Daraja la Mto Wami kulikoni Serikali inalifumbia macho? Tunasubiri vifo ndio tukurupuke?

Wadau,

Napenda kutoa wazo au ushauri au msukumo au kuishawishi serikali kwamba daraja hili la mto Wami sasa linatutia aibu na lijengwe kisasa sasa maana kwa miaka hii 50 ya Uhuru hatupashwi kuona magari yakisubiriana kupishana juu ya daraja

Mheshimiwa Rais wangu na Serikali yako embu fanyeni jambo juu ya hili daraja sasa maana ni kiungo muhimu kwa mikoa hii ya Kaskazini na nchi jirani na ni kiungo muhimu kwa uchumi wetu.Hili daraja likitengenezwa kisasa litasaidia mapato kwa nchi yetu. Litatoa hofu kwa watumiaji maana palivyo panatisha na ikizingatiwa kule chini kuna mamba haswa.

Najiuliza kama serikali imeweza kujenga daraja la Kigamboni tena juu ya bahari je hili la Wami ni nini mpaka ishindwe nikijaribu kufanya tathmini ya macho naona kama ku-cross pale hakuna hata mita 500 so hata gharama yake ya ujenzi yaweza kuwa ndogo zaidi kuliko ile ya daraja la Kigamboni au daraja la Mkapa kule Kusini.

Kuna manufaa makubwa yanayoweza kupatikana kwa ujenzi huu both Economically, Socially na hata politically.

Shime Serikali ya awamu ya tano embu fanyeni mabadiliko katika daraja hili lililopo kilomita kadhaa kutokea Chalinze kuelekea Arusha na mita chache ukishavuka eneo la mafunzo ya Kijeshi Msata (kwa wasiolijua).

Serikali ya CCM chini ya Jemedari wangu Rais Magufuli najua mtanisikiliza wazo langu na mtalitendea kazi.

Mafie Jr
Haya mabilioni tunayoyatumia kwenye chaguzi za marudio ya wanaojiuzulu kuunga mkono tungeweza kuyatumia kujenga daraja jipya na pana pale na kuachana na starehe za wanaojiuzulu kwakuwa kujiuzulu kwa hiyari ni starehe siyo takwa la msingi hivyo walipaswa waachwe hadi 2020 Lakini mkubwa mmoja huwa anapenda kusema kupanga ni kuchagua. Tumepanga na kuchagua kutumia mabilioni kuwapa starehe wanaojiuzulu!
 
Gentamycine: Salute bro....niligundundua hilo kosa baada ya kupost....ila najua wazee wa kazi watanisamehe najua wana uwezo mkubwa wa kupambanua mambo hili watalifunika maana hata mimi ni mzalendo NA naamini katika maslahi ya nchi kwanza....

Makosa na upungufu wa mada nisamehewe mimi
Sasa mbona yale majengo yapo karibu kabisa na barabara sasa kunakujificha kwa namna gani wakati kila mtu anayaona yale maghorofa. Mimi sioni kama kuna siri yoyote umefichua hapo kwakuwa wao wenyewe wamesogeza majengo yao barabarani kabisa kila anayepita anayaona
 
Nimependa UZI wako ila nimesikitika kidogo hapo uliposema " mita chache ukishavuka eneo la mafunzo ya Kijeshi Msata ". Mkuu usiamini Watu humu kwani kwa UBUNIFU na aina mpya ya UJASUSI uliopo duniani kwa sasa unaweza ukajikuta hicho ulichokisema tayari umesharahisisha Kazi za Watu. Vitu vingine tena hasa maeneo NYETI kama hayo epuka sana kuyaweka hadharani namna hiyo. Naomba radhi kama maelezo yangu haya yatakukwaza ila nirudie tu kukusihi tena kuwa USIAMINI kila Mtu humu Mtandaoni na hata hapo ulipo dunia ya sasa IMESHAHARIBIKA na Watu hadi Mataifa wanawindana / yanatafutana.

Ni kweli hilo daraja la Wami linatia AIBU ila huwezi jua yawezekana limeachwa hivyo lilivyo ili pengine liwe moja ya Kivutio cha Kale cha Watalii wa ndani ( sisi Wabongo na Wazungu ) na kumbukumbu kwa Watoto wetu akina Samora na Isabela na Vizazi vyao pia vijavyo.

