikuta wakiwa ni " wasindikizaji " wazuri wa ile Gari ( namaanisha WALIKUFA ) na maiti zao hazikupatikana kabisa.

Na Wajuvi wa masuala ya Mito wanakuambia ni kheri udakwe na Mamba wa Mto Ruaha kuliko Mamba wa Mto Wami jibu wanalo wenyewe.
Mkuu umesema ukweli kwani humu hata walimbi... Wamo
 
Mzee hebu punguza Imani potofu dah! !uko karne ya ngapi aisee?utaharibu hata watoto sasa. Kuhusu kambi ya jeshi ile sio siri bana mbona iko road kabisa!
 
Hata hivyo nilichokisema kilikuwa ni kama tu ushauri kwake sasa nashangaa " unavyopovuka ".
 
Back
Top Bottom