Msichokijua juu ya hilo daraja ni kwamba huwa kuna mambo ya " Kiswahili " sana hapo yanatendeka kama Matambiko ya Kabila fulani maarufu kwa miaka 10 iliyopita ambapo kwa Wenyewe Madereva wanaopita hapo kuanzia usiku wa Saa 4 wanasema kama haupo " fiti " kwa " miziziology " na Wewe unaweza hilo Daraja usilione au ukashtukia tu umeangusha Gari.

Na kama haitoshi Mto Wami ndiyo Mto ulio na KINA kikubwa sana ambapo mara zote maji yake ukiyatizama kwa juu yanaonekana yametulia ila chini yake yanaenda kwa SPIDI kubwa mno. Kwa rekodi nilizo nazo hakuna Gari hapo ambalo limewahi kutumbukia na likaokolewa na nakumbuka Miaka ya 1993 hadi 1994 kuna Hiace moja ilizama hapo na ikapotea ghafla tu na Watu waliokuwa wakijiona ni Waogoleaji wazuri na Wao wakaamua kupiga " mbizi " kwa minajili ya kuliokoa lile Gari lakini na Wao walijikuta wakiwa ni " wasindikizaji " wazuri wa ile Gari ( namaanisha WALIKUFA ) na maiti zao hazikupatikana kabisa.

Na Wajuvi wa masuala ya Mito wanakuambia ni kheri udakwe na Mamba wa Mto Ruaha kuliko Mamba wa Mto Wami jibu wanalo wenyewe.
Uko sahihi kuwa na tahadhari lkn kwa dunia hii ya kisasa maeneo ya kiusalama au silaha unazomiliki siyo siri tena ilikuwa zamani hizo. Siri inabaki kuwa mbinu na uwezo wako wa intelijensia. Ktk jeshi siku hizi siri ni uwezo na mbinu zako za medani /mapigano basi, silaha unazomiliki na uwezo wake siyo siri kwa sababu kwanza hizo silaha hukuzitengeneza wewe. Ila narudia kwa tahadhari yako ni vizuri hayo maeneo tukayaacha na unyeti wake.
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Kutoa lile daraja la Wami ni sawa na kuwahamisha wakwere wote waende kuishi Mwanza, hii si sawa wataenda tambikia wapi? Ndugu mmoja aliweza kutoa maji pale Wami akasambaza kwa Wakwere kila nyumba lakini daraja akaliacha mnafikiri alikuwa hamnazo? liacheni daraja lao kwani kama ni hasara ni kidogo tu inavumilikaa jamani na ndio maana hamjawasikia wabunge wao (2) wakilalamikia daraja hilo iweje pilipili usiyoila ikuwasheni?
Kama hilo daraja ni la muhimu sana kwao..basi liachwe then lijengwe jingine pembeni....
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Nimependa UZI wako ila nimesikitika kidogo hapo uliposema " mita chache ukishavuka eneo la mafunzo ya Kijeshi Msata ". Mkuu usiamini Watu humu kwani kwa UBUNIFU na aina mpya ya UJASUSI uliopo duniani kwa sasa unaweza ukajikuta hicho ulichokisema tayari umesharahisisha Kazi za Watu. Vitu vingine tena hasa maeneo NYETI kama hayo epuka sana kuyaweka hadharani namna hiyo. Naomba radhi kama maelezo yangu haya yatakukwaza ila nirudie tu kukusihi tena kuwa USIAMINI kila Mtu humu Mtandaoni na hata hapo ulipo dunia ya sasa IMESHAHARIBIKA na Watu hadi Mataifa wanawindana / yanatafutana.

Ni kweli hilo daraja la Wami linatia AIBU ila huwezi jua yawezekana limeachwa hivyo lilivyo ili pengine liwe moja ya Kivutio cha Kale cha Watalii wa ndani ( sisi Wabongo na Wazungu ) na kumbukumbu kwa Watoto wetu akina Samora na Isabela na Vizazi vyao pia vijavyo.

Msichokijua juu ya hilo daraja ni kwamba huwa kuna mambo ya " Kiswahili " sana hapo yanatendeka kama Matambiko ya Kabila fulani maarufu kwa miaka 10 iliyopita ambapo kwa Wenyewe Madereva wanaopita hapo kuanzia usiku wa Saa 4 wanasema kama haupo " fiti " kwa " miziziology " na Wewe unaweza hilo Daraja usilione au ukashtukia tu umeangusha Gari.

Na kama haitoshi Mto Wami ndiyo Mto ulio na KINA kikubwa sana ambapo mara zote maji yake ukiyatizama kwa juu yanaonekana yametulia ila chini yake yanaenda kwa SPIDI kubwa mno. Kwa rekodi nilizo nazo hakuna Gari hapo ambalo limewahi kutumbukia na likaokolewa na nakumbuka Miaka ya 1993 hadi 1994 kuna Hiace moja ilizama hapo na ikapotea ghafla tu na Watu waliokuwa wakijiona ni Waogoleaji wazuri na Wao wakaamua kupiga " mbizi " kwa minajili ya kuliokoa lile Gari lakini na Wao walijikuta wakiwa ni " wasindikizaji " wazuri wa ile Gari ( namaanisha WALIKUFA ) na maiti zao hazikupatikana kabisa.

Na Wajuvi wa masuala ya Mito wanakuambia ni kheri udakwe na Mamba wa Mto Ruaha kuliko Mamba wa Mto Wami jibu wanalo wenyewe.
ASIYAWEKE HADHARANI KWANI YAPO MBINGUNI| KAMA NI MAENEO NYETI BASI YANUNULIWE CHUPI.
 
Hoja ya maana kabisa, ila siwakati muafaka, taifa liko msibani mkuu, wakubwa hawakusikii, hebu jipe muda kisha urudie tena
 
Mzee hebu punguza Imani potofu dah! !uko karne ya ngapi aisee?utaharibu hata watoto sasa. Kuhusu kambi ya jeshi ile sio siri bana mbona iko road kabisa!
hahaa kweli maana ilo eneo sio la siri,na hao majasusi wanashindwa kupata location mpaka waje JF...
 
napata tabu sana napousikia mto huu naomba nipate majibu juu ya maswali yangu
1/wami umeanzia wapi
2/umekutana na bahari je ni sehemu gani
3/una unasaba na mto Ruvu wa malandizi
4/wami wa chalinze unahusiana na wami wa Korogwe
5/una unasaba na mto Pangani
6/wa chalinze umeingilia wapi baharini
kama una maelezo zaidi juu ya mito hii ruvu juu, ruvu chini, wami,pangani
 
Na kama haitoshi Mto Wami ndiyo Mto ulio na KINA kikubwa sana ambapo mara zote maji yake ukiyatizama kwa juu yanaonekana yametulia ila chini yake yanaenda kwa SPIDI kubwa mno. Kwa rekodi nilizo nazo hakuna Gari hapo ambalo limewahi kutumbukia na likaokolewa na nakumbuka Miaka ya 1993 hadi 1994 kuna Hiace moja ilizama hapo na ikapotea ghafla tu na Watu waliokuwa wakijiona ni Waogoleaji wazuri na Wao wakaamua kupiga " mbizi " kwa minajili ya kuliokoa lile Gari lakini na Wao walijikuta wakiwa ni " wasindikizaji " wazuri wa ile Gari ( namaanisha WALIKUFA ) na maiti zao hazikupatikana kabisa.

Na Wajuvi wa masuala ya Mito wanakuambia ni kheri udakwe na Mamba wa Mto Ruaha kuliko Mamba wa Mto Wami jibu wanalo wenyewe.
Marehemu Prof Maji Marefu hakuwahi kufika hapo?
 
napata tabu sana napousikia mto huu naomba nipate majibu juu ya maswali yangu
1/wami umeanzia wapi
2/umekutana na bahari je ni sehemu gani
3/una unasaba na mto Ruvu wa malandizi
4/wami wa chalinze unahusiana na wami wa Korogwe
5/una unasaba na mto Pangani
6/wa chalinze umeingilia wapi baharini
kama una maelezo zaidi juu ya mito hii ruvu juu, ruvu chini, wami,pangani
The Wami River lies entirely within Tanzania in the Pwani Region and Morogoro Region in eastern Tanzania. Its source is specified in the Kaguru Mountains and it flows East entering the Indian Ocean west of Zanzibar. But its catchment area extends from the Kinyasangwe River to far beyond Dodoma to the southern edge of the Maasai Steppe and is denoted with 43,946 km². Only after leaving the Mkata River basin on the northern edge of the Mikumi National Park is its name Wami. Due to deforestation and climatic changes in the region the runoff decreased.Wami river is the southern border of the Saadani National Park, the only coastal National Park in Tanzania.

Kwa maelezo ya kitafiti:rivers in the Wami River Basin
 
Wanasubiri watu wafe kisha wapate masalia ya pesa za rambi Rambo wakaongezee kwenye ujenzi wa reli ya mwendo kasi
 
Back
Top Bottom